Ukita nchi kuwa na uchumi imara na makini lazima iwe imepita ktk changamoto ya umasikini ukitaka jeshi liwe na nguvu imara,lazima liwe liliwahi kushindwa vita.Ukitaka kufaulu maisha,lazima upitie changamoto.
Na ukitaka kupata mapenzi ya kweli lazima ufuate kanuni na taratibu za mapenzi ambazo ndio dira ya kukuongoza na kukufikisha kwenye ndoto.
Ni wengi waloumizwa na mapenzi,ni wengi waloteseka na mapenzi,ni wengi wenye majeraha yasipona maumivu.
Maumivu ya mapenzi hayaelezeki,hayasimuli,ni siri kati ya mgonjwa na maumivu yenyewe.Ni uongo na kujidanganya kuwa utaweza kununua mapenzi ya kweli kama ununuavyo gari au nyumba au nguo au chochote kile.
Mapenzi ya kweli huzaliwa katika upendo wa kweli na hauihitaji pesa,utajiri,dini,rangi wala kabila.Pesa inaweza kununua mapenzi lakini pesa haiwezi kununua upendo ambao ndio mapenzi ya kweli.
Ashakum si matusi,utakapo toa pesa na kuhonga mapenzi utapata kitu kiitwacho " sex'' lakini ule upendo unaozaa mapenzi ya kweli yanayopelekea ndoa ya kudumu hautokuwepo kwani ni sawa na kuuwekea kumpa kuku aatamie yai la mbuni.
Mapenzi yamejengwa katika ukubwa ambao haulingani na thamani ya pesa.Ni masikini wangapi wameoana au kuolewa na matajiri,ni wenye elimu wangapi wameona na wasio na elimu ?Huo ndio ukubwa wa mapenzi,usiofanana na chochote kile.
Kweli wengi tunafanya kazi kwa juhudi zote ili tupate pesa za kupatia mapenzi lakini ni kweli tunapata mapenzi ya kweli au tunaishia kufanya mapenzi na mwisho wa siku kusalitiana,na kuachana vibaya.Hakuna soko la mapenzi duniani ambalo utafika na kuyanunua.
Mapenzi ya kweli hujengwa ktk mfumo wa mwili wa binadamu ambao upo ktk sehemu iitwayo upendo,upendo unatokea ktk roho au moyo wa binadamu.
Kwa kawaida upendo hauna macho wala masikio.
Upendo una akili na ufahamu peke yake.Hivyo basi,yule utakae muona mbaya,wenzako watamuona mzuri na yule utakae muona mzuri wenzako watamuona mbaya,hapo mapenzi hayana macho.Yule mchafu kwako,kwa wenzako ni msafi.
Mapenzi siyo sawa na bidhaa sokoni eti utoe hela uipate,laa.Mapenzi ni sawa na upofu,lakini upofu wenye maono.Hata ufanye nini,kwa wenye mapenzi ya kweli huwezi kuwatenganisha kwani hawakuyanunua sokoni wala dukani,wanatambua thamani ya mapenzi yao.
Muda mwema wote.