SoC03 Utata wa mkataba wa utoaji huduma ya umeme kati ya mteja na Tanesco

Stories of Change - 2023 Competition
May 5, 2023
7
5
UWAJIBISHWAJI WA SHIRIKA LA UMEME TANZANIA - TANESCO

Bila shaka tunatambua na kuona jinsi shirika letu la Umeme Tanzania ambavyo limekuwa likiendelea kutanua wigo wake wa kutoa huduma na kuja na mpango wa kuwafikia wakazi/wananchi waishio vijijini katika mpango wake wa ugawaji wa nishati ya umeme vijijini (REA), sambamba na hilo changamoto hazikosi ambazo zimekuwa kero na pengine hazijapatiwa majibu kwa muda mrefu ukiachilia mbali wawakirishi wetu Bungeni kutoyasemea au kuiagiza Wizara husika ya Nishati na Madini kushughulikia kero hizo ambazo baadhi yake nitazitaja hapa chini.

Hoja yangu kubwa;
Pamoja na huduma nzuri shirika la umeme linayoitoa lakini nimekuwa na swali ambalo sijapata majibu. Kwa kutambua kwangu ni kwamba biashara yoyote ya kutoa huduma kati ya mteja na mtoa huduma lazima kuwe na mkataba unaoonyesha masharti na muongozo wa huduma. Je, kwa nini TANESCO kupitia Wizara ya Nishati na Madini mpaka sasa haina mkataba wa utoaji huduma wake (Hii nazungumzia kwa watumiaji wa umeme wa majumbani/single phase) japo sijui utaratibu ukoje kwa makampuni na Taasisi zingine, Mkataba unaoweka wazi HAKI ZA MTEJA KISHERIA na HAKI ZA MTOA HUDUMA KISHERIA.

Hapa nikiwa na maana kwamba mteja anapohitaji kuunganishiwa huduma ya umeme kwenye eneo lake kinachofanyika kiofisi ni kupeleka ramani au wao mafundi wa Shirika kuja kuchora ramani ya jengo/banda ambalo linahitaji kuingiziwa huduma ya umeme (hapa mteja analipia gharama hizo) baada ya hapo kuna ujazaji wa fomu ya kubainisha eneo la Mteja, anuani na mengine ambayo hayabainishi masharti ya mkataba kwa mteja/mtoa huduma endapo itatokea ukiukwaji wa mkataba au hitirafu kwa sababu ni mifumo ya umeme ndiyo inayotumika.

Hii imekuwa imepelekea kutokea sintofahamu kubwa pale mteja anapopata hitirafu au kuunguliwa na vifaa vyake vya umeme sababu iliyosababishwa na Shirika la Umeme kwa makusudi au bahati mbaya kutokana na kukatika katika kwa umeme kusiko kwa kawaida. Mfano; Mimi nikiwa mhanga mwaka juzi na pia mwaka huu tuliunguliwa vifaa vya ofisi vingi na hivyo hivyo kwa majirani zetu pia karibia mtaa mzima tulipata hasara iliyotokana na uzembe wa makusudi wa mafundi wa Tanesco ambao walipewa taarifa za kuwa, kuna mojawapo ya Transfomer pale mtaani inahitirafu imekuwa ikitoa cheche kwa masaa kadhaa lakini hawakufika na badala yake Transformer hiyo kulipuka na kupelekea vifaa vya umeme katika mtaa wetu kuungua kwa kiasi kikubwa kulikotokana na kuongezeka kwa umeme mkubwa katika njia ya umeme (High voltage).

Baada ya kupata kadhia hiyo tulijaribu kuwasiliana na mamlaka husika/ofisi za shirika kupata ufumbuzi wa tatizo hilo lakini majibu yao walisema “Ikiwa vimeungua usiwashe tena umeme mpaka mafundi watakapo fika site kufanya marekebisho ya tatizo lililopo, kuhusu vifaa SHIRIKA HALINA UTARATIBU WA KUMLIPA MTEJA”

Nini kifanyike
Serikali kupitia Wizara ya Nishati na Madini ipitie upya sheria na sera zake zinazoliongoza Shirika la Umeme Tanzania ikiwa ni pamoja na kuandaa utaratibu mpya wa kuwakutanisha wadau tofauti (Wateja) nikiwa na maana ya kuwa wateja wanaotumia umeme mkubwa/viwandaji (Three phases nk) na wateja wa umeme wa majumbani (Single phase nk) ili kufanya maboresho ya kuunda sheria/Mkataba utakaokuwa na tija kwa pande zote mbili. Nikiwa na maana kuwa endapo itatokea Mteja kasababisha hasara kwa mtoa huduma basi sheria kutoka katika kipengele flani cha mkataba kisimamiwe na mhusika achukuliwe hatua za kisheria kama ilivyoainishwa.

Vilevile endapo mtoa huduma atasababisha hasara kwa mteja basi sheria kutoka katika kipengele flani cha mkataba kisimamiwe na mhusika achukuliwe hatua za kisheria kama ilivyoainishwa. Hii itakuwa ni hatua kubwa katika ustawi wa majukwaa ya haki kwa pande zote, si kama ilivyo sasa kwamba mtoa huduma (Tanesco) ndiye mwenye mamlaka ya kumchukulia hatua za kisheria mteja yeyote na wakati wowote endapo litatokea tukio la mteja kusababisha hasara iwe ni kwa bahati mbaya au makusudi.

Pia jambo jingine ni kwamba kumekuwa na kero kubwa hasa kwa watoa huduma kwa wateja (customer services) wa Tanesco mara wapatapo taarifa za hitirafu au matengenezo kutoka kwa wateja kutoyaripoti kwa wakati na mara nyingine kutokupokea kabisa simu ambazo namba hizo zimetolewa na mamlaka husika kwa ajili ya kuwasiliana na watoa huduma wake. Hivyo ni vema Shirika kupitia wafanyakazi wake wakachagua ni njia ipi nzuri ya kuwasiliana na wateja wake ikiwa hawawezi kutumia njia ya mawasiliano ya simu au kuajiri wafanyakazi waliopitia mafunzo ya huduma kwa wateja (Customer care) wenye weledi na kazi yao.

Vilevile shirika liwekeze kwenye teknolojia za kisasa zenye kuwezesha utambuzi wa matatizo/hitirafu katika mfumo wa umeme kwa haraka badala ya kuwa mafundi wanazunguka huku na huko kutafuta chanzo cha tatizo hali inayopelekea kukosekana kwa huduma ya umeme kwa muda mrefu, jambo ambalo linadhoofisha shughuli za uzalishaji mali na kukua kwa sekta ya Uchumi Nchini kupitia nishati ya Umeme.
 
Andiko lako ni bora kabisa, ila jf member wake hupendelea nyuzi za kimasihara, ushoga nk. Hii huwezi pata wachangiaji!
 
Back
Top Bottom