SoC03 Kero mbalimbali kwa watumiaji nishati ya umeme na maji

Stories of Change - 2023 Competition

Mamshungulii

Senior Member
May 3, 2023
124
66
Wakazi wengi wa mikoa tofauti tofauti nchini Tanzania wamekuwa wakilalamikia Shirika la Ugavi Umeme Tanzania (TANESCO) kwa kuwacheleweshea kuwafikishia huduma za umeme katika maeneo yao llicha ya kuwa wamelipia gharama zote za upatiwaji wa huduma hiyo.

Watumishi wa TANESCO huwahamasisha wananchi kujaza fomu za maombi ya umeme na kulazimu watu kuweka mifumo ya waya za umeme katika nyumba zao lakini inaweza kuchukua mwaka hadi miaka mitano bila kufanikisha kupatiwa umeme.

Kwamfano kutoka JAMIIFORUM Instagram wameeleza “Wenyeviti wa Vitongoji 3 pamoja na Wajumbe 7 wa Serikali ya Kijiji cha Uhambule , Halmashauri ya Wanging’ombe wamejiuzulu kwa madai ya kuwa Serikali imeshindwa kupeleka Nishati ya Umeme kwenye maeneo yao licha ya kuahidiwa kwa muda mrefu Mkuu wa Wilaya ya Wanging'ombe, Claudia Kitta amewataka viongozi hao kurejea kwenye majukumu yao kwa kuwa serikali inaendelea kutoa huduma hiyo na imekusudia kufikisha umeme kwenye kila kitongoji Amesema, "Hili linatusikitisha lakini mpango wa Serikali ulianza kwa awamu na upande wa vitongoji tayari serikali imeanza kutekeleza".

Ni suala lililo wazi kuwa nishati ya umeme ni ya muhimu sana katika Maisha yetu ya kila siku,ambapo binadamu huitumia nishati hiyo kwenye matumizi mbalimbali kama vile nyumbani ,mahospitalini, viwandani ,sehemu za ibada na kwenye shughuli mbalimbali za uzalishaji.

Shirika la Ugavi wa Umeme Tanzania (TANESCO) ndilo lenye dhamana ya kuzalisha na kusambaza umeme kwa upande wa Tanzania bara. Watumiaji wa huduma za nishati na maji mara nyingi wanakutana na changamoto kadha wa kadha wanapotumia huduma hizo.Mfano wa changamoto hizo ni kamavile:

• bili kubwa za maji,au umeme kuliko matumizi halisi,
• kusitishiwa huduma bila taarifa,
• migogoro ya usomajii wa mita na mita mbovu,
• uchakachuaji wa bidhaa za pettroli ,
• kuchelewa kuunganishiwa huduma za maji au umeme ,
• watoa huduma kushindwa kutoa mwitikio wa kuridhisha kwa maswali au malalamiko toka kwwa wateja
• uharibifu unaotokea majumbani kutokana na maji machafu na hitilafu za umeme Pamoja na changamoto nyingi.

EWURA CONSULTATIVE COUNCIL ,EWURA CCC ni Baraza la ushauri la Watumiaji wa huduma zilizodhibitiwa na EWURA ,yaani ni huduma za maji na nishati.Hii ni taasisi ya Umma iliyoanzishwa chini ya kifungu namba 30 cha Sheria ya Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za nishati na maji yam waka 2001,sura ya 414,Kifungu namba 31 cha sheria hiyo kimeeleza kazi anuai za EWURA CCC ambapo miongoni mwake kifungu namba 31 (1)(a) cha sheria hiyo kinaonesha kazi mojawapo ni kuwakilisha watumiaji na kusimamia maslahi ya watumiaji wa huduma zinazodhibitiwa na EWURA .

EWURA CCC na EWURA zote ni taasisi za serikali zinazojitegemea ambazo zimeundwa kisheria,EWURA inategemea maoni ,ushauri kutoka EWURA CCC juu ya maslahi ya watumiaji kama vile kwenye michakato ya uandaaji na upangaji wa bei,kanuni za ubora wa huduma na kushauriana na watoa huduma,wizara na mawaziri wa sekta zinasimamia huduma za maji na nishati.

Pia Kanuni ya 4(a)ya kanuni za utatuzi wa migogoro za Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji EWURA, Tangazo la serikali Na 428 la mwaka 2020, linaelezea kuwa mtu yeyote mwenye lalamiko lake anaweza kuwasilisha lalamiko lake EWURA dhidi ya mtoa huduma kwa kujaza fomu iliyo katika kanuni tajwa hapo juu.Na wanaoweza kuwasilisha lalamiko kwa niaba ya mlalamikaji ambao ni EWURA CCC au mwakilishi yeyote aliyeruhusiwa na mlalamikaji kuwasilisha lalamiko.

Mlalamikaji anaweza kupitia njia tatu kuwasilisha lalamiko lake
a) kuwasilisha lalamiko yeye mwenyewe
b) kupitia EWURA CCC
c) Kwakutumia mwakilishii yeyote aliyemruhusu kuwasilisha lalamiko

Pia kutokana na Mkataba wa huduma kwa wateja wa TANESCO ukurasa wa 8 ,sehemu E unaelezea kuwa TANESCO ina wajibu wa kutoa taarifa sahihi kuhusiana na huduma wanazozitoa kwa wateja wao.Mkataba huu unaonesha wazi kuwa ni haki ya mteja kupatiwa taarifa zote sahihi za huduma anayotumia pindi panapotokea tatizo lolote kutoka kwa mtoa huduma.

Ukurasa wa 4 wa mkataba wa huduma kwa wateja wa TANESCO unaeleza kuwa ,kama mteja amejaza fomu ya kuomba huduma ya kuungiwa umeme na kuwasilisha viambatisho vyote muhimu vinavyotakiwa,muda ufuatao wa kupewa makadirio ya gharama utazingatiwa:

a. Ndani yaku 7 za kazi iwapo miundombinu iliyopo inaweza kutumika (ndani ya mita 30 kwenye nguzo iliyo karibu)

b. Ndani ya siku 10 za kazi kama ujenzi wa njia ya umeme unahitajika(ambao siyo zaidi ya mita 100 kutoka kwenye nguzo iliyo karibu)

c. Ndani ya siku 14 kama mfumo mpya wa usambazaji unahitajika kujengwa au uunganishwaji wa mfumo kwa wateja wenye viwanda au biashara kubwa.

Kwa upande wa maji ,kanuni namba 54 (1)(b) ya kanuni ya ubora wa huduma za majisafi na usafi wa mazingira yam waka 2020,mtoa huduma anapaswa kumuunganishia mteja mppya huduma yam aji ndani ya siku 7 za kazi baada ya malipo kufanyika .Pia kanuni hiyo imetaja fidia ya mteja endapo ndanii ya siku 7 maunganisho yatakuwa hayajafanyika,basi mteja atatakiwa kulipwa shilingi elfu 15,000/= za kitanzania kama fidia ya msingi na 5000 kwa kila siku inayoongezeka.

HAKI NA WAJIBU KWA MTUMIAJI WA HUDUMA ZA NISHATI NA MAJI
• Matumizi halali ya huduma na mazingatio ya taratibu zote kwa mtumiaji
• Kulipia Ankara kwa wakati
• Kutoa taarifa kwa watoa huduma ili kupatiwa ufafanuzi
• Kutafuta taarifa sahihi
• Kutunza miundombinu
• Kudai fidia
• Kujielimisha
• Wajibu wa kulalamika

HAKI ZA MTUMIAJI WA HUDUMA ZA NISHATI
Haki ya:-
 Kupata huduma ya msingi
 Kufidiwa
 Kupata rarifa
 Kuchagua
 Kusikilizwa na kuwakilishwa
 Kuelimishwa
 Usalama na faragha

CHANGAMOTO ZA WAPATIWA HUDUMA KUPITIA EWURA
a) Watumiaji wa huduma zinazodhibitiwa na EWURA hawawezi kupeleka kesi zinazohusu huduma za maji na Nishati kwenye mahakama.heria ya Mamlaka ya udhibiti wa huduma za Nishati na maji inazitaka kesi zote zinazohusu huduma ya nishati na maji zinazodhibitiwa na kushughulikiwa na EWURA .Ingawa ,hukumu ya EWURA inaweza kukatiwa rufaa Kwenda baraza la ushindani FCT(jukwaa la watumiaji)

b) Hakuna sera ya Taifa ya kumlinda mtumiaji hivyo kunakwamisha utetezi mzuri kwa wapatiwa huduma , hivyo kuna haja ya kuwekwa sera ya mtumiaji ili kuleta tija katika huduma za nishati na maji.

InShot_20230623_044823786.jpg
 
Back
Top Bottom