marandu2010
JF-Expert Member
- Aug 7, 2010
- 1,199
- 435
Ukiwa na nyumba au kiwanja bila hati miliki haiwezi kukusaidia kupata mkopo, naomba wakuu mnisaidie mchanganuo wa gharama za kuipata hati miliki na taratibu zake, ninaanzia wapi na kuishia wapi?
Natanguliza shukurani zangu wakuu
Natanguliza shukurani zangu wakuu
Utaratibu
1. Pata barua ya utambulisho toka kwa mjumbe wako wa shina.
2. Andika barua kwa mkurugenzi wa Halmashauri kumuomba kibali cha kupimiwa (survey) eneo lako. Barua hiyo inatakiwa kupitia ofisi ya serikali ya mtaa na ofisi ya afisa mtendaji kata.
2. Fikisha barua hiyo pamoja na vithibitisho vya umiliki wa kiwanja chako (makubaliano ya mauzo au urithi) kwenye ofisi ya Serikali ya Mtaa pamoja na barua ya kuomba kupimiwa eneo. Serikali ya Mtaa itakukata kodi ambayo ni asilimia 10 ya thamani ya kiwanja. Serikali ya Mtaa itakutengenezea hati ya umili na kukupa ndamba ya kiwanja. Hati hii unaweza kuitumia kulipa kodi ya ardhi kila mwaka.
3. Pitisha barua hiyo ngazi ya kata. Hata hakuna makato zaidi ya "kamchango" kadogo ka ofisi kama sh. elfu 5 hivi. Huwa kuna michango ya shuguli za maendeleo etc kupitia huduma kama hizi.
4. Peleka barua hiyo kwa Mkurugenzi wa Halmashauri. Mkurugenzi atasubiri Baraza la madiwani likae ili kupitisha ombi lako iwapo eneo hilo halipo katika mpango wa matumizi mengine zaidi ya residency etc.
5. Baada ya kupata kibali toka kwa Mkurugenzi, tafuta kampuni ya survey wakupimie na kampuni hiyo itawasilisha ombi la title deed wizara ya ardhi kupitia kwa mkurugenzi.
6. Wizara ya ardhi itakukabidhi title deed iliyokamilika.
Kama umepata letter of offer maana yake kwamba hapo ofisi ya ardhi ya manispaa wanaandaa file mbili ambazo zote zinafanana yaani moja copy yako na nyingine nadhani itabaki kwa upande wa serikali imeandikwa CERTIFICATE OF OCCUPACY (Under section 29), THE LAND ACT, 1999 (NO. 4 OF 1999) ambazo watakupa uzipeleke kwa mwanasheria kuthibitisha kwamba wewe umekubali terms and condition.
Unarudisha Manispaa ambao watazipeleka (au unapeleka mwenyewe) ofisi ya Kamishina wa Ardhi ambapo utalipa stamp duty sh. 500 (mia tano ambayo hata hivyo itakuwa tayari imelipwa wakati kiwanja kinanunuliwa kama inavyoonekana hapo chini) kisha unaandikishwa kwenye daftari na kupewa siku maalumu ya kurudi kuona kama hiyo CERTIFICATE OF OCCUPANCY (ndio hati yenyewe) kama imesainiwa na Kamishina wa Ardhi pia inabandikwa na ramani ndogo ya viwanja vilivyopo eneo lako of which cha kwako kinawekewa alama nyekundu plus namba ya hati, ukubwa na vitu kama hivyo. Kama ikishasainiwa tu unapewa hati yako kabisa na unasepa zako.
Hiyo laki 350,000 hapo ni utata kwani gharama ya kiwanja hicho ime-include mambo mengi, embu check letter of offer yako uone jinsi mchanganuo wa gharama ya kiwanja kama ilivyo kwa mnunuzi wa kwanza, ukicheck utaona kuna
- Premium (hiyo ndio gharama ya kiwanja wanakuwa wameweka amount
- Fees for certificate of occupancy ambayo ni 3000 ila hata kama imepanda haiwezi kuwa juu sana (hii ilikuwa 2006)
- Registration fees ni 2106
- Survey fees 24,570
- Deed Plan fees 6,000
- Stamp duty on Certificate and Duplicate 1,000
- Land rent ya mwaka ambao amenunua kiwanja 11,000 (baada ya hapo kila July mhusika unakwenda kulipa
Hivyo ukijumlisha zote kuanzia premium mpaka hizo gharama nilizokuonyesha unapata gharama halisi ya kiwanja na ipo indicated kwenye letter of offer. Let say, kama gharama ya kiwanja ni milion moja (ambayo ndio imeandikwa premium kwenye letter of offer) maana yake gharama ya kiwanja jumlisha hizo cost ndogondogo.
Ukisoma hivyo vigharama utagundua kila kitu kilishalipiwa na mnunuzi wa kwanza ambapo kimsingi kilichofanyika ni kubadili jina tu condition zingine zinabaki vilevile, so hati ni bure in this case unless taratibu ziwe zimebadilika, gharama ambayo utaingia ni hiyo ya mwanasheria ambayo ukienda utalipa labda mwekundu anagonga mhuri na kupiga sahihi na wewe unapiga sahihi mbele yake.
Tafuta ofisi ya Kamishina wa Ardhi, huwa zipo kikanda upate taratibu.