Habari wana JamiiFrm.
Naombeni msaada,mimi ni mkazi wa Arusha,nina kiwanja changu chenye vyumba vyangu ila wakati wa kununua nilimtumia mchumba wangu akailipie kiwanja kwa jina lake.
Nataka nikiwekee hati miliki ya kiwanja hicho na nyumba yake.
Naomba mwenyekujua anijuze njia ya kufanya na Garama ya kutimiza lengo hilo.
NAMALIZIA KWA KUWASHUKURU,
ASANTENI
Nawakilisha kwenu kwa msaada.
Pole sana mleta mada hii.Nianze kwa kusema kuwa wewe na mchumba wako hamkuwa na makubaliano ya kisheria kuweza wewe kumwamini na kununua kiwanja ambachao mlikubaliana kiandkikwe jina la mchumba wako.Kwa ufupi wewe huna haki juu ya kiwanja hicho.Mwenye haki ni mchumba ni wako.Wachumba hawatambuliki kisheria kama wana ndoa,zaidi itajulikana kama ni marafiki wa kawaida.
Kama nilivyosema awali wewe huna haki na kiwanja hicho isipokuwa kilichopo hapa ni wewe na mchumba wako kuaminana,ambapo huwezi kupata nguvu ya kisheria endapo mchumba wako akaamua kujimilikisha na kukutoa nje ya umiliki unaosema.Huna ushadi kuthibitisha kama kweli wewe ulitoa hela kununua kiwanja hicho.
Pili hujaeleza kwa kipindi hiki kama unaishi na mchumba wako kama mume na mke.Kama mmekwisha kuoana ama kwa sheria za mila au kwa sheria ya ndoa ya mwaka 1971.Basi unapashwa kukubaliana na mkeo (kama ni wanandoa) juu ya jambo hili na namna ya kuliweke.Jambo linawezekana na ni rahisi sana kufikia muafaka na hivyo kupata aidha umiliki wa pamoja(mume na mke) au umiliki wako binafsi(mume)
Sheria ya ardhi iko wazi kabisa ,tatizo ni urasimu wa watendaji wetu,nashauri kwanza uwe na hati ya mauziano ya kiwanja hicho,pili upate muhtasari wa serikali ya kijiji au mtaa,tatu eneo lako lipimwe (watu wa ardhi au wanaotambulika kisheria) na kukewa bicons ili liweze kuingizwa katika ramani ya mji.Baada ya mambo haya kukamilika,utapata offer ya kiwanja ambayo kama mtakuwa mmekubaliana na mchumba wako/mke itakuwa kwa majina ya wote wawili au jina lako pekee.
Offer hiyo itakuwa na masharti fulani ikiwa ni pamoja na kuliendeleza eneo hilo,kitu ambacho wewe umekifanya tayari.
Kama offer utakuwa nayo,basi utapewa aidha faili lako kutoka ofisi za ardhi ili uende nalo au litatumwa Moshi ambako offer hiyo itasajiliwa na Kamishina wa Ardhi kanda,na baaada ya siku kama tatu hadi wiki moja utapata Title Deed unayoitaka. Kumbuka Moshi hakuana ushuru au kitu cha kulipia, ni bure. Kila kitu utakuwa umelipia katika ofisi za Ardhi kabla ya kwenda Moshi.
Aidha mchakato huu wote unahitaji hela hasa hasa katika upimaji wa eneo lako.Kama utaona gharama ni kubwa jaribu kutafuta marafiki wenye uhitaji wa kupimiwa maeneo yao walio karibu na wewe ili muweze kuchangia gharama hizo. Hivyo jiandae kwa gharama hizo.