Chama cha Mapinduzi chaanza kukabidhi Ilani Mpya Kwenye Matawi Nchi Nzima

Filosofia ya Rorya

JF-Expert Member
Sep 20, 2021
3,213
3,594
Chama Cha Mapinduzi kimeanza kugawa Ilani yake mpya na sasa kimefikia ngazi ya chini kabisa ya matawi toka juu.

Haikufahamika mapema kama wadau wengine wa chaguzi vikiwemo vyama vya siasa navyo japo vimekwishaandaa Ilani zao au la.

MNEC mmoja wa CCM alikaririwa akisema "CCM kina utaratibu wa kuanza mchakato wa uchaguzi mpya mara tu serikali mpya inapoapishwa kuanza kazi" kwamba hakisubiri hadi mwaka wa uchaguzi uwadie, kwamba kwa CCM kila mwaka ni mwaka wa uchaguzi.

Binafsi nadhani yapo ya kujifunza kwa CCM 100% na yapo ya kulaani 100% pia, ili kutengeneza mustakabali mzuri wa ustawi na ushamiri wa shughuli za kisiasa nchini.

Tupiganie uzingativu wa tunu za taifa majira haya ili tuwe na amani na utangamano katika vipindi hivi vya mpito kwa taifa vya 2024 na 2025. Nahitimisha kwa kaulimbiu hizi:-

Kidumu Chama Cha Mapinduzi.

Muungano wa Watu Siyo wa Serikali.

Haki Sawa Kwa Wote.

Peoples Power.
 
Ccm inashangaza sana inasema imewaletea wananchi maendeleo inasema inapendwa lakini inaogopa UCHAGUZI na kwenye Uchaguzi inatumia Katiba mbovu na Tume isiyo huru kusimamia Uchaguzi inatumia Vyombo vya dola kuvitisha vyama vya Upinzani Inaanza kampeni mapema kabla ya Muda wake na Tume yao ya Uchaguzi ipo kimya Msajili wa Vyama ambaye ni kada wa ccm ipo kimya
Je Kupendwa kwa ccm kupo wapi wakati inashida kwa kucheza RAFU?

Sent from my SM-A145R using JamiiForums mobile app
 
Tuyapinge mabaya yake bila woga, mema yake tuige bila hiana.
 
Chama Cha Mapinduzi kimeanza kugawa Ilani yake mpya na sasa kimefikia ngazi ya chini kabisa ya matawi toka juu.

Haikufahamika mapema kama wadau wengine wa chaguzi vikiwemo vyama vya siasa navyo japo vimekwishaandaa Ilani zao au la.

MNEC mmoja wa CCM alikaririwa akisema "CCM kina utaratibu wa kuanza mchakato wa uchaguzi mpya mara tu serikali mpya inapoapishwa kuanza kazi" kwamba hakisubiri hadi mwaka wa uchaguzi uwadie, kwamba kwa CCM kila mwaka ni mwaka wa uchaguzi.

Binafsi nadhani yapo ya kujifunza kwa CCM 100% na yapo ya kulaani 100% pia, ili kutengeneza mustakabali mzuri wa ustawi na ushamiri wa shughuli za kisiasa nchini.

Tupiganie uzingativu wa tunu za taifa majira haya ili tuwe na amani na utangamano katika vipindi hivi vya mpito kwa taifa vya 2024 na 2025. Nahitimisha kwa kaulimbiu hizi:-

Kidumu Chama Cha Mapinduzi.

Muungano wa Watu Siyo wa Serikali.

Haki Sawa Kwa Wote.

Peoples Power.
Ilani za uchaguzi za CCM ni kikwazo cha maendeleo
 
Kipindi Cha dhalimu magu alikuwa anasema uchaguzi ukiisha siasa zinahamia bungeni na wanaccm wakawa wanashangilia. Sasa sijui huyu anasema Nini?
 
Back
Top Bottom