Usiku wa deni haukawii kukucha, TANESCO tunawasubiri Februari 16, 2024

Mla Bata

JF-Expert Member
Jan 24, 2013
6,764
13,815
Wasalaam,

Zile mbilinge mbilinge, sarakasi na maigizo ya kuwachomoa wakina Maharage Chande na kina "kipara", matamko yasiyo kwisha na sababu lukuki zisizo za msingi za kukosekana kwa umeme wa uwakika katika nchi yetu ya "tanzagiza" yamefika ukingoni baada ya ahadi ya "mama Abduli" ya kumaliza kero ya umeme ifikapo tarehe 16 February 2024.

Ikiwa ni tarehe 15 ya February ni takribani masaa pungufu ya 24 kufikia tarehe 16, Je tutegemee ngonjera za kila siku na sababu zisizo na kichwa wala miguu au tujipe matumaini ya kuiona nchi ya ahadi?

USIKU WA DENI HAUKAWII KUKUCHA!

Wasalaam.

Tan 1.jpg
tan 2.jpg
 
AHADI ISIYOTEKELEZWA,NI MZIGO WA LAWAMA
1.Tuliambiwa,tatizo la umeme ni upungufu wa maji kwenye mabwawa,Mungu akaleta mvua ya kutosha,bado ikatafutwa sababu nyingine.
2.Tuliambiwa,tatizo litaisha tukiwasha mtambo katika mradi mpya wa bwawa la Nyerere,siku zikifika,wanasogeza tarehe mbele,utasikia sababu zingine,Mwezi Machi ndio shida itaisha kabisa..

Katika aibu,Serikali ione aibu ya kushindwa kujisimamia kwa kukosekana kwa umeme wa uhakika,huku Viongozi wakijitoa ufahamu kama vile ni suala dogo tu.,huku wakujua ukuaji wa uchumi unategemea umeme.
Wanànchi wanawangalia tu,mnatoa sababu zinazobadilika badilika kila siku bila hata aibu.
Mbona kama mnashindwa kudhibiti mambo yanayowaumiza wananchi;mnaacha bei zinapanda kiholela,hata hatua za udhibiti wa bei za bidhaa.
Hili la upungufu wa umeme tunawasubiri.
 
Ikifika Tarehe Hiyo Watakuja Na Sababu Ambazo Huwezi Amini
Maana Mvua Zimejaza Mabwawa Yote Na Bado....

Kama SGR Imekalishwa Chini Na CCM Watashindwaje Umeme
Kwanza Kauli Tu Ya Kusema Bei Haitapungua Hata Mashine Zote Zikifanya Uzalishaji
 
Wasalaam,

Zile mbilinge mbilinge, sarakasi na maigizo ya kuwachomoa wakina Maharage Chande na kina "kipara", matamko yasiyo kwisha na sababu lukuki zisizo za msingi za kukosekana kwa umeme wa uwakika katika nchi yetu ya "tanzagiza" yamefika ukingoni baada ya ahadi ya "mama Abduli" ya kumaliza kero ya umeme ifikapo tarehe 16 February 2024.

Ikiwa ni tarehe 15 ya February ni takribani masaa pungufu ya 24 kufikia tarehe 16, Je tutegemee ngonjera za kila siku na sababu zisizo na kichwa wala miguu au tujipe matumaini ya kuiona nchi ya ahadi?

USIKU WA DENI HAUKAWII KUKUCHA!

Wasalaam.

View attachment 2904416View attachment 2904417
Ikiwa ni tarehe 15 ya February ni takribani masaa pungufu ya 24 kufikia tarehe 16, Je tutegemee ngonjera za kila siku na sababu zisizo na kichwa wala miguu au tujipe matumaini ya kuiona nchi ya ahadi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom