Kumnyima mtoto kazi za nyumbani ni kumbomoa! Atapata shida kujitegemea na kuishi kwenye jamii, Baadhi ya wazazi wenye Pesa acheni huu umbumbumbu

sky soldier

JF-Expert Member
Mar 30, 2020
5,408
19,033
kisingizio cha wazazi hawa huwa “Sitaki mtoto wangu apitie Maisha magumu niliyopitia”, ni kweli huenda mzazi ulikuwa unanyanyaswa utotoni kwa kufanyishwa shughuli zaidi ya uwezo wako lakini sio sababu ya kumnyima mtoto wake shughuli za kufanya.

Mzazi unaweza kuweka elimu iwe kipaumbele kwa mtoto wako lakini bado sio sababu , matokeo yake mtoto anaweza kuwa msomi aliyeajiriwa sehemu nzuri ama ana biashara zake lakini kwasababu hukumzoesha kazi za nyumbani unakuta huko chumbani kwake Pamoja na utu uzima wake hatandiki kitanda, vyombo vipo chini ya kitanda, chumba chake kipo rafu, n.k. jamii nayo inamuona mtu wa ajabu maana hata hajali hata mazingira ya nyumba yake, Wewe mzazi ndie umetengeneza hili bomu kwa kulea watoto kijunia juniour.

hujamzoeesha mtoto kazi za nyumbani ila kuna kioindi ataenda chuoni ama boarding umri ushaenda ni ngumu kuzoea kazi hizi, Ni nani atapenda kukaa na mwanao mzembe wa kufanya shughuli zake ?

Kufanya shughuli hizi kunawaandaa mapema Watoto kujiandaa kisaikolojia kwamba kazi ndio tegemeo kubwa kwa watu wengi kuishi hapa duniani (asie fanya kazi na asile), kuanzia chakula wanachokula, mavazi wanayovaa, sehemu ya kuishi, elimu, n.k hivyo vitu vyote vina gharama yake sio bure, kwa mchango wao mdogo wa shughuli za nyumbaniwanapata akili kwamba angalau wanachangia kitu ili wale, hii huwa inasaidia sana kuondoa jinamizi la uvivu, kazi kazi!!

Kazi hizi zinasaidia pia watoto kuweza kuishi sehemu mbali mbali, hata sisi iwe mimi au wewe tunapenda Watoto wa ndugu zetu wakija hata kutusalimia wawe bize asubuhi wanafanya usafi wa nyumba, kama una gari anakuoshea, awe smart hata majirani wajue nyumba flani ina watu smart, mazingira yawe safi, n.k. sio mtu anakuja kwako hata chumba tu kusafisha ni ishu.

Mtoto anapofika miaka hata mitatu muanzisha vikazi vidogo vidogo chini ya uangalizi, hadi anafika miaka 12 awe ameshazoea kufanya hizo kazi hata bila ya kuambiwa.
 
Kweli aisee mimi nilidekezwa sana nakuja kujifunza kufua form one wiki ya orientation😂

Kupika ndo hivyo, sijui hata kusonga ugali hata kumenya karoti😂

Mambo ya kufagia sijui kulima uwanja yote nilijifunzia shule, nilipata tabu sana

Hadi kupanda daladala nilikua nakatazwa hadi nafikia la 7😂 msinione najiita mshamba

Kuna umuhimu....
 
Nakubaliana na ww mleta uzi utakuta mtoto mpka anamaliza secondary hajui kufua nguo zake mwenyewe ama kupika chakula kama ubwabwa na ugali mimi wangu kufua nguo zake, kupasi na kupika anajifunza akiwa na miaka 4 akifika miaka 11 hata chakula cha familia anajua kupika.. Yaani hadi raha.

Niliwahi kukaa na mdogo wangu wa kiume wa mwisho akisoma secondary na kuishi kwangu alijifunza kila kitu mpka anamaliza alivoenda home kijijini walishangaa kuona anajua kazi zote hasa kupika na kuosha vyombo ana kuchota maji nakumbuka mama alinipigia cm na kushangaa kwamba mimi nimefanyaje mpka mda wangu akawa hivi?

Nilimjibu tu kiufupi kuwa ukikubali kuisha kwangu lazima pia ukibali kufuata masherti yangu la sivyo utaondoka kwangu.. Huwezi kuishi kwangu harafu uishi utakavo no!
 
Nimeshuhudia mtoto wa ndugu yangu mwenye miaka 10 alikuja kunitembelea likizo lakini hatandiki kitanda, kuoga mpaka umkumbushe, kufagia uwanja nimemfundisha mimi, n.k.

Hali hii ilinifanya niwe na kiboko cha mpera ili twende sawa na nikiri hata huko kwao walianza kupiga simu nimemfanya nini mpaka aweze kujifanyia baadhi ya kazi, ila ubaya nni kwamba huko kwao hawamsimamii tena karudi vile vile, ni kweli shuleni anajiweza lakini ni aibu kama mtu hawezi kujitegemea !!.
 
kweli aisee mimi nilidekezwa sana nakuja kujifunza kufua form one wiki ya orientation😂

kupika ndo hivyo, sijui hata kusonga ugali hata kumenya karot...
Kuanza kujifunzia sekondari huwa ni ngumu sana maana na kiburi cha balehe huwa kinampa mtu jeuri ya kukataa kufanya mambo ambayo hajazoea.

Ni wachache wakifika umri huu wanajifunza kwa hiari,
 
Wazazi wengi wanawalea watoto wao kimandazi mandazi. Wanawadekeza wakidhani ndio upendo.
Mnadhani na ulimwengu utakuwa fair kwa watoto wenu kama mnavyowadekeza??

Ndio maana vitoto vya kiume vikianza mapenzi vikiumizwa vinasikiliza nyimbo ya marioo mara 60 non stop halafu vinaenda kujitundika.

Watengenezeni watoto wawe imara kimwili, kiakili na kihisia pia
 
Wenyewe wanajiita wa kushuka hata kitanda anatandikiwa na dada WA kaz
Hata vyombo mezan akimaliza Kula hatoi dada anaitwa aje atoe

Inaitwa pesa

Ila watoto WA kajamba nan
Sisi shida ndo inatufanya tujue kila kitu
Mtaani
 
tatizo huwa ni kwa watoto walio kwenye familia za kimaskini huwa wanafanyishwa kazi kuzidi uwezo wao kiasi kwamba inakuwa sio mafunzo tena bali mateso, na hawa wakiwa wakubwa wakipata pesa, baadhi yao huingia mtego wa kuwakataza watoto wao wasifanye kazi kabisa.
 
Wazazi wengi wanawalea watoto wao kimandazi mandazi. Wanawadekeza wakidhani ndio upendo.
Mnadhani na ulimwengu utakuwa fair kwa watoto wenu kama mnavyowadekeza??

Ndio maana vitoto vya kiume vikianza mapenzi vikiumizwa vinasikiliza nyimbo ya marioo mara 60 non stop halafu vinaenda kujitundika.

Watengenezeni watoto wawe imara kimwili, kiakili na kihisia pia
Mwanzoni umeandika point lakini hapo kwenye mapenzi ni kitu kingine kabisa, hata shule za kata wapo wanaoumizwa na mapenzi
 
kisingizio cha wazazi hawa huwa “Sitaki mtoto wangu apitie Maisha magumu niliyopitia”, ni kweli huenda mzazi ulikuwa unanyanyaswa utotoni kwa kufanyishwa shughuli zaidi ya uwezo wako lakini sio sababu ya kumnyima mtoto wake shughuli za kufanya.

Mzazi unaweza kuweka elimu iwe kipaumbele kwa mtoto wako lakini bado sio sababu , matokeo yake mtoto anaweza kuwa msomi aliyeajiriwa sehemu nzuri ama ana biashara zake lakini kwasababu hukumzoesha kazi za nyumbani unakuta huko chumbani kwake Pamoja na utu uzima wake hatandiki kitanda, vyombo vipo chini ya kitanda, chumba chake kipo rafu, n.k. jamii nayo inamuona mtu wa ajabu maana hata hajali hata mazingira ya nyumba yake, Wewe mzazi ndie umetengeneza hili bomu kwa kulea watoto kijunia juniour.

hujamzoeesha mtoto kazi za nyumbani ila kuna kioindi ataenda chuoni ama boarding umri ushaenda ni ngumu kuzoea kazi hizi, Ni nani atapenda kukaa na mwanao mzembe wa kufanya shughuli zake ?

Kufanya shughuli hizi kunawaandaa mapema Watoto kujiandaa kisaikolojia kwamba kazi ndio tegemeo kubwa kwa watu wengi kuishi hapa duniani (asie fanya kazi na asile), kuanzia chakula wanachokula, mavazi wanayovaa, sehemu ya kuishi, elimu, n.k hivyo vitu vyote vina gharama yake sio bure, kwa mchango wao mdogo wa shughuli za nyumbaniwanapata akili kwamba angalau wanachangia kitu ili wale, hii huwa inasaidia sana kuondoa jinamizi la uvivu, kazi kazi!!

Kazi hizi zinasaidia pia watoto kuweza kuishi sehemu mbali mbali, hata sisi iwe mimi au wewe tunapenda Watoto wa ndugu zetu wakija hata kutusalimia wawe bize asubuhi wanafanya usafi wa nyumba, kama una gari anakuoshea, awe smart hata majirani wajue nyumba flani ina watu smart, mazingira yawe safi, n.k. sio mtu anakuja kwako hata chumba tu kusafisha ni ishu.

Mtoto anapofika miaka hata mitatu muanzisha vikazi vidogo vidogo chini ya uangalizi, hadi anafika miaka 12 awe ameshazoea kufanya hizo kazi hata bila ya kuambiwa.
Juzi kati nilisikiliza kwenye jahazi yule mtoto wa likwelile alivyokuwa akilalamika maisha magumu anayopitia baada ya baba yake kufariki inasikitisha ila matokeo hayo ya kudekeza watoto kwa kila kitu.
 
Back
Top Bottom