Umuhimu wa kumjengea mtoto tabia ya kujitegemea mapema

Suley2019

JF-Expert Member
Oct 7, 2019
1,816
4,566
Na C-Sema

Wakati mwingine, wazazi na walezi tunapata wasiwasi juu ya maisha ya baadaye ya watoto wetu. Tunajiuliza: Watakuwa na maisha ya aina gani? Watakuwa watu wazima wa namna gani? Hivi watafanikiwa kielimu? Biashara?

Lakini kimsingi, sisi wazazi na walezi ndiyo watu pekee wenye jukumu la kuhakikisha kuwa tunalea watoto wetu katika mienendo ambayo tunaona ni mema, kama usemi maarufu wa wahenga usemavyo, mtoto umleavyo, ndivyo akuavyo.

Tabia ya kujitegemea, kwa kiasi kikubwa, huja kutokana na msukumo wa wazazi na namna makuzi yanavyotolewa. Ni muhimu kwa mzazi au mlenzi kuanza kwa kumpa fursa mtoto kujifanyia vitu, au mambo madogo-madogo kadiri anavyozidi kukua.

Mtoto anatakiwa aanze kujua, kwa mfano, dhana ya kunawa mikono peke yake kuanzia umri wa miaka mitatu au mapema zaidi. Mueleze kwa nini kunawa mikono ni muhimu. Mfunze kuoga pekee yake mapema. Aanze kufua nguo nyepesi kama kanga au shati la shule mapema.

Taratibu ajue akitoka shule pana kazi kadha wa kadha zinazomsubiri. Mtie moyo kwa kumsifu pindi anapojaribu kujifanyia jambo mwenyewe pasi kuambiwa. Hii itamfanya aendelee kujihusisha na jambo hilo mara kwa mara na mwishowe atavuna uzoefu katika hilo.

Heshimu mawazo ya mtoto. Watoto wetu hupenda sana kutoa maoni yao kama sehemu ya utatuzi wa changamoto za siku hata siku katika familia zetu. Zungumza na mtoto wako, kubaliana naye – lakini mpe sababu kwa nini unajua anachoshauri hakiwezekani.

Unamjengea uwezo wa kusimama pekee yake katika hoja. Mpe fursa ya kuchagua nguo anayopenda kuvaa – haya mambo madogo yanatafsiri ya uhuru wa kuamua. Huku nako ni kukuza dhana ya kujitegemea.

Upo ushahidi wa kutosha kuwa baadhi ya wazazi huwafanyia watoto wao kila kitu majumbani mwao kwamba wanawapenda sana. Lakini swali la kujiuliza ni kuwa je, utaishi na watoto wako maisha yao yote?

Mapenzi kwa watoto ni pamoja na kuwaandalia kesho yao kupitia kazi kama kufagia nyumba, kufuta vumbi madirishani, kuosha vyombo, kutandika kitanda, kujipangia ratiba ya siku, nakadhalika.

Mpe usaidizi wa masuala ambayo dhahiri ni magumu kwake. Namna ya kukabiliana na msiba, changamoto za kielimu.

The Chanzo
 
Wabongo hawajui yote hayo wao wanachojua ni fimbo tu! Fimbo ndio nyenzo kuu ya malezi kwa wazazi wa kiafrika
 
Nilitaka nikupigie kura kumbe hujaiweka kwenye shindano
 
Nilisikitika sana kuona watoto wa skuli fulani Zanzibar walivyokamatwa na shisha, bangi n.k isipokuwa mmoja aliyekutwa na kitabu kitakatifu. Wanaume tujitahidi kurudi nyumbani mapema kuchunga watoto wa kiume wanakoelekea si kuzuri.
 
Back
Top Bottom