USHUHUDA: Hivi ndivyo mafuta yanavyoibiwa Bandarini Dar...

USHUHUDA: Hivi ndivyo mafuta yanavyoibiwa Bandarini Dar...

Status
Not open for further replies.
Rais na Waziri wake mkuu watapata kazi sana kusafisha hii nchi,Ningewashauri kitu kimoja kama kweli wanataka kusafisha nchi hii na siyo "kuonekana wanasafisha" wakati ukweli hakuna kitu wanachofanya.

Wapo watu katika nchi hii wanazo taarifa za mifumo ya wizi katika sehemu mbalimbali jinsi inavyofanya kazi, either wao walishiriki na sasa hawapo kwenye hiyo mirija au wanashuhudia jinsi wizi unavyoendelea ingawa wao hawausiki. Rais angetengeneza utaratibu wa watu wema wenye taarifa ya madudu yanayofanyika katika taifa hili kupeleka hizo taarifa in details wakiwa wanajulikana au hawajulikani, iwe ni choice ya mtoa taarifa.

Nina uhakika wapo watu wangejitokeza kutoa hizo taarifa nikiwapo mimi.

Mimi nina uzoefu wa jinsi mafuta yanavyoibiwa bandarini:

Kwanza niweke wazi, mafuta hayaibiwi bandarini kwa kukadiria au sijui kwa sababu ya flow meters. Hakuna kitu kama hicho. Tena zile flow meter zilikuwa na capacity ndogo na zinaharibika mara kwa mara hivyo zikiharibika inabidi ku-bypass. Meli ikiwa inashusha mafuta inaweza kushusha kwa presha ya bar 16, zile flow meter zilikuwa hazihimili presha kubwa.

Mafuta yakishashushwa, kiwango cha mafuta kilichopokelewa kina pigiwa hesabu na ma-surveyor na wanatengeneza taarifa yao. Mchezo unaanzia hapo TRA, Mafuta yanayotakiwa kulipiwa ushuru ni ya local (yanayotumika humu nchini), na ya transit hayalipiwi ushuru. Sasa figure zinazoingizwa kwenye system ya TRA kwa ajili ya kulipiwa ushuru ndiyo hapo serikali inapoibiwa.

Na anayefanya mchezo huu ni afisa wa TRA kitengo cha mafuta akishirikiana na kampuni husika. Kuna makampuni ambayo yamekubuhu kwa mchezo huo. Makampuni ya watu binafsi yakiongozwa na yanayomilikiwa na waarabu. OILCOM ndio kinara, Lake oil, World oil, CAMEL Oil, etc.

Ipo mifano mingi ila natoa mmoja.

Kuna siku ilikuwa meli na mzigo mkubwa tu kana tani laki moja na nusu, Huo mzigo ulikuwa wa OILCOM. Kwenye Cargo manifesto ya meli ulikuwa umekuwa declared kama JET A1, (mafuta ya ndege) ya transit ya kwenda Zambia. Haya yana tax exemption.

Surveyor wa mzigo alikuwa kijana mmoja anaitwa ANDERSON kutoka Intertek. Akaenda kwenye meli akapima mzigo akaambiwa na wenye mzigo kuwa aandike kuwa ni JET A1 kwenye documents zake, ingawa mzigo ulikuwa ni diesel (GO), akaahidiwa dili ikishakamilika atapewa chake. Basi Anderson machale yakamcheza akaamua kutengeneza ducument set 2, moja akadiclare ule mzigo kuwa ni JET na nyingine kuwa ni GO.

Sasa kosa ambalo walilifanya hawakumuhusisha loading master wa pale manifold. Alipoambiwa afungue line ya kwenda oilcom, Yule mzee akafungua line ya JET ya kwenda OIL com. Sasa pale KOJ manifold kuna chujio za mafuta (Strainers) kwa ajili ya kila aina ya mafuta, na zina ukubwa tofauti kwaajili ya kuchuja mafuta. Mafuta yalipoanza kusukumwa, ile strainer ya JET ikaanza kupiga kelele yaani ikawa inapitisha mafuta kwa tabu.

Loading master akaamua kuangalia kwa nini inapiga kelele, akakuta mafuta yanayopita ni diesel tena ile diesel ya high sulphur (5000ppm). Akaita kwenye radio call, " We Anderson, hiyo mnayosukuma ni JET au DIESEL?", Hakuna mtu aliyejibu kenye radio, ikabidi pump za meli zizimwe washuke kwenye meli kwenda kuongea na loading master.

Sasa ile channel ya radio inayotumiwa kwa mawasiliano inasikiwa na watu wengi wakiwemo TRA, Usalama wa Taifa, Maofisa wa Bandari, n.k, baada ya kama nusu saa, watu zaidi ya 9 wakawa wamefika pale KOJ, wakiwemo maafisa wa usalama wa Taifa.

Kuona hivyo Underson akatoka na gari akakimbia, akamwacha Depot supervisor wa OILCOM, yule kijana wa oilcom ikabidi amtaarifu mzee ISLAM mwenyewe mwenye OILCOM kuwa kimesanuka. Ilikuwa ni Jumamosi, mzee Islam akaagiza watu wote walioenda kushuhudia ile saga waende OILcom, inavyosemekana kila mtu alipewa mil 80 cash palepale kwenye mifuko ya rambo. Na mzigo baadae ukashushwa kwenye line ya diesel.

Sasa ukiangalia wizi unaofanyika kwenye mafuta siyo wizi wa mafuta ila ni ukwepaji kodi, mafuta yanakuwa declared kama transit hayalipiwi ushuru ila yanauzwa local kwa bei ile ile. Na biashara hii ya kukwepa ushuru ilikuwa inasimamiwa na mwenyewe kamishna wa kodi ya forodha Bwana Masamaki.

Mafuta yakishaingiza kama transit yanatengenezewa document zote kuanzia za loading, Checkpoint zote za TRA, clearance ya Tunduma hadi upande wa pili wa boarder, na offloading documents na documents za ZRA(Zambia Revenue Authority). Na Bond clearance.

Hizi taarifa zote Usalama wa taifa wanazijua fika, kama Magufuli akitaka kusafisha, anatakiwa apate watu wa usalama wenye mtazamo kama wake. Laa sivyo, na wao watakuwa wanawashtua waalifu kwa meseji kama prof. Muhongo.

OIL COM ndio kinara.
God bless you
 
Ehee MUNGU nijaalie nipate kazi Bandarini kumbe 80M Unaanzaje kuikataa kwa mfano lol
Kuna jam sana pale mwaka jana nlienda na mzee wng mmoja kuchukua tank la mafuta ilikuwa usiku ilibidi tulale kwenye gari kumbe kuna watu usiku ule ndo wanafanya kazi wanapotoka hapajulikani magari ya ajabu ajabu yanaingia na kutoka kwa fujo kumbe ni deal za watu
 
Interesting! Angalau safari hii naona wadau mmeweka kando ile kauli ya "kumwonea wivu mtu aliye"hustle" kwa mafanikio yake makubwa". Mifano ya "waswahili" waliofanikiwa kwa kukingakinga "huto tumilioni 80" ni mingi na wamekuwa na utetezi mkubwa sana kwenye jamii yetu kama "wahangaikaji", "wajishughulishaji", "wajanja", n.k. Mtu anafanya kazi serikalini au taasisi ya umma, watu hawataki kabisa aguswe kwa "mafanikio" yake yasiyowiana na hali halisi.

Kama tunafikia hasira kali za kutaka kuwatimua nchini au kuwanyonga akina Oilcom, Camel oil, n.k. Ni vyema pia tujitambue sisi wenyewe kama jamii ya "wazawa" tukoje na harakati zetu za "kuuza nchi" au kuwatajirisha "wageni" kwa mafanikio binafsi "uchwara".
 
Nimejikuta natokwa machozi baada ya kusoma taarifa hii....yaani kila nikiona gari la OIL COM au kituo cha mafuta cha OIL COM.... najikuta natetemeka kwa hasira....
Hivi kwanini tusiwe tunawachinja hawa majizi jamaani....haaaaaaaaa......
Mkuu, bila ya kupitishwa sheria ya kupigwa Risasi Tanzania sijui Kama tutafanikiwa, sijui.
Yaani unasoma jambo mpaka unajisikia kutaka kulia, imekuwa Kama nchi isiyo na mwenyewe.
 
Mkuu, bila ya kupitishwa sheria ya kupigwa Risasi Tanzania sijui Kama tutafanikiwa, sijui.
Yaani unasoma jambo mpaka unajisikia kutaka kulia, imekuwa Kama nchi isiyo na mwenyewe.
Haswaa....hawa watu hawastahili kuishi kwa namna yoyote ile......
 
Nikisoma habari kama hizi naumia sana,imagine mtu mmoja anapewa mil. 80 za kumfunga mdomo!!!!
Najuta kuzaliwa Tanzania,Nchi ya wachache!
Wengine ni vile tumejikuta tumeshazaliwa Tanzania,hakuna namna nyingine!
Pole, makamanda tulitoka kidogo. Jumatano tutakuwa huko tena kwa siku chache .
 
Moja ya taarifa nzuri kabisa ambayo nimewahi kukutana nayo humu jamii forum. Bila shaka haitatua kwenye masikio ya viziwi bali wanaosikia na bila shaka itafanyiwa kazi. Jamani na wengine jitokezeni kutoa taarifa zitakazomsaidia rais wetu katika kuisafisha nchi. Tumempata rais mwenye uchungu na dhamira ya KWELI ya kuwasaidia wananchi. Tusimwangushe.
 
FUHRER ...huu ndio uzalendo, nina uhakika JPM na KMK wanania ya dhati na wangependa kupata taarifa hizi! Inabidi waandae mifumo ya kupata taarifa nyeti kama hizi. Hata hivyo ni imani yangu kuwa wao au wasaidizi wao wanapitia mitandao mbali mbali kama hii!
 
hii nchi aisee ukiifuatilia unaweza ukadata
Ndiyo sababu tuliambiwa maisha mazuri: Baba ana gari, mama ana gari Na watoto. Hata folen Dar zimetokana Na uwezo wa wana familia kumiliki magari. Napendekeza hata account za Watumishi wa umma na taasisi zake zidukuliwe! kujionea utajiri wao Wa haraka
 
Honestly habari kama hizi zinazidisha tu stress.. Hii nchi ngumu sana..
 
This world is not fair peopls.......dont catch feeling,that is just the way it is
 
Hii nondo imeshiba...nashauri Jamii Forum ifungue chumba kingine dedicated kwa ajili ya wapuliza filimbi (whistlebowers)..kila mtu alete taarifa in details kama huyu muheshimiwa....


tangu nianze kukujua, leo ndio umeandika jambo la busara! kudoz to you, tuweke mbali itikadi zetu za kivyama, UTAIFA KWANZA!.
 
huyo islam unaweza kuta ndio tajiri namba 1 afrika, noti analalia tu, mara ya kwanza toka mwaka 2007 ndo juzi tunalipiswa umeme ofisini kwetu, Magufuli tuzidi kumuombea
 
Hii taarifa je itafanyiwa kazi??? Baadhi ya mawaziri ndiyo watakao mwangusha Dr Magufuli
 
Tanzania Tanzania
Nakupenda kwa moyo wote
Nchi yangu Tanzania
Jina lako ni tamu sana
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom