USHUHUDA: Hivi ndivyo mafuta yanavyoibiwa Bandarini Dar...

Status
Not open for further replies.
Nahapa utashangaa
Rais anapokuwa mkali watu vilaza wanaanza kusema eti dikteta
Jamani mengine yanakera
We jamaa acha kuonyesha uwezo mdogo wa kufikiri katika mada muhimu, unaishushia hadhi mada hii. Hili sio suala la ukali bali ni kufuata sheria na sheria ndio kali katika mambo kama haya. Mtu anaitwa dikteta pale anapafanya jambo nje ya sheria na hasikilizi mawazo ya wengine. Au hujui hata maana ya neno Dikteta?
Hebu usitutoe katika mada na siasa zako hapa. Hili la Bandari nadhani sasa alishughulikie mwenyewe Magufuli maana inaonyesha hata watu ambao PM hawezi kuwashughulikia (kama mawaziri na wateule wengine) wanahusika hivyo aje mwenyewe mwenye uwezo wa kuwatimua.
 
Mimi naona ifadhi za mafuta zote ziwe chini ya serikali matenki yote ili kudhibiti wizi huu hakuna jinsi nyingine...pia kuwepo na mfumo mpya wa ulinzi kiundwe kukose cha ulinzi na usalama wandani
 
Ni makosa kama watu wa usalama wa taifa walioko bandarini bado ni wale wale wa awamu iliyopita.

Rais au Waziri mkuu aweke siku ya kukutana ikulu au popote na wanyetishaji habari muhimu kama hizi. Hata mimi nitampa yangu moja ya uhakika.
 
sure mkuu Fanya hivyo aisee..kuna watu wanaipenda hii nchi mtoa post ni no.1 mzarendo nimefarijika sana...
 
Msilete siasa hii issue sensitive i hope itafanyiwa kazi..

Mh majaliwa jipu hili
 
Kwa hiyo unashauri watu wanaojua madhambi mbalimbali wasiseme watulie tuu kwa vile JPM na Majaliwa wanajua kila kitu sio? Sasa kama wanajua kila kitu kwa nini suala la matumizi ya mita za mafuta na bomba mchepuko wamelikalia kimya Siku 100 toka waingie madarakani? Ni hasara kiasi gani imetokea kwa siku hizo zote?
Acheni kuwakatisha tamaa watu wenye nia njema kwa kufanya kila kitu ni siasa za mbwembwe hapa. Ili kujenga nchi yetu sote watu wa aina ya mleta mada sio wakukatisha tamaa bali wa kuenziwa kama tunavyo enzi watu wanaokamata silaha.


Wewe tuliza boli, miezi 3 siyo mingi kwa Raisi mgeni, kwanza kwa kawaida unahitaji hiyo miezi 3 kuitumia tu kuisoma na kuilewa nchi vizuri hivyo kwangu mimi wamejitahidi sana kwa yote waliyoyafanya mpaka leo hii!
Nchi nyingi hapa Duniani wanaombea hata siku moja wawe na Uongozi kama huu wetu wa kufanya yote haya ndani ya miez 3 tu, mabilioni ya fedha yameokolewa ndani ya miezi 3 tu, siyo kazi rahisi, watoto ambao walikuwa hawaendi Shule leo wanakwenda, TZ nzima tunasikia malalamiko madarasa yaliyokuwa yanachukuwa watoto 50 sasa wamekuja mia mbili inafikiri ni kwanini? Na hii yote ni ndani ya miezi mitatu tu!

Wahujumu uchumi wengi tu wana kesi Mahakamani, kuanzia TRA, TPA, mpaka Reli na TAKUKURU mpka NIDA kote huko ndani ya miezi mitatu tu!

Ndioy maana nikasema Raisi, WM na Serikali kwa ujumla wanafahamu yote hayo na walichokuwa wanakifanya ni kujielimisha kwanza zaidi kuhusu mfumo mzima ulivyo na sasa kazi imeanza, TIPER inarudi Serikalini kwa 100% na siyo 50% tena, unafikiri WM alikwenda pale huku akiwa hafahamu kwamba TIPER na wengineo walikuwa wamejiunganishia mabomba kiholela na kuiba mafuta?
 
Taarifa kama hizi ni muhimu zikafanyiwa kazi na wahusika
For the first time nakaa na wewe meza moja kula bia, jamaa ameelezea vizuri sana na natamabi gazeti la jamhuri waiandike hii kama ilivyo ila wasisahau kutupa credit huku, hivi yule mmiliki wake tulie nae humu aitwa nani vile
 
Ni makosa kama watu wa usalama wa taifa walioko bandarini bado ni wale wale wa awamu iliyopita.

Rais au Waziri mkuu aweke siku ya kukutana ikulu au popote na wanyetishaji habari muhimu kama hizi. Hata mimi nitampa yangu moja ya uhakika.


Mkuu ungeileta hapa ingekuwa poa zaidi. Nadhani ingeweza kumfikia mlengwa indirectly
 
Niliwahi kushauri iundwe special task force na watu wenye uzoefu na ubobezi wapewe kazi kuinyoosha bandari. Tunapoteza mabilioni ya pesa na tunaishia kutajirisha maarabu kwa tuliowapa dhamana kudanganyishiwa viela kiasi.
Hii nchi tunanyonywa na hawa wageni,wahindi,waarabu na wazungu utadhani nzi za ukoloni,tofauti kwasasa hatuchapwi fimbo tunatukanwa tuu na kutumikia kwa mshahara duni.
Mambo ya task force ndo yametufikisha hapa...

sasa hivi ni one man army na ziara za kushtukiza tu...
 
Mkuu itakuwa vizuri zaidi uongeze mifano miwili mitatu ili haya majipu yatumbuliwe
Mbona huu mfano unajitosheleza mkuu? Ametaja na maofisa waliyehusika, kampuni za mafuta zinazohusika, pamoja na kinara wao Masamaki aliyekuwa Kamisha wa forodha!
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom