USHUHUDA: Hivi ndivyo mafuta yanavyoibiwa Bandarini Dar...

Status
Not open for further replies.
Nadhani wananchi tuanze kususia bidhaa za makampuni haya yaliyotuibia muda mrefu ili tuonyeshe jinsi tulivyochukia.
Mkuu hili nalo neno,ingekua haya mambo yanatokea bara uropa na amerikani haya makampuni yangekosa wateja kabisa kwa kususiwa na wateja.
 
Tukipata watu kama wewe angalau hata hamsini wa kutoa taarifa za kina kutoka sehemu mbalimbali kuliko na majipu hakika tutakuwa tumesaidia sana watendaji pa kuanzia, kweli Tanzania ni tajiri kinachotakiwa tu ni uzalendo na uwajibikaji
 
@mega pixel hauna uzoefu na mijadala ya kwenye forums au siyo?
cause you sound kind of too emotional!

au we ni director wa huu uzi?
 
makada wa ccm ndio wanaongoza kwa ukwepaji kodi wakubwa ndani ya nchi hii wakijua kuwa wanasecurity hakuna wa kuwafanya kitu. Na uwizi wao wanafanya mchana kweupe. Kwa mfano uharamia wa meno ya tembo muhusika mkubwa ni kinaner huyu ni jipu la meno ya tembo kwa muda mrefu Sana hata meli yake ilishawai kudakwa na shehena ya meno ya tembo cha ajabu serekali aikufanya chochote.
 
Hii nchi ilishaoza kitambo aise! Yan wizi kila sehemu nahc kazi ya ziada inahtajika kama wazir umepewa dhamana kisha unatuma sms kushtua waizi? Noma sana
 
Duh hapo kazi ipo. Mkuu unaonekana utakua huko au unamtu wa kalibu sana
 
Rais na Waziri wake mkuu watapata kazi sana kusafisha hii nchi,Ningewashauri kitu kimoja kama kweli wanataka kusafisha nchi hii na siyo "kuonekana wanasafisha" wakati ukweli hakuna kitu wanachofanya.

Wapo watu katika nchi hii wanazo taarifa za mifumo ya wizi katika sehemu mbalimbali jinsi inavyofanya kazi, either wao walishiriki na sasa hawapo kwenye hiyo mirija au wanashuhudia jinsi wizi unavyoendelea ingawa wao hawausiki. Rais angetengeneza utaratibu wa watu wema wenye taarifa ya madudu yanayofanyika katika taifa hili kupeleka hizo taarifa in details wakiwa wanajulikana au hawajulikani, iwe ni choice ya mtoa taarifa.

Nina uhakika wapo watu wangejitokeza kutoa hizo taarifa nikiwapo mimi.

Mimi nina uzoefu wa jinsi mafuta yanavyoibiwa bandarini:

Kwanza niweke wazi, mafuta hayaibiwi bandarini kwa kukadiria au sijui kwa sababu ya flow meters. Hakuna kitu kama hicho. Tena zile flow meter zilikuwa na capacity ndogo na zinaharibika mara kwa mara hivyo zikiharibika inabidi ku-bypass. Meli ikiwa inashusha mafuta inaweza kushusha kwa presha ya bar 16, zile flow meter zilikuwa hazihimili presha kubwa.

Mafuta yakishashushwa, kiwango cha mafuta kilichopokelewa kina pigiwa hesabu na ma-surveyor na wanatengeneza taarifa yao. Mchezo unaanzia hapo TRA, Mafuta yanayotakiwa kulipiwa ushuru ni ya local (yanayotumika humu nchini), na ya transit hayalipiwi ushuru. Sasa figure zinazoingizwa kwenye system ya TRA kwa ajili ya kulipiwa ushuru ndiyo hapo serikali inapoibiwa.

Na anayefanya mchezo huu ni afisa wa TRA kitengo cha mafuta akishirikiana na kampuni husika. Kuna makampuni ambayo yamekubuhu kwa mchezo huo. Makampuni ya watu binafsi yakiongozwa na yanayomilikiwa na waarabu. OILCOM ndio kinara, Lake oil, World oil, CAMEL Oil, etc.

Ipo mifano mingi ila natoa mmoja.

Kuna siku ilikuwa meli na mzigo mkubwa tu kana tani laki moja na nusu, Huo mzigo ulikuwa wa OILCOM. Kwenye Cargo manifesto ya meli ulikuwa umekuwa declared kama JET A1, (mafuta ya ndege) ya transit ya kwenda Zambia. Haya yana tax exemption.

Surveyor wa mzigo alikuwa kijana mmoja anaitwa ANDERSON kutoka Intertek. Akaenda kwenye meli akapima mzigo akaambiwa na wenye mzigo kuwa aandike kuwa ni JET A1 kwenye documents zake, ingawa mzigo ulikuwa ni diesel (GO), akaahidiwa dili ikishakamilika atapewa chake. Basi Anderson machale yakamcheza akaamua kutengeneza ducument set 2, moja akadiclare ule mzigo kuwa ni JET na nyingine kuwa ni GO.

Sasa kosa ambalo walilifanya hawakumuhusisha loading master wa pale manifold. Alipoambiwa afungue line ya kwenda oilcom, Yule mzee akafungua line ya JET ya kwenda OIL com. Sasa pale KOJ manifold kuna chujio za mafuta (Strainers) kwa ajili ya kila aina ya mafuta, na zina ukubwa tofauti kwaajili ya kuchuja mafuta. Mafuta yalipoanza kusukumwa, ile strainer ya JET ikaanza kupiga kelele yaani ikawa inapitisha mafuta kwa tabu.

Loading master akaamua kuangalia kwa nini inapiga kelele, akakuta mafuta yanayopita ni diesel tena ile diesel ya high sulphur (5000ppm). Akaita kwenye radio call, " We Anderson, hiyo mnayosukuma ni JET au DIESEL?", Hakuna mtu aliyejibu kenye radio, ikabidi pump za meli zizimwe washuke kwenye meli kwenda kuongea na loading master.

Sasa ile channel ya radio inayotumiwa kwa mawasiliano inasikiwa na watu wengi wakiwemo TRA, Usalama wa Taifa, Maofisa wa Bandari, n.k, baada ya kama nusu saa, watu zaidi ya 9 wakawa wamefika pale KOJ, wakiwemo maafisa wa usalama wa Taifa.

Kuona hivyo Underson akatoka na gari akakimbia, akamwacha Depot supervisor wa OILCOM, yule kijana wa oilcom ikabidi amtaarifu mzee ISLAM mwenyewe mwenye OILCOM kuwa kimesanuka. Ilikuwa ni Jumamosi, mzee Islam akaagiza watu wote walioenda kushuhudia ile saga waende OILcom, inavyosemekana kila mtu alipewa mil 80 cash palepale kwenye mifuko ya rambo. Na mzigo baadae ukashushwa kwenye line ya diesel.

Sasa ukiangalia wizi unaofanyika kwenye mafuta siyo wizi wa mafuta ila ni ukwepaji kodi, mafuta yanakuwa declared kama transit hayalipiwi ushuru ila yanauzwa local kwa bei ile ile. Na biashara hii ya kukwepa ushuru ilikuwa inasimamiwa na mwenyewe kamishna wa kodi ya forodha Bwana Masamaki.

Mafuta yakishaingiza kama transit yanatengenezewa document zote kuanzia za loading, Checkpoint zote za TRA, clearance ya Tunduma hadi upande wa pili wa boarder, na offloading documents na documents za ZRA(Zambia Revenue Authority). Na Bond clearance.

Hizi taarifa zote Usalama wa taifa wanazijua fika, kama Magufuli akitaka kusafisha, anatakiwa apate watu wa usalama wenye mtazamo kama wake. Laa sivyo, na wao watakuwa wanawashtua waalifu kwa meseji kama prof. Muhongo.

OIL COM ndio kinara.
nimekusoma sana mkuu...kwa pamoja tutaijenga tz
 
Niliwahi kushauri iundwe special task force na watu wenye uzoefu na ubobezi wapewe kazi kuinyoosha bandari. Tunapoteza mabilioni ya pesa na tunaishia kutajirisha maarabu kwa tuliowapa dhamana kudanganyishiwa viela kiasi.
Hii nchi tunanyonywa na hawa wageni,wahindi,waarabu na wazungu utadhani nzi za ukoloni,tofauti kwasasa hatuchapwi fimbo tunatukanwa tuu na kutumikia kwa mshahara duni.
 
Wewe wala usijali sidhani kama Raisi Magufuli na Waziri Mkuu Majaliwa hawayajui hayo uliyoyaeleza wanayajua sana kwanza wanayajua kabla hata WM hajaenda hapo kwenye hiyo mitambo ya mafuta na ndiyo maana unaona hawakuweza kumdanganya ingawaje yeye WM siyo mtaalamu wa mambo ya mafuta, alikuwa na data zote na hata ukifwatilia maagizo aliyoyatoa siyo ya mtu ambaye hakuwa amejitayarisha na asiyejua alichokuwa anakifanya!

Hata ukiangalia huyo Masamaki uliyemtaja alishachomolewa zamani na ana kesi hivyo ninaweza kukutoa hofu wanajua kila kitu na ni swala la muda tu kwani lazima ujue kwamba wahalifu nao pia ni werevu hivyo ni lazima kwenda nao kwa umakini na mwisho wa siku sisi tunachotaka na fedha zetu ninakwambia kwa Magufuli kila jiwe litafunuliwa kama alivyosema Mzee Slaa, hao akina Oil Com, Lake Oil wote wako kwenye radar utasikia tu mdu siyo mrefu!

Hivyo wewe chill na relax Raisi na Serikali yake wanafahamu yote hayo na zaidi kuna sababu kwa nini Maswi aliletwa halafu akaondolewa baada ya kumaliza kazi yake hivyo sasa kazi ndiyo imeanza na haponi mhalifu yoyote yule amini usiamini!
Kwa hiyo unashauri watu wanaojua madhambi mbalimbali wasiseme watulie tuu kwa vile JPM na Majaliwa wanajua kila kitu sio? Sasa kama wanajua kila kitu kwa nini suala la matumizi ya mita za mafuta na bomba mchepuko wamelikalia kimya Siku 100 toka waingie madarakani? Ni hasara kiasi gani imetokea kwa siku hizo zote?
Acheni kuwakatisha tamaa watu wenye nia njema kwa kufanya kila kitu ni siasa za mbwembwe hapa. Ili kujenga nchi yetu sote watu wa aina ya mleta mada sio wakukatisha tamaa bali wa kuenziwa kama tunavyo enzi watu wanaokamata silaha.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom