Wewe wala usijali sidhani kama Raisi Magufuli na Waziri Mkuu Majaliwa hawayajui hayo uliyoyaeleza wanayajua sana kwanza wanayajua kabla hata WM hajaenda hapo kwenye hiyo mitambo ya mafuta na ndiyo maana unaona hawakuweza kumdanganya ingawaje yeye WM siyo mtaalamu wa mambo ya mafuta, alikuwa na data zote na hata ukifwatilia maagizo aliyoyatoa siyo ya mtu ambaye hakuwa amejitayarisha na asiyejua alichokuwa anakifanya!
Hata ukiangalia huyo Masamaki uliyemtaja alishachomolewa zamani na ana kesi hivyo ninaweza kukutoa hofu wanajua kila kitu na ni swala la muda tu kwani lazima ujue kwamba wahalifu nao pia ni werevu hivyo ni lazima kwenda nao kwa umakini na mwisho wa siku sisi tunachotaka na fedha zetu ninakwambia kwa Magufuli kila jiwe litafunuliwa kama alivyosema Mzee Slaa, hao akina Oil Com, Lake Oil wote wako kwenye radar utasikia tu mdu siyo mrefu!
Hivyo wewe chill na relax Raisi na Serikali yake wanafahamu yote hayo na zaidi kuna sababu kwa nini Maswi aliletwa halafu akaondolewa baada ya kumaliza kazi yake hivyo sasa kazi ndiyo imeanza na haponi mhalifu yoyote yule amini usiamini!