Ushirikiano kwenye sekta ya kilimo kati ya China na Tanzania kusaidia kupunguza umaskini

ldleo

JF-Expert Member
Jan 9, 2010
1,010
1,036
1688454516504.png


Kwenye maonyesho ya tatu ya uchumi na biashara kati ya China na Afrika yaliyofanyika mjini Changsha, Mkoani Hunan, sekta ya kilimo ilikuwa ni moja ya maeneo yaliyopewa uzito mkubwa kwenye biashara na makongamano yaliyofanyika sambamba na maonyesho hayo. Licha ya kuwa sekta ya kilimo ni eneo moja tu la ushirikiano kati ya China na Afrika, sekta hii ina umuhimu wa kipekee kwa kuwa inagusa watu wengi sana barani Afrika.



Sekta ya kilimo bado inaendelea kuwa uti wa mgongo kwenye uchumi wa nchi nyingi za Afrika. Pamoja na ukweli kwamba katika siku za karibuni sekta nyingine zimekuwa na maendeleo makubwa, sekta ya kilimo inaendelea kuwa ni tegemeo kwa watu wengi na imeajiri watu wengi. Juhudi zote za kupambana na umaskini katika nchi za Afrika, haziwezi kukamilika bila uwekezaji madhubuti kwenye sekta ya kilimo.



Nchini Tanzania kilimo cha soya kimekuwa ni moja ya maeneo ambayo China na Tanzania zimetoa kipaumbele katika juhudi za kuendeleza kilimo na kuwaondoa watu katika umaskini. Tangu China ilipotangaza kufungua soko lake la soya kwa nchi za Afrika, Tanzania imekuwa ni nchi inayoruhusiwa kuuza maharage ya soya bila ukomo. Hii ina maana kuwa bila kujali Tanzania inazalisha maharage hayo kwa kiasi gani, soko limehakikishwa kwa muda mrefu.



Ili kutumia vizuri fursa hiyo, makampuni mbalimbali ikiwa ni pamoja na yale yanayojihusisha moja kwa moja na kilimo, na yale yanayofanya biashara ya mazao ya kilimo yameanzishwa. Moja ya makampuni hayo ni kampuni ya Delmoche iliyoko mjini Dar es salaam, ambayo imeweka utaratibu wa kutoa mbegu, kutoa mashamba na hata kutoa mafunzo kwa wanawake na wanaume vijana, ili waweze kulima zao hilo kwa ufanisi. Mkuu wa kampuni hiyo Bibi Lulu Eric Mora, amesema kampuni yake ina programu kamili inayoendeshwa katika eneo la majaribio mkoani Mbeya ambayo kila atakayeshiriki atakuwa na uwezo wa kujitegemea baada ya miaka miwili.



Kampuni hiyo inaandikisha watu na kuwapa mbegu za soya, kuwapatia mafunzo na ujuzi wa kuhakikisha kuwa wanalima kwa njia za kitaalam, na hata kuwahakikishia soko, kuwa baada ya kuvuna watanunua maharage yao yote. Kampuni hiyo imeamua kuwa na hatua hizo mseto kwa kuwa inatambua changamoto walizonazo wakulima wa Tanzania kwenye upande wa teknolojia katika kuendeleza kilimo hasa kwenye upande wa mbegu, ardhi inayofaa kwa kilimo na hali ya hewa, na pia inatambua kuwa kutokana na uwezo mdogo wa kifedha na kutoweza kuyafikia masoko. Kwa hiyo kwa kufanya hivi sio kama tu wataweza kuwasaidia wakulima kuwa na ujuzi wa kilimo cha zao hili na hata kuwahakikishia soko, lakini pia kampuni hiyo inachangia moja kwa moja kwenye juhudi za serikali ya Tanzania kupambana na umaskini na kuwainua watu wa vijijini.



Kaulimbiu ya maonyesho hayo ilikuwa ni “maendeleo ya pamoja, kwa mustakabali wa pamoja”. Kauli mbiu hii inaonyesha nia thabiti ya China kutumia maendeleo yake kuwa fursa kwa nchi rafiki ambazo ziko nyuma kimaendeleo. Lakini licha ya fursa kubwa kama hii, undani wa sekta ya kilimo katika nchi nyingi za Afrika ikiwa ni pamoja na Tanzania unaonesha kuwa bado una udhaifu mwingi. Kilimo bado kinaendelea kufanyika kwa njia za jadi, matumizi ya mashine bado ni tatizo kubwa kwa wakulima wengi.



Kampuni ya Delmoche pia inajitahidi kuangalia wazalishaji wa zana za kilimo za bei nafuu, ili kuangalia uwezekano kwa kampuni hizo kufikisha zana hizo kwa wakulima nchini Tanzania na kuongeza uzalishaji wao.
 
Back
Top Bottom