Ushirikiano wa kiuchumi kati ya China na Afrika kwa mwaka 2024 unatarajiwa kuimarika

ldleo

JF-Expert Member
Jan 9, 2010
1,010
1,035
VCG111465819325.jpg


Katika kipindi cha miongo miwili iliyopita, China imejenga uhusiano wa kina wa kiuchumi na nchi za Afrika, na kuifanya kuwa mshirika mkubwa zaidi wa biashara wa nchi hizo, na chanzo muhimu cha uwekezaji wa moja kwa moja. Katika kipindi cha miaka miwili hadi minne iliyopita, kutokana na changamoto mbalimbali duniani eneo la ushirikiano wa kiuchumi na biashara kati ya pande hizo mbili limekumbwa na changamoto kiasi, lakini kutokana na mipango na mikakati ya ushirikiano kati ya China na Afrika, mwelekeo kwa mwaka 2024 ni wa matumaini.

Katika nusu ya pili ya mwaka 2023, shughuli nyingi za ushirikiano wa kiuchumi na kibiashara kati ya China na nchi za Afrika zimeonekana kurudi katika hali ya kawaida. Itifaki ya kupambana na COVID-19 ambayo ilileta changamoto kwenye usafiri na biashara, imeondolewa kwa ukamilifu na sasa si changamoto tena, na shughuli nyingi za ushirikiano wa kiuchumi na kibiashara zimerejea katika hali ya kawaida.

Hali hii inafanya miradi yote mikubwa ya ushirikiano, na mikakati yote ya ushirikiano kati ya China na Afrika ikiwa ni pamoja na uwekezaji wa moja kwa moja, irudi kwenye njia yake ya awali japokuwa kuna haja ya juhudi zaidi kufanyika ili kurudisha hali iliyokuwa kabla ya janga la COVID-19 na hata kuwa zaidi ya hapo. Wataalamu wa uchumi wamekuwa wakitaka kuwa kama uchumi wa China utapungua kwa asilimia moja, uchumi wa Afrika utapungua moja kwa moja kwa asilimia 0.25, na kama uchumi wa China utaongezeka uchumi wa Afrika pia utaongezeka, na hii ndio hatma ya pamoja ambayo China imekuwa inaitaka mara kwa mara kwenye uhusiano kati yake na nchi za Afrika.

Takwimu zinaonesha kuwa thamani ya uwekezaji wa moja kwa moja (FDI) wa China barani Afrika kwa mwaka 2022, ulikuwa ni karibu dola za kimarekani bilioni 1.8. Kiasi hicho ni chini ya nusu ilikinganishwa na mwaka uliotangulia, na sababu kubwa ni misukosuko mbalimbali iliyoonekana duniani kutokana na janga la COVID-19 na maswala mengine yanayoendelea duniani. Hata hivyo fedha hizo zilizoenda Afrika zimekuwa na mchango mkubwa katika sekta muhimu za uchumi kwa nchi za Afrika.

Wachumi na watunga sera wa nchi nyingi za Afrika, wamekuwa na maoni yanayofanana kuhusu uwekezaji wa moja kwa moja wa China barani Afrika, yaani umekuwa na mchango mkubwa katika kuhimiza maendeleo ya kiuchumi na kijamii barani Afrika. Mbali na kutoa nafasi za ajira kwa nchi za Afrika, uwekezaji huo pia unaongeza vyanzo vya mapato ya serikali, na hata kuchochea sekta nyingine za uchumi. Pamoja na kuwa China ni nchi iliyoendelea kiteknolojia, na inaweza kufanya uwekezaji unaotumia teknolojia zaidi kuliko nguvu kazi ya binadamu, kwa makusudi kabisa uwekezaji unaofanyika ni ule unaoajiri idadi kubwa ya wenyeji.

Tofauti kati ya uwekezaji wa China barani Afrika na ule wa nchi za magharibi, ni kwamba uwekezaji wa China unalingana zaidi ya mahitaji ya nchi za Afrika kwenye juhudi za kufikia maendeleo endelevu, japokuwa uwekezaji wake unaweza kutokuwa na thamani kubwa ikilinganishwa na ule wa Marekani na Umoja wa Ulaya, lakini matokeo yake katika kuhimiza maendeleo ya kiuchumi na kijamii ni makubwa zaidi (multiplier effect). Uwekezaji wa nchi za magharibi unajikita zaidi kwenye kutafuta faida kubwa na kutojali sana uwekezaji huo unanufaisha vipi watu wa nchi inayopokea uwekezaji.

Mwaka 2024 utakuwa pia ni mwaka muhimu wa mikutano ya ushirikiano kati ya China na Afrika, kama vile mkutano wa baraza la ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC). Bila shaka kupitia majukwaa hayo kutakuwa na fursa zaidi kwa nchi za Afrika.
 
Back
Top Bottom