Ni redio ya wahuni tuwapuuze cloud
Hao ni wachambuzi wa magazeti,sio wachambuzi wa habari
litakaloandikwa la kipropaganda wanatiririka nalo,hawajitegemei kiakili,kiuelewa
Jamani ina maana hamjui kuwa hii ni redio ya udaku kama yalivyo magazeti ya udaku? Kutwa kuongelea maisha ya mtu mmoja mmoja
Mkuu umenichekesha sana yaani umejiunga mwaka 2009 lakini leo ndiyo kwanza una post 3 hivyo kwa wastani ni kila mwaka ni 0.75...hahahah jitahidi basi uwe unapost hata mara moja kwa mwaka...
Leo asubuhi kwenye kipindi cha Power breakfast watangazaji wa Clouds FM wameongea mengi ya kumbeza Lema na kesi yake. Sijui sasa hivi wanajisikiaje baada ya hukumu kusoma.
Ombi langu kwa vyombo vya habari:
Msioneshe waziwazi kwamba mnaegemea upande fulani wa chama cha kisiasa kwani vyombo vyenu hivyo ni vya kibiashara. Jamii ikigundua kuwa mna mlengo flani itawasusa.
Mwana JF aliyesikiliza kipindi hicho anaweza akaongeza yale yalokuwa yakiongelewa..
Leo asubuhi kwenye kipindi cha Power breakfast watangazaji wa Clouds FM wameongea mengi ya kumbeza Lema na kesi yake. Sijui sasa hivi wanajisikiaje baada ya hukumu kusoma.
Ombi langu kwa vyombo vya habari:
Msioneshe waziwazi kwamba mnaegemea upande fulani wa chama cha kisiasa kwani vyombo vyenu hivyo ni vya kibiashara. Jamii ikigundua kuwa mna mlengo flani itawasusa.
Mwana JF aliyesikiliza kipindi hicho anaweza akaongeza yale yalokuwa yakiongelewa..
Binafsi nimesikiliza kipindi cha PB asubuhi ya leo nikielekea kazini kwa masikitiko makubwa. Kuanzia leo sisikilizi kipindi hiki tena kwani sikubaliani na itikadi ya redio hii kwa sasa. Hii ni redio ya watu inatakiwa kuwa neutral kabisa! Hakuna ubishi, hii redio sasa imechagua waziwazi kuwa upande wa watawala na kushabikia kila linaloangukiwa upande huo.
Ki ukweli wale jamaa wanatakiwa watangaze mambo ya bongo flavour tu! lakini hawana kitu cha maana kichwani cha kuwa wachambuzi zaidi ya umbea na majungu! wamekaa kihuni huni sana!
Kuna nchi nyingine bila kuwa na degree ya chuo kikuu hupewi kadi ya uandishi wa Habari na kuna chombo maalum cha kusimamia taaluma hiyo kama vile baraza la habari au Maelezo.Uganda wao wanahitaji angalau Diploma, naamini kwenye sheria ya vyombo vya habari ambayo MOAT,MCT na wadau wengine wanadai kutoka serikalini lazima uweke standards za weledi katika tasnia ya habari ili kuepuka MAKANJANJA KAMA HAWA WA CLOUDS.
Usiwaite waandishi maana tutakuomba ututajie vyuo walivyosoma (kuna madj na wasema chochote tu pale though wachache sana ndio wanataaluma hizo), kuna kipindi watu waliokuwa wana deal na mambo ya procurement walikuwa na chombo chao kilichokuwa kinafuatilia kuhusu makampuni na taasisi mbalimbali kuajiri watu wenye utaalamu na hiyo kazi baada ya kuonekana kuna watu wengi wanafanya kazi bila kuwa na utaalamu wa procurement, hivi kwenye issue kama radio na tv hakuna mamlaka za kufuatilia maana ni rahisi kwa chombo kupotosha watu kama kitakuwa hakina watu makini na ndio maana vyombo vingi vina watu ambao wamebobea kwenye fani though vinajiri watu wasio na weledi sana but supervision inakuwa kali.
Mfano mzuri hii issue ya yule jamaa mwizi wa vifaa vya magari, kuna mtangazi akawa anasema huyu jamaa amevuka level ya mwizi tumwite Haramia au Jangili wakati hapo kila neno lina maana yake maana ukifanya uhalifu wa majini kwa either kupora au kuiba huo ni uharamia na kama nyara za serikali huo ni Ujangili. (hapo watakuwa wamepotosha wangapi sasa kama mtu anaropoka tu maana kama wangekuwa wanaandika yale wanayoongea na kupitiwa ingekuwa poa.
Mwenye e-mail ya Zimbwera wa East Africa radio aniwekee hapa ili nimrushie hii link aone jamii ilivyokereka na washindani wenzake.
Mwenye e-mail ya Zimbwera wa East Africa radio aniwekee hapa ili nimrushie hii link aone jamii ilivyokereka na washindani wenzake.