Ushindi wa Lema, aibu kwa Clouds FM

Ushindi wa Lema, aibu kwa Clouds FM

alfu hawa watangazaji wa coudz wengi wao kama vile wanacamerooniwa(refer: nchi zlipewa masharti gani ili kupewa misaada)
 
Clouds ni radio ya wahuni,wenye taaluma ya uhandishi pale ni kama hakuna tu,wengi ni wale Vijana wajanja wajanja wa mjini wanaozijua story za vijiweni,kuvuta bangi na starehe!zaidi ya hapo ni uharo mtupu,hakuna mwenye uwezo wa kujenga au kuchambua hoja!
 
redio za aina hii ni hatari kama zile zilizochangia mauaji Rwanda na Kenya. They should adhere to professionalism.
 
gerard hando alinibore sana kuni hata kama ukubaliani na mwandishi sio kuongea vile na kucheka kidharau mda mrefu kwa kurudia rudia kihivyo
 
Clouds tumeshawasema friendly mpaka tumechoka. Kuelekea 2015 lazima virus vyote tuvisafishe otherwise wataleta machafuko.
 
Mkuu hata mimi ni shahidi nimewasikia Hando na Mwenzake PJ wakibeza headline ya Tanzania Daima inayomhusu Lema. PJ akasema kabisa si bora (waliombatana na Lema kutoka Arusha) wangetumia hela walizogramia safari kula na familia zao. Swali langu kwa CLOUDS FM je wanalipa watu mishahara hata muwapangie matumizi?. Hii radio watangazaji wake inaokota bar? hawana weledi kabisa wa taalumu ya utangazaji, ni bora ukasikiliza Zembwela anavyochambua habari kuliko kusikiliza mipasho ya Clouds kuanzia PB mpaka Jahazi umbea mtupu.
 
clouds FM ni nini mbona sijahahi kusikia kitu kama hicho hapa dar! usikute ni hizi radio za mazoezi
 
lack of knowlege kwa wanahabari clouds FM, wanasubiri nafasi za kupewa,kama vile ukuu wa wilaya na ukuu wa mkoa ndo maana huwa wanasifia mambo ya kipuuzi ya CCM.ili Jk awaone.mbululaa hao.
 
Nimewasikia sana hawa jamaa bana! Yaani wameijadili hiyo habari toka Tanzania Daima yenye kichwa hiki;
h.sep7.gif
RUFAA YA LEMA: Hukumu ya kihistoria leo
 
Achaneni na vilaza hao!!!! Tudumishe chama mamluki hawatakiwi sasa tunataka mabadiliko
 
Nilikuwa nawapenda sana na nilipenda sana kusikiliza vipindi kumbe wanatumiwa na mafisadi,nilijua ni radio ya watu kumbe sio hivyo,sasa wameumbuka,sijui kama ni wanahabari waliosemea uanahabari, big up Lema ,big up CDM
 
Leo asubuhi kwenye kipindi cha Power breakfast watangazaji wa Clouds FM wameongea mengi ya kumbeza Lema na kesi yake. Sijui sasa hivi wanajisikiaje baada ya hukumu kusoma.

Ombi langu kwa vyombo vya habari:
Msioneshe waziwazi kwamba mnaegemea upande fulani wa chama cha kisiasa kwani vyombo vyenu hivyo ni vya kibiashara. Jamii ikigundua kuwa mna mlengo flani itawasusa. Mwana JF aliyesikiliza kipindi hicho anaweza akaongeza yale yalokuwa yakiongelewa..

Walihukumu mapema pasipo kujua vifungu vya sheria
 
Msipate taabu sana ya kuwaongelea watu ambao uwezo wao wa kufikiri ni mdogo, fanyeni mambo mengine ambayo ni ya msingi. Pale hakuna mtu mwenye shule ya maana..omba cv zao kama watakupa....ha ha ha ha...
 
Clouds FM ni redio ya kusikiliza mipasho na burudani kama umechoka. Si redio ya kusikiliza mambo makini na muhimu kwa jamii. Hapo inatakiwa mtu kuwa na akili ya kuchambua kujua pumba na mchele. Ni kama gazeti, hutegemei kununua Ijumaa kupata habari za uchambuzi, hutegemei kusikiliza Clouds FM kupata habari za uschambuzi au maadili ya jamii. Full mipasho na vichekesho. Thats their business model.
 
:A S cry:Baadhi ya watangazaji wa clouds siku nyingi wanaonesha kujikiomba kwa ccm na baadhi ya viongozi kwa ajili ya matumbo yao! Ila wajue huu ni wakati wa ukombozi na watu wako serious na maisha yao, yasije yakawakuta ikiwemo kususia hiyo redio yao, kwa nza nisha anza maana wao wanaongea udaku mtupu!!!
 
Hapo kwenye red, kunakuhusu wewe na vilaza wenzako wa clouds, mleta mada hajakurupuka, ila wewe na wenzako clouds ndo mnakurupuka, hata mtu akisoma hii post yako ataelewa tu uwezo wako wa kufikiri ni mdogo kama wa kiroboto.

Duh! msamehe mkuu; inawezekana huyu ni mfanyakazi wa Clouds FM; aangalie wachangiaji wangapi wanaungana naye. Kama hataki kirekebika mwache tu!
 
Back
Top Bottom