Ushindi wa Lema, aibu kwa Clouds FM

Ushindi wa Lema, aibu kwa Clouds FM

Unajua weakness ya Chombo cha habari kama Clouds ni kwamba wanaokota Ma-DJ wenye umaarufu wa kijinga jinga na Washereheshaji wa Kitchen parties na kuwageuza waandishi. Hivyo ni u kanjanja kwenda mbele. Wengi shule hakuna pale wala hakuna mwenye mafunzo ya Ki taaluma kutoka kwenye chuo vinavyoeleweka. Na matokeo yake ni rahisi kutambua matundu ya udhaifu wao pale inapotekea mijadala unakuta hata uwezo wao wa kuchambua mambo unakuwa very limited na wamekuwa wakipwaya kwa kiasi kikubwa.

Mi huwa hata siwasilizagi kwa kweli vihiyo hawa wa Cloud. Wamejaa misifa ya kimjini mjini na ushakumpe.

Wanahitaji kubadilisha mtazamo na ku reshape chombo hiki kama wanataka watu makini wawachukulie serious kwa kweli.
 
Waandishi waliopo pale hawana weledi wa aina yoyote zaidi ya kubwabwaja tu maneno yasiyokuwa na mpangilio.

Usiwaite waandishi maana tutakuomba ututajie vyuo walivyosoma (kuna madj na wasema chochote tu pale though wachache sana ndio wanataaluma hizo)
, kuna kipindi watu waliokuwa wana deal na mambo ya procurement walikuwa na chombo chao kilichokuwa kinafuatilia kuhusu makampuni na taasisi mbalimbali kuajiri watu wenye utaalamu na hiyo kazi baada ya kuonekana kuna watu wengi wanafanya kazi bila kuwa na utaalamu wa procurement, hivi kwenye issue kama radio na tv hakuna mamlaka za kufuatilia maana ni rahisi kwa chombo kupotosha watu kama kitakuwa hakina watu makini na ndio maana vyombo vingi vina watu ambao wamebobea kwenye fani though vinajiri watu wasio na weledi sana but supervision inakuwa kali.

Mfano mzuri hii issue ya yule jamaa mwizi wa vifaa vya magari, kuna mtangazi akawa anasema huyu jamaa amevuka level ya mwizi tumwite Haramia au Jangili wakati hapo kila neno lina maana yake maana ukifanya uhalifu wa majini kwa either kupora au kuiba huo ni uharamia na kama nyara za serikali huo ni Ujangili. (hapo watakuwa wamepotosha wangapi sasa kama mtu anaropoka tu maana kama wangekuwa wanaandika yale wanayoongea na kupitiwa ingekuwa poa.
 
hapa nadhani mnawachafua clauds bure,tafadhali mfanye tena utafiti wa kina kujua mnachokisema kama ni sawa

Fuatilia vipindi vyao kama utasikia lolote la maana zaidi ya maongezi utafikiri wako kijiweni, bongo flavor za kitoto kwa sana bas; huwezi kusikia hata nyimbo zenye maadili,

Walianza vizuri lakini siku hizi wanapoteza kabisa mwelekeo.
 
Naomba kuhabarishwa! Lema kashinda??? MUNGU MKUBWA LOL!!
 
Nilisikia Gerald Hando alichosema ni kwamba kivipi kesi hiyo inaweza kuwa ni ya kihistoria? Kwamba je, huyo ndo mbunge wa kwanza kuvuliwa ubunge? Kwamba watu wanawezaje kufunga safari kutoka Arusha kuja Dar kusikiliza kesi tu? Hakuna neno hata moja lilotaja CCM wala Chadema.

Tatizo lenu mlio wengi hamjipi muda wa kuchambua na kutafakari kuhusu hoja husika.

Kwanza Clouds siyo chama cha siasa na wala haifungamani na upande wowote. Hiki hakiwezi kuwa chombo cha kusifia hata upuuzi eti kwasababu umefanywa na cha pendwa, never. Tuache kukurupuka.
 
Kiukeweli mimi niliwasikiliza hawaq jamaa yaani wameniboa sana, tatizo la Clouds wanapenda kualikua kuwa MC kwenye birthday ya JK na hivyo wanaona kuwa wakiibeba CCM ndo wanajihakikishia ulaji.

Ajenda yao ilikuwa kuipinga habari iliyoandikwa na gazeti la Tanzania Daima kuwa hukumu ya kesi ya lema ni ya kihistoria lakini wameshindwa kuelewa maaana pana ya habari hiyo.

Kwa mfano:
Mimi naweza kusema kuwa sijawahi kushuhudia hukumu ya rufani ktk kesi ya uchaguzi tena yenye kuvuta hisia za watu wengi kama hii ya Lema, kwa hiyo kwangu mimi hiyo ni historia.

Wakumbuke kuwa kama sio ya kihistoria kwa huyu inaweza ikawa ya kihistoria kwa yule.

R.I.P coudz udaku
 
attachment.php

Wenzetu wanasema amlipaye mpiga zeze ndiye uchagua wimbo, hawa hawana jinsi they are simply remote controlled, at one time their boss financed Jk's birthiday party.

Just ignore them they have no alternative because they are beneficiries of the System.
 

Attachments

  • LEMA.jpg
    LEMA.jpg
    37.4 KB · Views: 376
Mbona wakiisifia CHADEMA hamsemi?

Redio hawatakiwi kuwa wanaaa hebu Jiulize hivi kutokana na makala hii huwaoni kama hao watangazaji ni wazembe?;

Nimefuatilia mwenendo wa kesi hii lazima nimpongeze Lema.

Hongera Lema kwa Kurudi Bungeni Aliyekuwa Mbunge wa Arusha Godbless Lema amerudishiwa ubunge wake baada ya kushinda katika rufaa ya kesi yake ya kupinga matokeo iliyosomwa jijini Dar es Salaam leo. Hukumu imeangalia haswa swala la "Locus Stand" ya kama "waliofungua kesi walikuwa na haki kisheria ya kufanya hivyo".

Kadiri ya pingamizi ya mawakili wa Lema Ndg. Kimomogoro na Tundu Lissu, waliofungua shitaka dhidi ya Lema hawakuwa na "Locus Stand" ya kufanya hivyo. Kwa hiyo mengine yote yanakuwa "null and void".

Hukumu haikuchukua hata nusu saa aibu iliyoje hii?.
Hoja moja tu tena ya kwanza kati ya hoja 18 zilizowasilishwa na upande wa rufaa kupinga hukumu hiyo mbele ya majaji Salum Massati, Bernard Luanda na kiongozi wao Nathalia Kimaro imeonesha ukomavu wa mawakili Kimomogoro na Tundu Lissu.

Nachukua fursa hii kuwapongeza majaji hawa Salum Massati, Bernard Luanda na Nathalia Kimaro na mawakili Kimomogoro na Tundu Lissu kwa kuonesha ukomavu wao na kuthibitisha kuwa taaluma yao haina mashaka hata chembe. Mungu awajaalie wazidi kuwa na mafanikio makubwa na heri katika kazi zao, tunahitaji wazalendo kama hawa ili nchi iwe na ustawi na kudumisha haki.
Lema alivuliwa ubunge Aprili 5, 2012 katika hukumu iliyotolewa na Jaji Gabriel Rwakibalira, kutokana na kesi iliyofunguliwa na makada watatu wa CCM; Mussa Mkanga, Happy Kivuyo na Agnes Mollel, wakipinga ushindi wake katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010.

Serikali inatakiwa kumchunguza kwa makini Jaji Gabriel Rwakibalira. Kwa maoni yangu nadhani huyu ni kada wa CCM na kama sivyo basi taaluma yake ni batili na butu sharti achunguzwe pia alisomea wapi kwani hawa ndiyo akina KIHIYO wanaogushi vyeti na kukalia nyadhifa muhimu huku wajuzi walio makini wakikosa nafasi kwa kuwa hawana ndugu wa kuwapachika katika nafasi hizo. Hivi karibuni kulitokea tuhuma zilizoenea kuwa baadhi ya majaji na mahakimu hawajui Kiingereza hali inayosababisha kushindwa kutoa hukumu sahihi kwa misisngi ya haki bali wanahukumu kwa utashi na matakwa yao hii ni hatari kwa taifa letu.

Hakika kuna haja ya uteuzi wa Majaji kuchunguzwa upya hii ni aibu kwa Mheshimiwa Rais na washauri wake kwani huu ni mfano mmoja tu wa majaji uozo, Je, wako wangapi wa sampuli yake?


Swali la msingi la kujiuliza ni:
Je, ni raia wema wangapi wameathiriwa na hukumu butu kama hizi hizi za Jaji Gabriel Rwakibalira na wakatumikia adhabu zisizo sahihi kwa kukosa utetezi wa mawakili makini?
 
Leo asubuhi kwenye kipindi cha Power breakfast watangazaji wa Clouds FM wameongea mengi ya kumbeza Lema na kesi yake. Sijui sasa hivi wanajisikiaje baada ya hukumu kusoma.

Ombi langu kwa vyombo vya habari:
Msioneshe waziwazi kwamba mnaegemea upande fulani wa chama cha kisiasa kwani vyombo vyenu hivyo ni vya kibiashara. Jamii ikigundua kuwa mna mlengo flani itawasusa. Mwana JF aliyesikiliza kipindi hicho anaweza akaongeza yale yalokuwa yakiongelewa..

wanajikomba kwa magamba... Amjuwi?
 
Hiki hakiwezi kuwa chombo cha kusifia hata upuuzi eti kwasababu umefanywa na cha pendwa, never. Tuache kukurupuka.
Hapo kwenye red, kunakuhusu wewe na vilaza wenzako wa clouds, mleta mada hajakurupuka, ila wewe na wenzako clouds ndo mnakurupuka, hata mtu akisoma hii post yako ataelewa tu uwezo wako wa kufikiri ni mdogo kama wa kiroboto.
 
hao ndo kawaida yao mim mwenyewe nimewasikia kiukwel iafike mahal vyombo vya habar katika mambo ya ushabik visionyeshe upande vinakoegemea.

hao ndio kawwaida yao imejigeuza uhuru n'a TBC kwa propaganda hivi sasa imebaki kusikilizwa n'a maderreva n'a makkonnda wa daladala
 
Hiyo ni studio ya freemasons hamkumbuki "sir chande" alikwenda kuangalia mahesabu yake na wakauonesha umma huyo mzee akitoka huko na mkongojo wake? Tuwaombee toba kwa MUNGU atusamehe kwa niaba yao HAKIKA hawajui walitendalo
 
Nani asiye a kuwa clouds ni wanafiki na wazandiki?

Hawa wanajua kupambanua kila kitu na si kwa uyakinifu bali kwa standard wanazojua na walizo jiwekea wao (double standard).

Hiki chombo kinamatatizo sana.
 
Back
Top Bottom