Kenneth Nollo
Member
- Dec 20, 2012
- 98
- 18
Hakuna redio nzuri kama Clouds fm hasa kipindi cha Power BREAK FAST! Jamaa hawa egemei itikadi yoyote!
nimekuwa mshabiki kwa sehemu wa kusikiliza redio ya clouds FM asubuhi nikiwa kwenye foleni.Lakini leo nilijuta niliposikia maneno ya kejeli na dhihaka dhidi ya gazeti la Tanzania Daima lililoongea kuwa "hukumu ya Lema ni ya kihistoria".Hata kama asingeshinda mimi ningeona ni ya kihistoria kwa CDM tungekuwa tumenyang'anywa jimbo na Ikulu.Hii ilishatamkwa wazi na Lema na Ikulu haijapinga kwa lolote.Sasa Gerald akajifanya hakuna chochote kipya katika kesi hii na anashangaa gazeti na wananchi wa Arusha na wanachama wa CDM kushabikia kesi hii.SASA M4C TUMESHINDA.GERALD UNASEMAJE PAMOJA NA PJ WAKO?.Nyinyi ni vijana wenzetu,mbona tunakulana wenyewe?
Redio hawatakiwi kuwa wanaaa hebu Jiulize hivi kutokana na makala hii huwaoni kama hao watangazaji ni wazembe?;
Hakika kuna haja ya uteuzi wa Majaji kuchunguzwa upya hii ni aibu kwa Mheshimiwa Rais na washauri wake kwani huu ni mfano mmoja tu wa majaji uozo, Je, wako wangapi wa sampuli yake?
Swali la msingi la kujiuliza ni:
Je, ni raia wema wangapi wameathiriwa na hukumu butu kama hizi hizi za Jaji Gabriel Rwakibalira na wakatumikia adhabu zisizo sahihi kwa kukosa utetezi wa mawakili makini?
Nilimsikia hata mie nikamshangaa sana. Huwa nawaheshimu sana hawa jamaa lakini leo nilishtuka sana. Uhistoria wa kesi ya Lema unatokana na mambo yafuatayo:
1. Hukuma za mahakama hutunga sheria yaani hukumu iliyopita na haikuwa challenged inaweza kutumika kutoa hukumu nyingine. Hii hukumu kila mtu hata CCM wenyewe walijua ni hukumu mbaya ni vile tu mahakimu/majaji wana kinga. Kusimama kwa hukumu hii kunge-set precedence mbaya iliyowahi kutokea katika sheria.
2. Lema alichaguliwa na wananchi kwa kura nyingi sana akimshinda Mama Buriani kwa mbali. Kwa kutumia haki ya asili (natural justice) haikuwa sahihi kuwanyang'anya wananchi wa Arusha Mbunge wao kwa sababu ambazo hazikuathiri matokeo kwa namna yoyote ile.
3. Mama Buriani hakuwahi kutokea mahakamani kutoa ushahidi wa kutukanwa na Lema, wala hakufungua kesi ya madai ya kudhalilishwa. Kosa kama hili ni lazima muhusika mwenyewe ajitokeze. Na hata hivyo adhabu yake haingekuwa kumvua Lema ubunge wake.
4. Kosa la kumtukana mtu ni la jinai. Mtuhumiwa anatakiwa ashitakiwe na Jamuhuri, aliyetukanwa anakuwa shahidi. Hakuna polisi waliomshika Lema na kumshitaki kwa kutenda kosa la jinai. Na hata hivyo adhabu yake ni faini, au kifungo au vyote kwa pamoja. Nadhani kila tusi ni kama miezi mitatu hivi.
5. Kushindwa kwa Lema kwenye rufaa hii kungeweka record mbaya kabisa katika utendaji wa mahakama.
6. Kushida kwa Lema kwenye kesi hii kunaweka record ya pekee ya ujasiri wa Majaji kuamua kwa uhuru kesi ambayo kwa namna kubwa Serikali ilikuwa na maslahi yake. Kwa hiyo Lema ameshinda kesi against all odds. Ni historia kwa kweli
Kwa hivyo Jerad Hando na PJ wawe wanafanya fair analysis badala ya kuponda kwa mrengo wa kupendelea upande fulani. Ushindi wa Lema ni ushindi wa mfumo wetu wa sheria na mahakama. Hiki siyo kitu kidogo hata, wakumbuke Jaji Mkuu alijitoa kwenye kesi hii. Tusifanye speculations lakini wahenga walisema ukiona moshi basi ujue kuna moto chini au dalili ya mvua ni mawingu au La kuvunda halina ubani. Tuwe makini hapo Clouds tufurahishe wasikilizaji lakini tukumbuke ku-balance mambo.
Kama mnataka kusifiwa Chadema anzisheni redio yenu,pro chadema mmekua watu wa kuchukia watu wote ambao wapo analytical!
hapa nadhani mnawachafua clauds bure,tafadhali mfanye tena utafiti wa kina kujua mnachokisema kama ni sawa