Ushawahi kutumia mbinu chafu kufaulu masomo?

Kenenisa

JF-Expert Member
Feb 13, 2021
564
1,100
Uhali gani mwanaJF,

Rejea kichwa cha habari hapo juu.
Kuanzia shule ya msingi mpaka a-level nilikuwa mtakatifu (Clean student) nikifaulu kwa juhudi zangu.

Hali ilibadilika baada ya kuingia chuo kikuu. Nikaanza kuwa muhuni na kuwa top cheater nikitumia mbinu zufuatazo
I) Kuandika mkononi au kwenye shati formula mbalimbali.

2) Kuweka daftari la kozi husika toilet na katikati ya mtihani naomba ruhusa ya kwenda toilet kumbe naenda kuangalia majibu ya maswali yaliyonishinda

Je, wewe ushawahi kutumia umafia gani kufaulu kwenye elimu yako?
 
Uhali gani mwanaJF

I)Kuandika mkononi au kwenye shati formula mbalimbali
2)Kuweka daftari la kozi husika toilet na katikati ya mtihani naomba ruhusa ya kwenda toilet kumbe naenda kuangalia majibu ya maswali yaliyonishinda

Je, wewe ushawahi kutumia umafia gani kufaulu kwenye elimu yako?
Kweli nimeamini kuna matendo usipoyafanya katika umri unaostahili kuyafanya basi unakuja kuyafanya katika umri usiostahili
 
2)Kuweka daftari la kozi husika toilet na katikati ya mtihani naomba ruhusa ya kwenda toilet kumbe naenda kuangalia majibu ya maswali yaliyonishinda

Je, wewe ushawahi kutumia umafia gani kufaulu kwenye elimu yako?

Tuliwahi kufanya hivi kwenye Supplementary, mlinzi akagundua akaenda kulitoa. Tulipoenda kupiga chabo kwa kisingizio cha kwenda Toi tukalikosa
 
Kasheshe ilikua kuna malecturer walikua nuksi sana, hasa wale waliopiga Upper First na kushikwa mkono kuwa enrolled tu na chuo kufundisha na kusimamia wanafunzi. Wanakua viherehere kama chuo cha baba yao vile!

Yaani ma bingwa kwa kuharibu formation. Ukimuona tu kaingia chumba cha mtihani ujue anakuja kuchana mkeka. Dakika 5 nyingi ukicheki kushoto winga amekabwa, kulia winga amekabwa. Midfield kati kapotezwa! Hapo ndio utajua hujui!!!

Full patol kama defender la polisi.

Hapo mtihani lazima ukupige kipigo matata, mpaka unajikuta unatamani kusimama ghafla na uanze kuwa na we invigilator wa mtihani.
 
Mbinu rahisi kuliko zote ni kuingia na karatasi ya majibu hasa unapokisia maswali fulani yataulizwa au tayari umeuona mtihani. Kiujumla kuingia kwenye chumba cha mtihani huku una majibu yaliyokokotolewa huko ni kukosa akili. Utamu wa kufaulu mtihani uingie chumba cha mtihani ukiwa huna majibu au hukufanya mbinu zozote kuvujisha mtihani. Kujiamini kufanya mtihani bila mbinu za kimafia ndiyo akili yenyewe inayotakiwa
 
Uhali gani mwanaJF,

Rejea kichwa cha habari hapo juu.
Kuanzia shule ya msingi mpaka a-level nilikuwa mtakatifu (Clean student) nikifaulu kwa juhudi zangu.

Hali ilibadilika baada ya kuingia chuo kikuu. Nikaanza kuwa muhuni na kuwa top cheater nikitumia mbinu zufuatazo
I) Kuandika mkononi au kwenye shati formula mbalimbali.

2) Kuweka daftari la kozi husika toilet na katikati ya mtihani naomba ruhusa ya kwenda toilet kumbe naenda kuangalia majibu ya maswali yaliyonishinda

Je, wewe ushawahi kutumia umafia gani kufaulu kwenye elimu yako?

aisee kuna kikaka kilikuwa kinanipenda pale MUHAS alikuwa anaingia na simu afu mimi nakaa nyuma yake akimalz pepa ananipasia aisee popote ulipo japhet Ubarikiwe
 
aisee kuna kikaka kilikuwa kinanipenda pale MUHAS alikuwa anaingia na simu afu mimi nakaa nyuma yake akimalz pepa ananipasia aisee popote ulipo japhet Ubarikiwe
Daktari sasa itakuaje nikija kutibiwa na ulidesa paper
 
Kuna hii mbinu unaandika majibu (possible ) kwenye answer sheet kama vile ni mtihani umefanywa unasubiri tu kukusanywa

Nusu saa au lisaa baada ya mtihani kuanza unatoa missiles zako na kuanza kuzifanyia kazi bila msimamizi kugundua kwamba mzigo umeandikiwa nje ya chumba cha mtihani

Kuna kipindi unaweza kuta answer sheet uliyoandika majibu inatofautiana na answer sheet walizogawa kwa ajili ya kujibia hapo mbinu zingine za kimedani lazima zigusishwe

NB: Mwalimu wangu wa kinge aliniambia "intelligence is to know where the right answers is"
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom