Mbinu za kutumia ufaulu mitihani yako

MMASSY

JF-Expert Member
Jan 13, 2011
290
193
Tunapatikana Arusha, tupigie au tuandikie tutakufikia.

Kitabu hiki ni kizuri sana kwa wanafunzi wa ngazi zote. Lugha yake na mifano iliyotumika inamfanya mwanafunzi kuelewa kirahisi na maelekezo yaliyotumika yanamfanya msomaji wake aweze kuelewa kirahisi sana mbinu na mikakati ya kukabiliana na changamoto za maandalizi ya mitihani na hata zile za wakati wa kujibu maswali katika chumba cha mtihani.

Kufaulu mitihani hakutokani na uwezo wa mwanafunzi kukariri kile alichojifunza darasani, wala hakutokani na bahati nzuri. La hasha! Kufaulu ni matokeo ya utayari wa mwanafunzi kujifunza, hutokana na bidii ya mwanafunzi kusoma kwa bidii na ni lazima mwanafunzi huyu afundishwe namna ya kukaa kama mwanafunzi, ili mwanafunzi afaulu lazima ajue ni kwanini yuko shuleni; ndio maana katika kitabu hiki mwandishi ameandika kwa kina kumfundisha mwanafunzi sababu za yeye kuwa shuleni na umuhimu wa kusoma kwa bidi ili afaulu mitihani yake.

Ni ukweli usio na kikomo kwamba ili mwanafunzi afaulu masomo yake ni lazima aondokane na dhana potofu juu ya elimu kama vile, “Mimi nasoma ili niwe kama nani wakati nina ndugu zangu wamesoma lakini hawana maisha bora?”Au “mbona jirani yetu hajasoma lakini ni mfanya biashara mkubwa na ana maisha mazuri kuliko ya kwetu wakati baba na mama yangu wamesoma na wanafanya kazi ofisi zenye mshahara mkubwa?” Kitabu hiki kinatoa mafundisho mazuri sana katika eneo hili ili mwanafunzi awe na munkari ya kusoma kwa bidii na kufaulu mitihani yake kwa kiwango cha juu sana.

Kitabu hiki kimeandikwa kwa utaalamu na ufundi mkubwa. Mwandishi anamwonyesha mwanafunzi sababu zinazowafanya wanafunzi wafeli mithani yao, mbinu na mikakati ya kusoma ili mwanafunzi aweze kuelewa kile anachokisoma ni shemu muhimu sana katika ufaulu wa mwanafunzi, ndio maana mwandishi akachambua kwa kina eneo hili ili mwanfunzi aweze kutambua na kuzitumia mbinu hizi na baadaye afaulu kwa kiwango cha juu mitihani yake.

Kitabu hiki pia kinafundisha kwa kina mbinu bora za kujiandaa na mtihani, ufahamu wa kinachotakiwa katika maandalizi hayo na mikakati ya nini mwanafunzi awapo katika chumba cha mtihani akifanye.Zipo kanuni(Principles) katika kitabu hiki ambazo mwanafunzi akizitumia lazima ataibuka mshindi katika kila mtihani atakaoufanya.

Uwe wa wiki (weekly tests) wa mwezi (monthly test) au hata wa muhula na baadaye wa chuo au ule wa taifa(Necta). Yapo maisha ambayo mwanafunzi akiyaishi awe nyumbani au shule yatamjengea mazingira ya kufanikiwa katika masomo yake, na zipo tabia ambazo mwanafunzi akiwa nazo lazima atafaulu mitihani yake.Yote hayo yameelezwa kwa mifano hai katika kitabu hiki.

Kitabu hiki kinalenga kumtanabaisha mwanafunzi juu ya namna gani ajiweke/ afanye ili hatimaye apate matokeo mazuri.Kumbuka katika nchi yetu, na katika nchi nyingi za Kiafrika, mtihani unatumika kuamua ufaulu wako katika taaluma kwa kiasi kikubwa sana.Inawezekana ukawa na uelewa na uzoefu mkubwa katika jambo flani kubwa, lakini kitakachokufanya uitwe katika usaili ni ufaulu katika cheti chako kwanza, ndio baadaye waangalie unafauluje huo usaili.

Ukisoma matangazo mengi ya ajira utagundua wanataka watu wenye GPA ya ngazi flani mathalani 4.5.

Kwa wale walio na mitihani ya taifa hasa kidato cha pili, cha nne na cha sita,kitabu hiki ni msaada mkubwa sana kwao katika kuamua mafaniko yao katika matokeo yaani wakiweza kutumia kanuni hizi wakati wakijiandaa na mitihani yao ya taifa, zitawasaidia sana katika kufaulu mitihani.

Kitabu hiki kinatoa mwaliko kwa wazazi, walimu, walezi na wanafunzi katika mtazamo mpya wa matumaini katika taaluma,mtazamo chanya kuwa kufaulu kunawezekana. Mara nyingi kufaulu kunachangiwa na kile ambacho kimeelezwa katika kitabu hiki.Kupitia kitabu hiki, mwandishi anatoa njia ama kanuni anuai zitakazomsaidia mwanafunzi kufanya vizuri katika mitihani yake kama atazifuata na kuzizingatia.

Kanuni hizi zimetengenezwa kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa elimu wakiwemo Walimu mashuhuri, wanafunzi waliofaulu sana mitihani yao ya kitaifa, wataalamu wa elimu kutoka taasisi mbalimbali, wazazi, viongozi na makundi mengine mbalimbali kwenye jamii ambayo yana mapenzi ya dhati kwenye sekta hii ya elimu.

Kijitabu hiki ni msaada kwa; Mzazi, Mlezi, Mwalimu na mshauri wa wanafunzi hasa katika masuala ya taaluma kupata mbinu zitakasomsaidia mwanfunzi/wanafunzi afanye vizuri katika masomo yake. Ni kitabu ambacho tunatamani kila mwanafunzi, mzazi, mlezi, mwalimu na hata shule iwe nacho ili kuiinua kitaaluma.

Jerome Mmassy
Mwandishi mwandamizi na Mkurugenzi Mtendaji
Holy Hands Book Project
+255(0) 758673441
 
Tunashukur sana mkuu , Good lesson
Muonekano wake
IMG_20180920_111454_368.JPG
 
Back
Top Bottom