Ushawahi kutongoza/ kutongozwa na jini? Ikawaje?

Ushawahi kutongoza/ kutongozwa na jini? Ikawaje?

Mwenye stori yakweli aje asimulie hapa,naona watu wanarukaruka tu.
 
Mbezi, ya Africana, kuna beach ile ipo jiran na jeshi, kwa wanaopafahamu watakuwa wanapaelewa, pale kuna mdada mmoja mmoja anapiga moja matata sana, mfano wa Sanchi, nimewahi kupishana na Yule dem Kama mara tatu hivi na mara zote Mimi nikimuona Kama mwanamke mrembo anayetoa moto mdomo ni huku we zangu wakiona Kama ni kundi kubwa la Nyuki linakuja mbele, huyu ndio alikuwa wa kwanza kumi fanya macho yangu yaani even kuwatambua hawa viumbe, Safari ili anzia hapo..huyo sikuwa hi kutongoza wala kujaribu kufikiria kufanya hivyo kwa maana nilikuwa nikimuona Mimi we zangu hawamuoni, wanachoona ni nyuki, naanza na huyu.
Mkuu mbona humalizii
 
Mm nilimkuta binti mrembo kituo cha basi mwenge usiku saa 4 kavaa jeans black na t-shirt red akiomba lift. Nikasimama, nikamuuliza anaenda wapi? akadai sio mbali ni tangi bovu tuu. Nikamchukua akakaa kiti cha nyuma (corola). Kufika karibu na tangi bovu nikataka kumuuliza ndio hapa unashuka? Kuangalia nyuma hayupo! Daaa, nikapaki gari nikaangalia kama kadondoka? Sikuamiani nilichokiona, basi kuulizia kesho nikaambiwa ni kawaida yake hilo jini kwa njia hiyo.
 
Majini ya kike kidogo tabia zinafanana hasa wale waopenda mahusiano na wana damu, ni wanawake wapole, wasafi muda wote, wengi hype delta kuwa na ushungi, na wanapenda sana ngono Nina maana mnapotea ya mapenzi wanatabasamu Mendeleev tu na hapo Kama una kichwa kiburi utam jua tu, wengine hapo ukimpa vitu fresh sijui hujisahau ama kusudi hubadilika.....Leo naanza moja baada ya nyingine jinsi nilivyokutana nao bila kufahamu kwa ndio wao
 
Kabla sijakutana na KAISKA nilikutana na NALKHAT, ilikuwa Morogoro, miaka kumi iliyopita, kipindi hicho nilikuwa Nina Newell nyingi kichwani( nazifunga kwa nyuma) siku moja wakati nimeona kituo I kupanda daladala kuna dada mmoja dizain alikuwa Kama ananifuatilia hivi, siku tulia maanani sana, nikamchukulia kama ni abiria tu Kama Mimi, bahati mbaya nikapata Siri ambayo tulikaa pamoja, nikamsalimia akaitikia vizuri tuu, nikimuangalia vizuri ni pini sio kitoto pia alikuwa na lafudhi ya kizanzibar, tukatokea kuzoeana sana, mwisho, akasema amezipenda nywele zangu, pia yeye ni msusi mzuri kama sitojali angependa anirekebisha siku nikiwa na muda, nikamwambia kesho nina muda ambayo ilikuwa ni jumapili Kama Leo, mi nilishuka nae aka shuka kituo hicho hicho, lakini Mimi baada ya kushuka nilitangulia sababu sikutaka kufahamiana nae kivile,

Baada ya masaa kama mawili hiv simu ikaita naangalia jina la Yule mwanamke wa katika daladala, sikumpatia namba yangu, wala sikuchukua yake,

Nikapokea akasema kama sitojali anaona aje home apajue ili kesho yake aje mapema, nikamwambia sawa, nikamuelekeza, ajabu Ankara simu mlango unagongwa nachungulia dirishani napokelewa na harufu ya marashi na tabasamu moja matata sana..

Nikastuka kidogo kwa tulio lile ila nikajisemea huyu kuna analolitaka, mbona anajileta hivi? Poa mi nilifungua akazama ndani...aisee Yule mwanamke alikuwa ni mzuri mno na vile alijistiri, kaacha sura tuu.....

Naendelea hapo chini kuna ufumbuzi napata ktk hiki kidude ninachitumia kuandika hii kitu.
 
Mtaniwia radhi kunakuwa na meneno inaonekana Kama nimekosea kuandika lakini sivyo dhamira iPad imeamua kunizingua Leo


Nilimuuliza Kama anatumia kinywaji chochote akasema hapana, akasema sa hizi ni saa kumi, naomba Kama hapa nikurekebishe kichwani nikaona poa, mine huyo katikati ya miguu ya bible, yeye alikaa juu ya sofa Mimi nimekaa chini, aliposhika tu kichwa changu nilihisi vitu vinasisimka mwili mzima Kama shoti flani na hata yeye alistuka, nikamsikia akisema nisamehe..wewe uko vizur sana, je unalijua Hilo, mi nikamwambia sijui kwani vipi? Wakati huo nilikuwa naskia nywele zinakaza nikajua ananisuka lakini haikuwa hiyo, Yule mwanamke kuna jambo lilimsibu aliponishika, nikamsikia tena akisema nisamehe tena.. Naomba nikumalizie niondoke na wakati namalizia kumwambia poa, yeye akasema tayari...we kijana mzuri....niliposikia kijana mzuri, nikapaniki kidogo aje mtoto wa kike aniite mzuri, alafu aje tu, anilekebishe kichwa ndani ya dakika? Nikiwa vilevile nimekaa, nikamshika mikono yake kuivuta kwa mbele, aisee nilihisi Kama nimeshika miguu ya mbele ya mbuzi..akawa Kama anajizuia nisione, nikamwambia nimeshakujua acha nione ila ki ukwel mkojo ulishaanza kuuma na mwili kuishi wan guvu nilijikaza tu, kweli ile mikono ilikuwa kama ya mbuzi na ni ya kijani, kijani kabisa
 
Nikageuka kumwangalia sura, alikuwa na sura ileile ya kibinadamu ila mikono mfano wa mbuzi, na macho yake yalikuwa ya kijivu ila yanayong'aa sana, nikamuuliza? Ninaota? Akasema huoti hii ni Real, nimekupenda sana na ninashindwa kujizuia lakini mwili wako una kinga ndio inayonifanya niwe hivi...duh niliposikia ninakinga kidoogo nikaona hapa naweza salimika, nikamuuliza je nifungue mlango? Maana mi hapa nakuogopa na natamani utoke uondoke zako na usirudi...akanitaja jina na kusema we usijali mi ni rafiki mwema tu kwako wala sijawasiliana kumdhuru mtu maisha yote niliyoishi ila watu ndio humid huru Mimi, kama wewe umenidhuru nilipokushika kichwa nilikuwa naungua mikono..mie Duuuh.....
 
Alirudi katika Hali ya kawaida nikamwambia tukakae kibarazani nje tuongee kweli alikuwa like nikawa naongea nae, na majirani wakijipitisha kuona chuma ninachopiga Nacho stori, yaani wangejua, wala wasingekuwa wamsifia...tuliongea hadi saa kumi na mbili jioni akasema anarudi kwake kusali, nikamuuliza kwako ni wapi, akajibu Zanzibar, my nikamwambia haya, ahsante kwa kukufahamu...aliniuliza kitu wakati anaondoka kwamba? Bado namuogopa?nikamwambia eeh kidogo Iola simuamini, akasema kesho nataka tufanye mapenzi siku nzima, nikamuuliza unayo ya kawaida Kama ya binaadamu akasema Yap..nikamwambia poa....akaondoka anacheka, huwezi amini alipotoka tu, mi mbili nikafunga mlango, vaa viatu huyoo mpaka msamvu nikapanda abood ya mwisho, huyoo dar, nikahisi nikilala pale, naweza kulaliwa.
 
Huyo ni wa kwanza alikuwa ni Mpole sana, mstaarabu na muda wote yupo Kama binaadam labda aje mjinga kumzingua....alikuwa ananipenda sana Iola wivu na kupenda kufanya mapenzi muda mrefu kuleni fanya nimtafute njia ya kumkwaza asepe....bado ya huyu kisu rani KAISHKA.
 
Majini huwa wanatoka wapi? Ni kwamba wana nchi yao? Nani aliwaumba? Kuna majini wacha Mungu kabisa? Naomba mwenye jibu anipe kwa sababu wakristo sisi hatufundishwi habari za majini
 
Ukikutana na jini hutatamani kumwachaa ila uwe shujaa wakati fulani.
Nilikutana na chini anakwenda shule evening class, akanambia anasoma ili kurudia mtihani wake wa kidato cha nne...
Nilimshawioshi asiende shule badala yake tukaenda geto... yaani anaomba kitu kama huna basi kufumba na kufumbua kinapatikana mfano...anaomba maji ya chupa ukisema duka lipo mbali unashangaa anafunua shuka na kutoa maji.kiboko ni pale alipotaka dinner nikajibu huwa sipiki labda twende tukale kwa mama mtilie, akajibu kwani wewe unapenda kula nini? nikajibu kitimoto...akanichapa kibao mzee nilishangaa nini tena nikajifanya nimemaind nikatoka nje kuzuga...niliporudi nikakuta mashuka tu...
Haaaaahh,umenifurahisha sana mkuu .Naipenda sana jf jamani hata kama ukiwa kiazi vipi hapa utakwiva kwa sababu NO stress!
 
Huyo ni wa kwanza alikuwa ni Mpole sana, mstaarabu na muda wote yupo Kama binaadam labda aje mjinga kumzingua....alikuwa ananipenda sana Iola wivu na kupenda kufanya mapenzi muda mrefu kuleni fanya nimtafute njia ya kumkwaza asepe....bado ya huyu kisu rani KAISHKA.



unazingua ujue...story yako unaibania..tiririka
 
Kaka muda, hapa niko natafta rizki kwanza si unajua tena Hali tuliyo nayo, ninapotulia ndio natupia
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom