Ushawahi Kupendwa Mpaka Ukawa Unahisi Kero?

Ushawahi Kupendwa Mpaka Ukawa Unahisi Kero?

Wakuu
Katika maisha ya mahusiano tunapitia mengi,unaweza ukapendwa sana mpaka ukawa unahisi ni kero sasa

Mtu kila saa anakutafuta,anakutumia text,anakupigia,ukimjibu au ukichelewa kumjibu anakulaumu na "mbona kimya" zinakuwa nyingi

Hali hii mimi binafsi huwa siipendi na ikitokea mwanamke wa namna hii basi nampiga chini haraka sana,siwezi kuwa saa niko na simu tu nachati au naongea na wewe kama nimekosa kazi ya kufanya.

Nimeachana na first11 ya wanawake dizaini hii.

Usawahi kudate na mdada au mwanaume wa namna hii? Hali ilikuwaje,ulikabiliana nae vipi na mahusiano yako bado yapo?
Cc Binti Sayuni03
Hao sio wa kuchezewa ni wa kuoa,kwa mchezeaji lazima uone kero...
 
Huyu kadogo2 nae muongomuongo mwezi uliopita alikuwa analialia hapigiwi simu wala hamjali,mwezi huu kapata wa kumpigia simu anamjali anasema anamkera kweli mwanamke hajui nini anataka
😂😂 hujanielewa tu nilicho maanisha
Hakuna mtu hapendi kutafutwa tafutwa ila kuna mipaka jamani
Yule niliokuwa nalialia alikuwa hanitafuti kabisaa yaani unaweza kaa siku 4 mpk wiki yupo kimya sasa hapo si lazima ujisikie vibaya

Mahusiano ambayo yananoga ni yale ya kiasi amekutafuta Asubuh na mchana na muda wa kulala inatosha
Sasa unakutana na mtu kila saa anapiga simu anatuma sms na hana cha maana cha kuongea huo unakuwa ni usumbufu… mtu anakupigia simu mara 15 kwa siku kama umezaa nae vile anaulizia hali ya mtoto wake aiseee mimi hayo mahusiano siyawezi

Kipindi kile nalialia humu sio kwamba nilikuwa sitongozwi na wengine nilifuata ushaurii wa wengi humu kusema kwamba jamaa hanipendi.. hivyo nilianza ku move on nikamkubali mtu mwinginee ambae yeye ananielewa zaidi
Hatutafutani kama tunadaiana ila tunawasiliana haiwezi pita siku hatujawasiliana hayo ndio mahusiano nayo yatakaa Joannah
 
Back
Top Bottom