Ushauri wa Zitto kwa Lema na RC Gambo

Ushauri wa Zitto kwa Lema na RC Gambo

HIVI MUNGU HAJUI NANI KAFANYA NINI MPAKA TUTUMIE NGUVU ZOTE HIZI KUONYESHA NANI KAFANYA NINI? HIVI HUU MRADI NDIO UTAMFANYA LEMA ADUMU KUWA MBUGE? MBONA AMEKUWA MBUNGE BILA YA HUO MRADI KUWEPO?
KAMA ALIVYOSEMA ZITO HII NI AIBU KWA VIJANA
Wewe comte mbona unaharibu jina,huyu comte alikuwa mmoja kati ya wanafalsafa wakubwa,ana nasharia nyingi za kufikirisha.Mbona hulitendei haki hilo jina?

Unamjua Yesu Vizuri wewe au unakisia tu,hataYesu mwenyewe kabla ya kuachana na wanafunzi wake alitaka "Recognition".Yesu alitaka kujua je hata wale walio karibu yake wanajua yeye ni nani na mchango wake ni upi?Ndio maana aliwauliza wale wanafunzi wake "Eti mimi ni nani na watu wanasema mimi ni nani?

Wale wanafunzi wake wengine wakasema aaaa wewe wanasema Nabii Elia,mara Musa mara ooo!!Yesu akamuuliza Petro...Petro mimi ni nani?Pale pale Petro akasema,wewe ni Yesu Kristo mwana wa Mungu aliye juu...Hata kabla hajamaliza,pale pale Yesu akampa Petro "shavu"...Kwamba wewe ndio Peteo (Kefa) na juu ya mwamba huu nitalijenga kanisa,utakalolifunga duniani na mbinguni litafungwa.....Yaani baada ya "Recognition" tu,Yesu akampa shavu Petro...
 
Nakasirishwa sana kuona viongozi vijana wanafanya mambo ya hovyo. Mkuu wa mkoa wa Arusha mdogo wangu Mrisho Gambo una dhamana zaidi kwa vijana. Mnapofanya mambo ya kijinga mnaharibu nafasi ya vijana kuaminiwa zaidi. Kaa na Mbunge Godbless Lema mnywe kahawa pale New Arusha na muanze upya. Ndugu yangu Lema nashauri punguza munkari. Juhudi zako Arusha haziwezi kufutika kirahisi. Nakushauri kaa chini na Mkuu wa Mkoa wako mpige mstari muanze Kazi upya kwa pamoja. Viongozi jiepusheni kuonyesha hasira zenu hadharani. Sio hekima.
Umeutoa wapi ujumbe huu? Kama wewe ni Zitto au rafikiye, you are very wrong! Labda kama huijui safari ya mkuu wa mkoa huo hadi kufika hapo. Kuna tabia zisizoondoka kwa mahubiri.
 
Bila kujali nani alisababisha mvutano huo wa aibu, lakini picha iliyochorwa vichwani mwa wafadhiri hao ni kwamba watanzania hatuelewani. Hii ni aibu na mbaya zaidi mwakilishi wa rais akituhumiwa kuhusika kuvuruga mkutano.

Tukio hilo ni kashfa kabisa na ni aibu kwa taifa ambalo linajipambanua kuwa ni lenye umoja na mshikamano kwa wananchi wake. Rais Magufuli afuatulie kiini cha mzozo huo na kuchukua hatua kukomesha tabia hiyo ya aibu.

 
Huzijui siasa za Arusha, wala hujui mkakati wa CCM dhidi ya Arusha. Una hekima lakini huwezi kutumia hekima hiyo kwa kinachofanywa na Gambo! Na ukweli reaction ya Lema iko pouwa, na ndio pekee itakayoisaidia nchi katika mazingira ya sasa. Hekima hupelekwa kwa wenye hekima!

Mwana siasa hujijenga mwenye ,kwa kutumia palaform kama media , kitendo alichofanya lema hatakaa aalikwe kwenye media yoyote hapa tanzania , labda cdm ianzishe media yao
 
LEMA ameonekana live akileta fujo kwenye hafla ya uzinduzi wa mradi kwa kuingilia hotuba ya mgani rasmi.Je sheria inaruhisu kwa Lema kuchukuliwa hatua?
 
Mkuu Zitto hivi unashushaje "munkari" kwa mtu aina ya Gambo?RC mwenye kisasi na fitina kila wakati??

Ni bahati mbaya watu wengi wanaliona hili tukio ktk "clip" ya vipande vipande.Bwana mdogo Gambo hakufanya uungwana toka mwanzo;alialikwa lkn hakutaka kuja kwa sharti la Lema kutokutakiwa kuwepo yeye atakapokuwapo.Hata alipofika mesa kuu;alitoa mkono kwa watu lkn akamruka Lema.Hii ilikuwa "indicator" tosha kuwa RC kaja kwa shari.Mkuu wakati mwingine mbwai mbwai tu...kama mtu ana madaraka na jeshi la kukuweka ndani,basi wewe uwe na ujasiri na uthubutu wa kuukemea uonevu;hata kama huwezi kumpiga mtu;basi hata mchukie na kumkaripia tu...hii ndio silaha iliyobaki lwa Lema.

Jitihada zikafanyika kwa kumpigia katibu mkuu kiongozi;akiwa kama sehemu ya mamlaka ya juu ya RC atumie nafasi yake kumshawishi mkuu wa mkoa kufika ili pawepo na uwakilishi wa kiserikali katika jambo la heri kama lile;baada ya kutakiwa na "watu wa juu" kufika bado Gambo alichelewa sana eneo la tukio;na hata alipofika aliamuru MC asimpe Lema nafasi ya kuongea na akataka yeye ndio aanze kuongea ili kuuwa protocol,na kwa sabb ya itifaki,angeongea yeye kulikuwa hakuna "room" tena ya Lema kuongea na upotoshaji ule ungemea kama mmea kandokando ya kijito.

Ili kuweka historia sawa,Lema ilibidi aseme palepale,maana hata hao wafadhili huyo Gambo hawamjui,mkataba uliingiwa na Lema wakati Gambo akiwa Korogwe akimtukana Mwanasheria wa Wilaya ya Korogwe kuwa ana degree ya chupi.Hao Maternity hawamjui Gambo kwa sbb wakati wanaleta ramani ya hospitali ya Mama na Mtoto pale Arusha,Gambo alikuwa kwenye kizimba cha Tume ya Maadili ya Utumishi wa Umma akijibu mashitaka yake ya kukiuka taratibu za utumishi wa Umma.

Ukiwa hujawahi kukaa katikati ya siasa za Upinzani Afrika utamuona Lema "Chizi".Lkn ule ndio upinzani wa Afrika,lazima uwe chizi,lazima ujifyatue kudeal na watu aina ya Gambo.Vijana wasio na rekodi yoyote ya maana ktk utumishi wa umma,unatia aibu kwa kuanza kuelezea historia ya ujenzi na umiliki wa kiwanja kwa maneno ya vijiweni badala ya documents.Ile ni aibu,aibu kwa aliyemteua na anayemuacha Gambo kwenye nafasi ile mpaka sasa.

Nina milion 6.5,nikipata laki tano naweza kufunguka zaidi,kwa sasa ngoja niishie hapa,Nitafungwa;lkn Gambo aache uhuni,asijipendekeze kijinga jinga;historia itamuhukumu.Hakuna Ukuu wa Mkoa wa kudumu.
Asante Mkuu,pia pole kwa kuwa sehemu ya watanzania wanaovumilia kuwa watanzania.
Inauma sn,haka ka nchi kana viongozi ambao ni maajabu.
 
LEMA ameonekana live akileta fujo kwenye hafla ya uzinduzi wa mradi kwa kuingilia hotuba ya mgani rasmi.Je sheria inaruhisu kwa Lema kuchukuliwa hatua?
Hii ni chuga jomba sio simiyu mb.ula
 
Someone will be assassinated soon Lema si mtu wa mchezo mchezo "I am Sorry for this nasty comment"
Umeongea mdomo usinuke tu sio ? Vitu vingine muwaze mara mbili kabla ya kuandika "assassinated" maana yake nini ?
 
Watu tulio nje ya mkoa wa Arusha ni sahihi tusingeona jinsi Mh Lema alivyopuuzwa. Ila wale waliondani ya mkoa, ambao wamemchagua Mh Lema wanajua ukweli upo wapi. Malengo ni mawili.
1. Hospitali ijengwe ndio lengo kuu
2. Kuondoa sitomfahamu kwa wadhamini wetu.
NB. Lakini kilichotokea nadhani hata wale wadhamini wametushangaa, kama mradi ulitarajia kuanza hivi punde basi tayari tumesha haribu.
Pengine hili usikute lilipangwa makusudi ili hao wadhamini waondoe huo ufadhili wao ,Kinondoni walitaka kutengeneza kiwanda cha kuchakata takataka tupate mbolea na kuweka jiji safi matokeo yake serikali yetu hii sikivu na takatifu ikaweka kodi kubwa kwenye hiyo mitambo,yaani mtu akupe msaada halafu huo msaada alipie na kodi ? ili tu wasifanikiwe kisa upinzani ndio wanaongoza

Hao wanaotakiwa washushwe waishi kama mashetani ndio mashetani wenyewe wanao tuongoza
Kwa mwendo huu wacha tupoteze miaka 5 bure mpaka tutakapo pata akili na ujasiri wa kukataa udhalimu hadharani
 
Eti Mgambo aliyeteuliwa na mtu mmoja tu (baba Jes.ca anataka ashindane na Lema aliyechaguliwa na wakazi wote wa jiji la Arusha, kama si upuuzi ni nini?
 
Zuberi amesema ukweli, Gambo kawadhalilisha vijana wenye uwezo wa kuchukua nafasi za kiuongozi, kitaaluma na hata za kisiasa. Huyu jamaa hafai kuwa mkuu wa mkoa.

Lema nae ana hasira za kijinga, hana uvumilivu na ameendeleza ile dhana kuwa waafrika bado hamnazo. Angetumia njia nyingine kufikisha ujumbe wake baada ya "kupuuzwa"!!
Hivi ni njia gani kwa mfano ulitaka Lema aitumie kufikisha ujumbe wake ? Hebu tupe hizo njia na pia uhainishe ni wapi hizo njia zilitumika nchi hii zikaleta maana kwenye utawala huu

Watu wanafoji barua ya mahakama kuzuia uchaguzi wa meya Dar hapo ni sebuleni kwa raisi hakuna hatua walizochukuliwa ila mama Kilango kusema hakuna wafanyakazi hewa jioni hana kazi

Muda mwingine wacha iwe jino kwa jino ,Felix Ntibenda uliwahi kumskia akikwaruzana na mpinzani yeyote ?
Aliondolewa Arusha tu kwa sababu yeye anasikilizana na watu wote

Kwa mbwembwe Gambo akateuliwa kushika nafasi yake
Sasa atakacho kifanya leo Gambo utanishawishi vipi hakina baraka ya aliyemteua ?

Nachomwambia Gambo kisicho riziki hakiliki hawakuwa wapumbavu hawa wahenga wetu kusema hayo
 
Alipoalikwa kwenye uzinduzi, alijua fika atakutana na mbaya wake hivyo alipaswa kujiandaa kisaikolojia, asingepata aibu zote zile. Hana sifa za kuwa kiongozi kwa kukosa uvumilivu.
 
Taangu nianze Uchumba na mama yako baada ya Ababa yako kufa hajawahi kunitukana kama hivi unanikosea heshima.
Nilipokutukana ni wapi ? Shauri zako ulimi uliponza kichwa

Asante pia kwa matusi ya mama yangu japo ana miaka 90
 
Lema hakuna aibu aliyopata kila MTU anajua juhudi za lema katika ule mradi ata wafadhili wanajua bila lema mradi usingefika pale aliyopata aibu anajulikana
 
Basi sawa wewe unazo!!
"Lema hatakagi ujinga"
 
Back
Top Bottom