Mkuu
Zitto hivi unashushaje "munkari" kwa mtu aina ya Gambo?RC mwenye kisasi na fitina kila wakati??
Ni bahati mbaya watu wengi wanaliona hili tukio ktk "clip" ya vipande vipande.Bwana mdogo Gambo hakufanya uungwana toka mwanzo;alialikwa lkn hakutaka kuja kwa sharti la Lema kutokutakiwa kuwepo yeye atakapokuwapo.Hata alipofika mesa kuu;alitoa mkono kwa watu lkn akamruka Lema.Hii ilikuwa "indicator" tosha kuwa RC kaja kwa shari.Mkuu wakati mwingine mbwai mbwai tu...kama mtu ana madaraka na jeshi la kukuweka ndani,basi wewe uwe na ujasiri na uthubutu wa kuukemea uonevu;hata kama huwezi kumpiga mtu;basi hata mchukie na kumkaripia tu...hii ndio silaha iliyobaki lwa Lema.
Jitihada zikafanyika kwa kumpigia katibu mkuu kiongozi;akiwa kama sehemu ya mamlaka ya juu ya RC atumie nafasi yake kumshawishi mkuu wa mkoa kufika ili pawepo na uwakilishi wa kiserikali katika jambo la heri kama lile;baada ya kutakiwa na "watu wa juu" kufika bado Gambo alichelewa sana eneo la tukio;na hata alipofika aliamuru MC asimpe Lema nafasi ya kuongea na akataka yeye ndio aanze kuongea ili kuuwa protocol,na kwa sabb ya itifaki,angeongea yeye kulikuwa hakuna "room" tena ya Lema kuongea na upotoshaji ule ungemea kama mmea kandokando ya kijito.
Ili kuweka historia sawa,Lema ilibidi aseme palepale,maana hata hao wafadhili huyo Gambo hawamjui,mkataba uliingiwa na Lema wakati Gambo akiwa Korogwe akimtukana Mwanasheria wa Wilaya ya Korogwe kuwa ana degree ya chupi.Hao Maternity hawamjui Gambo kwa sbb wakati wanaleta ramani ya hospitali ya Mama na Mtoto pale Arusha,Gambo alikuwa kwenye kizimba cha Tume ya Maadili ya Utumishi wa Umma akijibu mashitaka yake ya kukiuka taratibu za utumishi wa Umma.
Ukiwa hujawahi kukaa katikati ya siasa za Upinzani Afrika utamuona Lema "Chizi".Lkn ule ndio upinzani wa Afrika,lazima uwe chizi,lazima ujifyatue kudeal na watu aina ya Gambo.Vijana wasio na rekodi yoyote ya maana ktk utumishi wa umma,unatia aibu kwa kuanza kuelezea historia ya ujenzi na umiliki wa kiwanja kwa maneno ya vijiweni badala ya documents.Ile ni aibu,aibu kwa aliyemteua na anayemuacha Gambo kwenye nafasi ile mpaka sasa.
Nina milion 6.5,nikipata laki tano naweza kufunguka zaidi,kwa sasa ngoja niishie hapa,Nitafungwa;lkn Gambo aache uhuni,asijipendekeze kijinga jinga;historia itamuhukumu.Hakuna Ukuu wa Mkoa wa kudumu.