Ushauri wa Zitto kwa Lema na RC Gambo

Ushauri wa Zitto kwa Lema na RC Gambo

Ndugu yangu Chabusalu, hapo umekosea, heshima wananchi wa Arusha kwa Mheshimiwa Lema haiwezi kushushwa na Mhe. Gambo kwa kutotambua mchango wa Mhe. Lema. Ninajua Mheshimiwa Lema amekosea, tena sana katika hili.
Ninachofahamu mimi, hapo sio suala la heshima tu, ni zaidi ya hapo. Na ukweli Lema akifuata ushauri kama huu hawezi kuongoza wananchi wake kwa mafanikio, Gambo ameletwa Arusha kwa mkakati maalum, na yeye Gambo haamini katika heshima, anaamini katika uhuni! Mwacheni Lema, anajua anachokifanya!
 
Hii ni sawa na kichaa amekukuta unaoga akachukua nguo zako nawe ukatoka uchi wa mnyama kumfukuza huyo kichaa ili umnyang'anye nguo zako. Lazima wewe ndiye utaonekana ni kichaa. Kwa muungwana chuchumaa tafuta mbinu mbadala.

Mh Lema alichokifanya ni ujinga+ na hata wanaomuunga mkono fikra zao ni finyu+
Mfano wako hauingii katika mkakati unaofanywa na Gambo dhidi ya ubunge wa Lema, Gambo hata kama hana IQ lakini anatumika kumvuruga Lema kwa maslahi ya CCM, kumuunga mkono Lema haiwezi kuwa ni ufinyu wa mawazo, pengine kama unapenda kutumia lugha hiyo ungeigeuza kwa Gambo!
 
kama RC amefikia hatua yakuzuia muwakilishi wa wananchi asifanye majukumu yake ni hatari sana. kwa hali ilivyo inaonekana rais anafurahishwa na mnyukano huu wa viongozi hao hapo Arusha...
 
nadhani pale utatuzi haukufikiwa

Mara nyingi kwa kilichotokea kwa Lema, si kama nasupport direct alichofanya, huwa ni hatua ya mwisho ya uvumilivu, waweza iita point of no return.

And note that ukifikia katika point ya mwisho ya uvumilivu then uta-act as computer do, ukiletewa ujinga utadisplay ujinga uliyoletewa, its "Garbage in.....garbage out". You cant write matusi in your keyboard expecting computer display maneno ya hekima.

You will just be acting like a mirror, what stand in front of a mirror is what kitachoonekana katika mirror hiyo. And eventually, can say Gambo saw himself kupitia kwa Lema.

Ni mawazo yangu tu Mkuu.

Asante
 
Hii ni sawa na kichaa amekukuta unaoga akachukua nguo zako nawe ukatoka uchi wa mnyama kumfukuza huyo kichaa ili umnyang'anye nguo zako. Lazima wewe ndiye utaonekana ni kichaa. Kwa muungwana chuchumaa tafuta mbinu mbadala.

Mh Lema alichokifanya ni ujinga+ na hata wanaomuunga mkono fikra zao ni finyu+
sawa kabisa. ukimfukuza chizi ukiwa uchi we ndo unaonekana chizi
 
The Book said:
siwezi kutetea ujinga

Lema na Mkuu wa Mkoa wote wana makosa

Lema angejaribu kutumia busara sio ugomvi

Unaunga mkono wakati huko juu ulimnanga Lema peke yake
naunga mkono hoja ya msitari wa wa mwisho
 
Uongozi ni busara, hekima, uvumilivu, staha na maarifa.

Awali ya yote niseme tuu kuwa si lengo langu kujikita kwenye mzizi wa tatizo la ugomvi kati ya RC Gambo na Mh. Lema, hatahivyo, nachukua fursa hii kuongelea mtafaruku uliotokea juzi kwenye uzinduzi wa zahanati ya mama na mtot jijini Arusha.

Mengi yamesemwa ila kwa bahati mbaya naona shutuma nyingi zikielekezwa kwa RC Gambo. Kwa maoni yangu hata kama RC Gambo alikuwa ndio chanzo lakini Mh. Lema amekosea sana. Ngoja nifafanue;-

Jambo la kumpongeza mtu ni jambo la kiungwana tuu ila sio kitu cha lazima na sio kosa wala dhambi. Kwa jinsi nionavyo mimi, ugomvi ule wa juzi ulitokana na kitendo cha RC Gambo kutokumtambua Lema (kwa jina lake binafsi) kama mdau muhimu katika ufanikishaji wa mradi huo.

Pia kitendo cha RC Gambo kutoa historia isiyo sahihi (kwa mujibu wa Lema na wenzake).

Mosi, ni kwele kiongozi anaweza akakosea kutoa taarifa flani, hii inaweza ikawa kwa bahati mbaya au kwa makusudi. Inapotokea hali kama hiyo, nini unapaswa kufanya? Je, Lema alichukua njia sahihi na stahiki?

Pili, mchakato ule kwa nielewavyo mimi haukufanywa na Lema kama Lema bali ulifanywa na watu mbalimbali wakiwa kama taasisi, yaani Arusha Development Fund (ArDF).

Sasa ni kwanini Lema apige kelele kuwa amefanya kazi usiku na mchana na iweje asitambuliwe, yaani yeye kwa jina lake ilihali RC Gambo alishatambua mchango mkubwa wa ArDF kwenye mafanikio ya mradi? Lema ameonesha ubinafsi ama kwa lugha nyingine yeye ndio alikuwa anafanya siasa kwenye jambo lisilo la kisiasa.

Tatu, taifa limepata aibu na hali ile unauweka mradi kwenye wakati mbaya. SWALI; N i nani aliyesababisha hali hiyo? N RC Gambo kwa kushindwa kumtambua Lema kwa jina lake binafsi au Mh. Lema aliyepaza sauti na kuleta taharuki kwa sababu jina lake halijatajwa.

Mimi naona Mh. Lema ndio alikosea kufanya vurugu zile mbele za wageni kwani kama ni kweli ana uchungu na watu wa Arusha angetulia kwani shughuli ilikuwa inaenda vizuri halafu baadae akatengeneza mazingira ya kuongea ukweli.

Kupayuka na kupiga kelele mbele za wageni ambae kwa mujibu wa Lema wanaujua ukweli kuwa yeye ndio aliwatafuta kulikuwa hakuna maana yoyote bali ni kulidhalilisha taifa na kujidhalilisha yeye binafsi.

Gambo angekataa kufungua hapo sawa ila kiongozi amekuja, amewashukuru wadau sasa yeye ilikuwaje apige kelele kama sio uhuni na utoto wa kutaka sifa rahisi?

Tatizo letu Watanzania tunalichukulia hili jambo kiushabiki CCM vs CDM. Kwa mtazamo huo tutafeli na mimi sasa simshangai tena Mh. Lema bali nawashangaa wale wanaounga mkono kitendo chake kiovu.
 
Umeongea fact.. hata kama lema hakutajwa pale.. ilimbidi atulie ili baadae aelezee hali hali halisi.. lkn kwa alichokifanya nachelea kusema waliomchagua wanapaswa kujitathmini upya kama zilikuwa akili zao au viroba...
 
Kwa jinsi yeyote ile, ulipata daraja la tano (5) kidato cha nne.
 
Mpuuzi kweli wewe. Mbona alimtambua mawalla?
 
hilo la upuuzi ni la kwako labda ufupi wa akili yako ndio umekufanya unione mm mpuuzi labda akili ingekuwa kidogo ungeona nikisema kumtambua mtu ni jambo la kiungwana ila sio lazima na si dhambi
 
Hivi ile kitu ilishafutika ukitaka kupewa uongozi unachunguzwa na taasisi flani huo utaratibu mzee wetu nyerere alikufa nao, tukio la arusha ni ndoto nchi yetu kupiga hatua ya maendeleo kwa viongozi aina ya ile Kaunda suti ya kidumu
 
Mzee Lowassa amejipambanua mbele ya macho ya watanzania na mataifa kuwa yeye ni bingwa na simba wa siasataka. Alionyesha namna mchezo wa siasa unavyopaswa kuchezwa, aliweza kutenganisha kati ya siasa na maisha yake mengine ya kawaida. Dunia imemuamini kuwa anaweza kudumisha amani sio tu ya Tanzania bali hata ya Africa na Dunia.

Halipuki wala kukurupuka kama alivyofanya Mh. Lema alipokwazwa na Mh. Gambo kule Arusha. Baadhi ya Viongozi wa UKAWA hawana subira kama Lowassa, wanataka leoleo na ikiwezekana sasa sasa mambo yote, hii nadhani haiwezekani kufanyika hivyo hasa pale unapotaka kupambana na mtu mwenye dola na nyenzo zote muhimu zinazomsapoti yeye.

UKAWA wamepoteza fursa ya kupata katiba mpya yenye nafuu kuliko hii ya sasa anayoitumia Rais Magufuli na Mh. Gambo. Wangekubali kwanza (kwa muda) katiba pendekezwa ya JK, kisha kuikarabati na kuviondoa vifungu vyenye ukakasi punde watakapokuwa madarakani. Lakini looo!!!, hawa jamaa wanataka "either whole or none" leo leo na sasa sasa. Leo leo waingie Ikulu, leo leo serikali tatu, leo leo muungano wa mkataba, na sasa sasa wapambane na Gambo akiwa bado hajashuka jukwaani. Hata Nyerere (rip) aliupata uhuru na Urais kidogokidogo kwa kuanzia na uwaziri mkuu. Hata alipoingia Ikulu hakuanza na katiba mpya na kila kitu kipya na cha kwake. Katiba yetu hii ya sasa inamruhusu Gambo kufanya kile alichokifanya kwa Lema, katiba waliyoikataa UKAWA nina imani kuwa ingekuwa na ahuweni kuliko hii ya Gambo. Hakika watamkumbuka JK tena na tena.

UKAWA msichokozeke hata pale mnapochokozwa ili watu waione tofauti ya mchokozaji na mchokozwaji, kwani vyote hivi havifanyikii chumbani vinafanyikia hadharani mbele ya macho ya kitaifa na kimataifa. Onyesheni kama mko tayari kuichukua dola.
 
hilo la upuuzi ni la kwako labda ufupi wa akili yako ndio umekufanya unione mm mpuuzi labda akili ingekuwa kidogo ungeona nikisema kumtambua mtu ni jambo la kiungwana ila sio lazima na si dhambi
Haiondoi wewe kuwa mpuuzi. Unaangalia unapoangukia badala ya kisiki ulichojikwaa.
 
Back
Top Bottom