Ushauri wa Zitto kwa Lema na RC Gambo

Ushauri wa Zitto kwa Lema na RC Gambo

Wewe comte mbona unaharibu jina,huyu comte alikuwa mmoja kati ya wanafalsafa wakubwa,ana nasharia nyingi za kufikirisha.Mbona hulitendei haki hilo jina?

Unamjua Yesu Vizuri wewe au unakisia tu,hataYesu mwenyewe kabla ya kuachana na wanafunzi wake alitaka "Recognition".Yesu alitaka kujua je hata wale walio karibu yake wanajua yeye ni nani na mchango wake ni upi?Ndio maana aliwauliza wale wanafunzi wake "Eti mimi ni nani na watu wanasema mimi ni nani?

Wale wanafunzi wake wengine wakasema aaaa wewe wanasema Nabii Elia,mara Musa mara ooo!!Yesu akamuuliza Petro...Petro mimi ni nani?Pale pale Petro akasema,wewe ni Yesu Kristo mwana wa Mungu aliye juu...Hata kabla hajamaliza,pale pale Yesu akampa Petro "shavu"...Kwamba wewe ndio Peteo (Kefa) na juu ya mwamba huu nitalijenga kanisa,utakalolifunga duniani na mbinguni litafungwa.....Yaani baada ya "Recognition" tu,Yesu akampa shavu Petro...
SASA HAPA YESU NANI- GAMBO ALIYETUMWA NA MAGUFULI (MUNGU) AU LEMA MWAKILISHI WA MAFALISAYO?
 
Mzee Lowassa amejipambanua mbele ya macho ya watanzania na mataifa kuwa yeye ni bingwa na simba wa siasataka. Alionyesha namna mchezo wa siasa unavyopaswa kuchezwa, aliweza kutenganisha kati ya siasa na maisha yake mengine ya kawaida. Dunia imemuamini kuwa anaweza kudumisha amani sio tu ya Tanzania bali hata ya Africa na Dunia.

Halipuki wala kukurupuka kama alivyofanya Mh. Lema alipokwazwa na Mh. Gambo kule Arusha. Baadhi ya Viongozi wa UKAWA hawana subira kama Lowassa, wanataka leoleo na ikiwezekana sasa sasa mambo yote, hii nadhani haiwezekani kufanyika hivyo hasa pale unapotaka kupambana na mtu mwenye dola na nyenzo zote muhimu zinazomsapoti yeye.

UKAWA wamepoteza fursa ya kupata katiba mpya yenye nafuu kuliko hii ya sasa anayoitumia Rais Magufuli na Mh. Gambo. Wangekubali kwanza (kwa muda) katiba pendekezwa ya JK, kisha kuikarabati na kuviondoa vifungu vyenye ukakasi punde watakapokuwa madarakani. Lakini looo!!!, hawa jamaa wanataka "either whole or none" leo leo na sasa sasa. Leo leo waingie Ikulu, leo leo serikali tatu, leo leo muungano wa mkataba, na sasa sasa wapambane na Gambo akiwa bado hajashuka jukwaani. Hata Nyerere (rip) aliupata uhuru kidogokidogo kwa kuanzia na uwaziri mkuu. Hata alipoingia Ikulu hakuanza na katiba mpya na kila kitu kipya na cha kwake. Katiba yetu hii ya sasa inamruhusu Gambo kufanya kile alichokifanya kwa Lema, katiba waliyoikataa UKAWA nina imani kuwa ingekuwa na ahuweni kuliko hii ya Gambo.

UKAWA msichokozeke hata pale mnapochokozwa ili watu waione tofauti ya mchokozaji na mchokozwaji kwa vyote hivi havifanyiki chumbani vinafanyika hadharani mbele ya macho ya kitaifa na kimataifa. Onyesheni kama mko tayari kuichukua dola.
KAKA NYERERE ALIKUBALI HATA UCHAGUZI WA KURA TATU- WAMBIE PAPARA HAZINA TIJA NI SIFA YA UWANAHARAKATI
 
KAKA NYERERE ALIKUBALI HATA UCHAGUZI WA KURA TATU- WAMBIE PAPARA HAZINA TIJA NI SIFA YA UWANAHARAKATI
Kama Nyerere angewaambia wakoloni kuwa kama tukipata uhuru atataifisha mashamba yote na mali zote za wazungu na wahindi na kuwa mali za umma wazungu wasingekubali kumpa Ikulu kama alivyofanya Jecha. Hawa jamaa walionyesha wazi wazi mchana kweupe kama wangeshinda uchaguzi wangevunja muungano badala ya kuufanya uwe imara, nani angekubali ujinga kama huo. Ama hawana plan, hawafai au wanawazuga tu wale wanaopenda mabadiliko.
 
Well said.
Ni dhahiri shahiri huu ugomvi wa Mbunge Lema na RC Gambo unaelekea kubaya. Wakti wowote tunaweza kushuhudia kilichotokea Mwanza hivi karibuni kati ya RC na RAS kurushiana chupa za maji kwenye kikao! RC Gambo anaonekana hana maadili na hikima za kuongoza watu! Sijui hata JPM alipomteua kuwa RC alitumia vigezo gani!!

Mimi nimshauri Rais Magufuli kama anataka kazi zifanyike kwa ajili ya Maendeleo ya Arusha na Tanzania kwa ujumla,afanye 1 kati ya mambo 2. Moja, ni wakti wa kumtumbua na kutengua u-RC wa GAMBO. Kama hilo haliwezekani kwa maana kwamba Gambo bado ni lulu kwa Serikali ya CCM basi Gambo ahamishiwe Makao makuu ya TAMISEMI au IKULU na awekwe ofisi ambako hawezi kuwa anakutana na watu kila siku kama RC!

JPM amekuwa akijinasibu kuwa MAENDELEO HAYANA VYAMA, sasa kama Mkuu wa mkoa anataka kuzuia maendeleo ya kujengwa Hospitali tena ya kuhudumia kina Mama na Watoto hafai kuwa Kiongozi hata kidogo!!
Kwa kukusaidia tu Amewekwa hapo ili afanye anayoyafanya sasa.Husitegemee uteuzi wake kutenguliwa.Inaonekana huyo ndo waliyemuona anafaa pengine kulikomboa jimbo.
 
Kwa kukusaidia tu Amewekwa hapo ili afanye anayoyafanya sasa.Husitegemee uteuzi wake kutenguliwa.Inaonekana huyo ndo waliyemuona anafaa pengine kulikomboa jimbo.
Nadhani hapana, Rais Magufuli anaendelea kukomaa kwenye kiti cha urais, sidhani kama atataka mtu amharibie sifa yake ili watu wapoteze imani na serikali yake. ndiyo mana alimudu kumpa Bakheresa ardhi na kupeana mikono na Lowassa. Ilishayafahamu makosa yake, alishaufahamu umuhimu wa watanzania kuishi bila chuki na kukamiana, alishafahamu umuhimu wa wafanyabishara, alishafahamu pia umuhimu wa kuwasikiliza wapinzani hasa baada ya UKUTA. Gambo kwa vigezo vyote alipaswa kuiga alichokifanya Rais Magufuli ili kujiletea heshima kama mkuu wa mkoa na kuitafutia kura CCM mwaka 2020, lakini kuiepushia nchi aibu mbele ya wageni. Gambo alipaswa kujua kuwa Arusha iko chini ya CHADEMA na Lema ndiye chaguo lao, hivyo ugomvi na Lema ni ugomvi na CDM na ugomvi na wananchi wengi. Kufahamu hilo hakuhitaji elimu ya chuo kikuu. Atumbulie tu au boss amuonye asirudie.
 
Imefika wakati wazee wa Arusha wakae kwa pamoja na kuwaita watoto wao Gambo na lema.nakuodoa tafauti zao kwa manufaa ya wananchi wa Arusha na Tanzania kwa ujumla.
 
Waxee wa Arusha sio watu wa mchezomchezo.
Hawana time ya kuuza sura kama wale wa mkoa ule
 
Imefika wakati wazee wa Arusha wakae kwa pamoja na kuwaita watoto wao Gambo na lema.nakuodoa tafauti zao kwa manufaa ya wananchi wa Arusha na Tanzania kwa ujumla.

Mtoto akiwa anagombana na mzazi wake wazee hawamwiti mzazi humwita mtoto na kumkanya aache hiyo tabia.Gambo ni babaake Godbless Lema maana yeye ni mkuu wa mkoa wote wa Arusha wakati Godbless Lema ni mbunge wa kisehemu kidogo tu cha mkoa wa Arusha ambacho ni pale Arusha mjini tu.Wazee wamwite huyo mtoto kuwa we kitoto koma kugombana na babaako
 
Mtoto akiwa anagombana na mzazi wake wazee hawamwiti mzazi humwita mtoto na kumkanya aache hiyo tabia.Gambo ni babaake Godbless Lema maana yeye ni mkuu wa mkoa wote wa Arusha wakati Godbless Lema ni mbunge wa kisehemu kidogo tu cha mkoa wa Arusha ambacho ni pale Arusha mjini tu.Wazee wamwite huyo mtoto kuwa we kitoto koma kugombana na babaako
Hapo ndipo unapohitimisha ile hesabu ya mmoja kati ya wanne(1:4)
 
Mkuu Zitto hivi unashushaje "munkari" kwa mtu aina ya Gambo?RC mwenye kisasi na fitina kila wakati??

Ni bahati mbaya watu wengi wanaliona hili tukio ktk "clip" ya vipande vipande.Bwana mdogo Gambo hakufanya uungwana toka mwanzo;alialikwa lkn hakutaka kuja kwa sharti la Lema kutokutakiwa kuwepo yeye atakapokuwapo.Hata alipofika mesa kuu;alitoa mkono kwa watu lkn akamruka Lema.Hii ilikuwa "indicator" tosha kuwa RC kaja kwa shari.Mkuu wakati mwingine mbwai mbwai tu...kama mtu ana madaraka na jeshi la kukuweka ndani,basi wewe uwe na ujasiri na uthubutu wa kuukemea uonevu;hata kama huwezi kumpiga mtu;basi hata mchukie na kumkaripia tu...hii ndio silaha iliyobaki lwa Lema.

Jitihada zikafanyika kwa kumpigia katibu mkuu kiongozi;akiwa kama sehemu ya mamlaka ya juu ya RC atumie nafasi yake kumshawishi mkuu wa mkoa kufika ili pawepo na uwakilishi wa kiserikali katika jambo la heri kama lile;baada ya kutakiwa na "watu wa juu" kufika bado Gambo alichelewa sana eneo la tukio;na hata alipofika aliamuru MC asimpe Lema nafasi ya kuongea na akataka yeye ndio aanze kuongea ili kuuwa protocol,na kwa sabb ya itifaki,angeongea yeye kulikuwa hakuna "room" tena ya Lema kuongea na upotoshaji ule ungemea kama mmea kandokando ya kijito.

Ili kuweka historia sawa,Lema ilibidi aseme palepale,maana hata hao wafadhili huyo Gambo hawamjui,mkataba uliingiwa na Lema wakati Gambo akiwa Korogwe akimtukana Mwanasheria wa Wilaya ya Korogwe kuwa ana degree ya chupi.Hao Maternity hawamjui Gambo kwa sbb wakati wanaleta ramani ya hospitali ya Mama na Mtoto pale Arusha,Gambo alikuwa kwenye kizimba cha Tume ya Maadili ya Utumishi wa Umma akijibu mashitaka yake ya kukiuka taratibu za utumishi wa Umma.

Ukiwa hujawahi kukaa katikati ya siasa za Upinzani Afrika utamuona Lema "Chizi".Lkn ule ndio upinzani wa Afrika,lazima uwe chizi,lazima ujifyatue kudeal na watu aina ya Gambo.Vijana wasio na rekodi yoyote ya maana ktk utumishi wa umma,unatia aibu kwa kuanza kuelezea historia ya ujenzi na umiliki wa kiwanja kwa maneno ya vijiweni badala ya documents.Ile ni aibu,aibu kwa aliyemteua na anayemuacha Gambo kwenye nafasi ile mpaka sasa.

Nina milion 6.5,nikipata laki tano naweza kufunguka zaidi,kwa sasa ngoja niishie hapa,Nitafungwa;lkn Gambo aache uhuni,asijipendekeze kijinga jinga;historia itamuhukumu.Hakuna Ukuu wa Mkoa wa kudumu.


Duh??? Bado ni mkuu wa mkoa kweli huyo Jamaa??

Ama kweli Ausha kuna vitimbwi.....!

Katoka Megesa Mulongo Akaingia aliyeonewa wa kigoma..... mara Gambo.
 
Ninachofahamu mimi, hapo sio suala la heshima tu, ni zaidi ya hapo. Na ukweli Lema akifuata ushauri kama huu hawezi kuongoza wananchi wake kwa mafanikio, Gambo ameletwa Arusha kwa mkakati maalum, na yeye Gambo haamini katika heshima, anaamini katika uhuni! Mwacheni Lema, anajua anachokifanya!

Ninaamini katika nililolishauri, ni juu ya Mhe. Lema kutafakari na kuchukua hatua, sina uhakika kama wafadhili wa Mhes. Lema walifurahia. Hata kama wangefurahia, sio njia bora nyakati zote.
 
Back
Top Bottom