Waisilamu nchini wamekuwa wakiilamu serikali kwamba imewaundia chombo ambacho ni BAKWATA, na kwamba hawakitaki kwa kuwa hakijaundwa na waisilamu. Waisilamu hao hao wanaitaka serikali iwaanzishie chombo kinachoitwa Mahakama ya Kadhi. Sasa hapa naona kuna ujinga fulani. Unalalamika serikali kuwaingilia kwa kuanzisha BAKWATA, halafu unalalamika kwa nini serikali haiwaingilii kwa kuwaanzishia Kadhi. Waisilamu wawe wazi basi, wanapenda kuingiliwa au kutoingiliwa na serikali?
My take:
Kwa kuwa waisilamu wameshalalamika sana kwa suala la 'kuundiwa BAKWATA', naishauri serikali isijiingize kabisa kujaribu kuwasaidia tena, kwani watakuja kuilaumu tena na tena serikali kwa kuwaingilia. Waisilamu wajipange, waanzishe Mahakama ya Kadhi, waiendeshe wenyewe, wahukumiane wenyewe na hata hukumu zikiwa mbaya, walaumiane wenyewe
Wewe wacha hoja za kijinga na ukifuu.
Bakwata ni taasisi ya iliyo undwa kwa kiasi kikubwa na Nyerere lengi ikiwa udhibiti wa waislam wasipinge sera zake la kulinufasisha kanisa kama alivo liahidi.hata baada ya kuondoka yeye
Bakwata ni sawa na tawi la ccm limekuwa likichaguliwa viongozi kwa kuwekwa hata watu wasio soma mfano wa mufti wa sasa.
Hili waislam wamesha achana nalo na bakwata imebaki kutangaza siku ya eid kwa vile inakua holiday otherwise haina impact yoyote na kila muislam anaejijua ameachana nayo.
Tuje kwenye mahakama ya Kadhi.
Hii ni mahakama ya sheria.
Kama mahakama nyengine mfano mahakama ya chini ya juu yaani high court au mahakama ya appeal.
Pia ni sawa na mahakama ya kazi au mahakama ya watoto au mahakama ya biashara au mahakama ya ardhi.
Hizi zote ni mahakama lengo likiwa ni kuendesha mashtaka madai na kutoa hukumu kwa mujibu wa sheria zinazohusika.
Na serikali imezigawa court hizi ili kuleta ufanisi zaidi.
Mahakama ya kadhi nayo ni mahakama ya sheria itakayo simamia haki na sheria inazohusu ndoa na mirathi ya waislam.
Waislam wana utaratibu wao katika mambo hayo.
Katika nchi yenye serikali halali yenye katiba mambo yote yanayohusu sheria huwa chini ya serikali yenyewe ndio msimamizi wao ndio dola.
Mahakama hizi zitaajiri wanasheria na majaji walo somea islamic law kwa viwango vitavo wekwa kama majaji wengine wa sasa hivi. Hapa bakwata hawaingii wala sio suala la kuwaundia waislamu kama ilivo kuwa bakwata.
Sheria siku zote husimamiwa na serikali na mahakama zake..na hio hufanya hukumu zitolewazo kuwa halali kwa zinakuwa kwa mujibu wa katiba ya nchi na katiba inazilinda.
Njee ya mfumo wa serikali hakuna mahakama .
Hapo nyuma mahakama hizi zikikuwapo na hazikuleta problem yoyote.chuki ya nyerere kwa waislam ndio akazifuta bila ya sababu za msingi.
Chuki ile ndio amewarithisha leo mkaona mkatae tu .
Inavo elekea nchi hii waislam wao wakubali ku sacrifice mambo mengi ili kuleta umoja na uwelewano.mfano nchi za kiislam zinapumzika alkhmis na ijumaa ili wapate muda wa kusali siku ya ijumaa.vile vile nchi za kikristo wao hupumzika jumamosi na na jumapili ili wasabato na wakatoliki wapate muda wa kwenda kanisani.
Tanzania sio nchi ya kikristo ila mkoloni alikua mkristo akatuwekea utaratibu huu kwa vile alikuwa jumapili anaenda kanisani. Utaratibu huu tukaurithi mpaka leo na waislam wameridhia kama njia ya kustahamiliana.pia
Serikali imekua ikiingia mikataba mingi kwa niaba ya kanisa pia imekua ikiziendesha tasisi zake zake kwa mabilion kila mwaka inawalipa madaktari wote katika hospital za kanisa na hospital hizo hazitoi huduma bure ila kwa malipo na ni ghali mno na waislam pia hilo wanaliona sawa ni katika kuvumiliana.
Leo kuendesha mahakama yenye mahakimu wasio zidi 50 kulipa mshahara hawa watu basi wakristo wana mind sana !! Ilhali hizi mahakama kimsungi ni za madai hivyo kuna malipo yakufungulia kesi na pia kwenye urithi sehemu ya mali hukatwa kama kodi kwa serikali.
Wakristo wanaonesha chuki tu kwa visababu vya uongo uongo ili jambo hili lisipite wao wanadhani ndio wanauzuia uislam usisambae tanzania.
Tunahitaji kustahamiliana kuleta utengano katika nchi.
Haya tuyowafanyia waislam kwa vile mumehodhi bunge sio la kujisifia nchi inaenda kidogo kidogo kwenye mawazo ya hili la waislam na hili la wakristo..nchi moja njia tofauti hatutofika popote zaidi ya kuchukiana ndani ya nchi moja