mazaga one

JF-Expert Member
Apr 16, 2015
2,463
3,932
Baada ya Mchakato wa Ajira kukamilika na Majina kutoka Sasa kumekuwa na lawama nyingi Sana kwenda Kwa Tamisemi.

Mimi nilikuwa na Ushauri Kama ufuatao....

1. Kuna ulazima Gani wa watu kwenda Kuripoti ilhali lawama zimekuwa nyingi na Watu wamekosa Imani kabisa na Serikali yetu ya CCM Kupitia Ajira hizi Mpya zilizotolewa.

2. Ni kwa nini kwenye Awamu ya kwanza mlishindwa Kuwachukua Walimu waliopo vituonii tayari ambao Walikuwa wanajitolea huko mashuleni na vyeti vyao wenye sifa hao Wakuu wa Shule wanavyo na Taarifa zao pia Mliomba kutoka mashuleni.

3. Kama mlishindwa kuajiri wanaojitolea, Kuna Wahitimu wengine Wapo Internship ya TAESA(Tanzania Employment Services Agency) ambao Hawa wapo chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu Kuna vijana wengi tu wapo internships kwenye mashule huku wakilipwa na Serikali ya CCM 150,000/= kwa Mwezi na kwa taarifa za Haraka wengi wao wapo Wamefanya tayari mwaka mmoja Kama mikataba yao Ilivyo.

Ila kwenye Ajira hizi za Tamisemi pia hawajakumbukwa ilhali waliomba pia.Sasa Serikali yangu pendwa mtalikwepaje Hili jinamizi la lawama la nyie kulaumiwa kuajiri Walimu Hewa au feki kwenye orodha ya majina hayo mliyoyatoa ilhali.

✔️Tayari Kuna Watu walikuwepo mashuleni na bado majina yao kwenye Ajira Mpya hawapo?
✔️Haya Basi tuseme Waliokuwa wanajitolea list ya kuja Kwenu ilikuwa feki,Je hao waliopo kwenye internship ya TAESA zaidi ya

Mwaka na vyeti vyao TAESA walikagua na kujiridhisha lakini bado masikini ya Mungu Vijana wapo tu Mtaani na wengine internship imeisha na Ajira hizo waliomba Ila Hawamo...Ukiangalia hili Ni Jambo ambalo kwenye Ilani ya CCM lipo kabisa kwamba mtawapa mafunzo ya kazini wahitimu Ili waweze kuajirika, lakini la hasha hao Vijana wa Internship mmewalipa Karibu Million 1.8 kwa kila Interns kwa mwaka mzima huku wengine wakiwa shule za Serikali ambapo walisaidia Sana hata kwenye ufaulu wa matokeo ya Mitihani ya Taifa na wengine wachache wakiwa shule binafsi pia Ila mmekuja kuwatosa kwenye Ajira Sasa Serikali yangu ya CCM Kuna umuhimu Gani wa Kuwapa watu Internship na kuwalipa hela ilhali kwenye Ajira ambazo nyie wenyewe mnazitoa mnashindwa kuwaajiri???
Ki ukweli maswala ya Lawama na kila kitu TAMISEMI nyie wenyewe mmeyataka.

Lawama ni Nyingi Machozi na Majonzi ni Mengi Vilio Stress zimetawala kwa Vijana,Wengi wao wanaongea Maneno yakusikitisha Sana Huku Mimi mwenyewe Kama Kada wa CCM nikiyasikia kwa kinywa changu.


Nimeamua kuleta huo Ushauri wangu wa Bure.

Mungu Ibariki Tanzania!
Mungu tubariki Vijana Wote nchini Tusio Jua Kesho yetu ni Ipi.!
Mungu Mbariki Rais wetu JPM.!
Mungu wabariki wote wenye Nia Njema na Vijana Tusio na Ajira.!
Mungu naomba Uwape Moyo wa Huruma wa kutusaidia sisi Vijana wale wote wenye dhamana nasi Watanzania!


Mazaga One
Job Seeker
 
Msijali, kwa sasa bunge limejaa kijani, wale wanaokwamisha maendeleo hawapo. Budget zitapita wangu wangu na ajira bwerere zinapatikana. Kidumu chama cha mapinduzi...
😭😭😭😭😭😭😭😭
 
Msijali, kwa sasa bunge limejaa kijani, wale wanaokwamisha maendeleo hawapo. Budget zitapita wangu wangu na ajira bwerere zinapatikana. Kidumu chama cha mapinduzi...
Na watumishi watapata stahiki zao za malimbikizo,salary ongezeko, n.k.


5 tena!
 
Back
Top Bottom