Ushauri: Ukiwa chini ya ulinzi wa polisi jitahidi kupunguza dharau, fuata maelekezo yote. Utakuja uuliwe uwaachie msiba ndugu zako

Tangu awamu ya 4 ya Mh. Kikwete polisi Tanzania wana stress sana . Sababu kubwa ni kuachwa gape kubwa la kimaslahi na askari na maofisa wa JWTZ. Posho na mishahara ya hawa watumishi ziko mbalimbali.

Kwakuwa jeshi ni utii polisi wetu wamekuwa watii kwa serikali lakini hasira zao zinaishia kwa wananchi.

Na hiki kikokotoo kimewagaragaza mapolisi na kuwaacha wanajeshi.

Wanasema inamaana kama kikokotoo ni kizuri kwanini hayo mema wasipelekewe pia maaskari na maofisa wa jwtz?

Ukiwa chini ya ulinzi wa polisi nakuomba acha ujuaji, utakufa.

Mimi sio polisi wala sina ndugu wa damu ambaye ni afisa au askari wa jeshi la polisi. Nawapa tu ushauri.
Kweli mkuu kikokotoo kwao ni Janga kubwa sana, yani utakuta kamanda wa polis wa mkoa ana lipwa kiinua mgongo shilingi million 20 wakati mwenzake wa Jwtz ana lipwa million 180.

Sent from my SCV48 using JamiiForums mobile app
 
Miaka ya 1980's Arusha waliwakata vijana sita wakiwa na bunduki moja siku ya pili maiti zao zilianikwa mbele ya kituo Kikuu cha jijini.
Walikamatwa wakiwa hai na hapakuwepo mapigano.
 
Nafikiri iangaliwe na weledi na maadili ya askari pia.

Hapa unazungumzia mtu anayeweza kukutafutia kosa ili umuhonge elfu mbili au kwa kushirikiana wanaua mfanyabiashara ili wagawane pesa.

Kama maslahi wengine hatujaajiriwa kabisa
 
Tangu awamu ya 4 ya Mh. Kikwete polisi Tanzania wana stress sana . Sababu kubwa ni kuachwa gape kubwa la kimaslahi na askari na maofisa wa JWTZ. Posho na mishahara ya hawa watumishi ziko mbalimbali.

Kwakuwa jeshi ni utii polisi wetu wamekuwa watii kwa serikali lakini hasira zao zinaishia kwa wananchi.

Na hiki kikokotoo kimewagaragaza mapolisi na kuwaacha wanajeshi.

Wanasema inamaana kama kikokotoo ni kizuri kwanini hayo mema wasipelekewe pia maaskari na maofisa wa jwtz?

Ukiwa chini ya ulinzi wa polisi nakuomba acha ujuaji, utakufa.

Mimi sio polisi wala sina ndugu wa damu ambaye ni afisa au askari wa jeshi la polisi. Nawapa tu ushauri.
Hata hivyo ni busara kuheshimu kazi za wengine haijalishi ni Polisi au shoe shiner.
 
Moral of the story ni divide and rule.

Hii njia walitumiaga wakina nani Wafaransa au Wabelgiji? Wazee wa history nikumbusheni tafadhali
Divide and rule walikuwa ni Waingereza,,,Wafaransa wao ilikuwa assimilation policy.....kutengeneza watawaliwa na wao kujiona ni Wafaransa...
 
Tangu awamu ya 4 ya Mh. Kikwete polisi Tanzania wana stress sana . Sababu kubwa ni kuachwa gape kubwa la kimaslahi na askari na maofisa wa JWTZ. Posho na mishahara ya hawa watumishi ziko mbalimbali.
Jeshi (JWTZ) na Polisi ni vitu viwili tofauti kabisaa.....Ni Wizara mbili tofauti kabisa ...

usifananishe wala Polisi wasijifananishe na Jeshi ..
 
Kwahiyo mnatuambia sisi Watanzania Askari wetu huwa wanaua watu wasio tii amri zao?

• Mwenye Kisa na akiweke hapa.

Ama, mnatuambia Askari wetu wana stress?

• Mwenye aliyefanya tafiti aweke hapa.

Hatahivyo ndio mnasema kuwa maaskari huwa wanaua Raia ambao huwa hawatii amri?

Askari wanaoua Raia katika nchi za nje nao wana stress?

Je, raia wanao uliwa na polisi huwa hawatii amri?

Kwa mtazamai wangu haya masuala ni ya kuokota, na mara nyingi huwa yanayotokea nje ya nchi yetu zaidi, na, yanavyo tokea nchini mwetu.

Ni kuchonganisha Polisi
 
Back
Top Bottom