Ushauri: Tiba ya kikohozi na mafua

Ushauri: Tiba ya kikohozi na mafua

Sikiliza!.

Dawa alizokupa Mzizi Mkavu tumia wakati shida imekukabili kwa sasa. Baada ya hapo jizuie na kunywa vitu baridi sana hata kama una kiu kiasi gani. Inawezekana tatizo lako si mafua hasa bali aina fulani ya pumu. Kwa kunywa vitu baridi sana hupelekea kusinyaa kwa mishipa ya kupitishia damu na hewa hivyo kukufanya ujihisi vibaya katika kupumua.

Vitu vyengine ambavyo upunguze matumizi yake ni vitu vikali kama vile machungwa na maembe ambayo hayajapevuka,pili pili n.k. Hivi unapokula vinapelekea kupata mate mazito na pindi umekunywa vitu baridi koo lako linakuwa halina uwezo wa kuyasukuma hivyo unajihisi kusongwa na hicho unachokiita ni mafua.
 
Hebu jaribu hii: chukuwa jivu laini ujazo wa kizibo cha soda, kisha wakati utakapojiandaa kwa ajili ya kulala. Utaitumia kama vile wafanyavyo drug users kwa matundu yako yote ya pua.

Baada ya hapo, utapiga sana chafya mfululizo na baadae itatulia na hatimaye, ukilala ukiamka asubuhi utakuwa huna mafua tena. Inaweza kukuchukua takribani mwaka mmoja au zaidi kutokuumwa mafua. It is the best way, try and you 'll see.
 
Helo JF,
Imekuwa ni kawaida kila unapofika msimu huu wa mwezi March, April sehemu kubwa ya watu tunakumbwa na mafua na kikohozi, maana hapa nilipo pua zinapokezana kuziba nikienda kulala ndio kabisa pua moja inaziba kabisa kutokana na mafua na wakati mwingine kikohozi, bila kusahau kupiga chafya mara kwa mara nikafikiri ni peke yangu kumbe karibu kila mtu analalamika mafua, mafua mara kikohozi.

Swali kwa madokta wa JF,
Je, kikohozi na mafua vinasababishwa na nini? na kwanini hutokea zaidi msimu huu? Mimi niliwahi kusikia kuwa msimu huu mazao mbalimbali kama vile mahindi n.k, hutoa mbelewele ambazo hupukutisha ungaunga fulani hivi na inadaiwa ndio unaosababisha kuharibu mfumo wa hewa wa mwili na hatimaye kuleta mafua na vikohozi, je hili nalo lina ukweli ndani yake.

Na je, dawa yake baada ya kukumbwa na mafua haya ni ipi inafaa zaidi? Je ni Goodmorning, Cofta, Komflyin n.k. au kuna dawa nzuri zaidi?

Nawasilisha! na pia nawatakia Kwaresma njema!
 
Jamani, nisaidieni. Nina mafua yasiyopona kwa miaka kumi sasa, pia na chafya mara kwa mara mpaka nadhoofika kila nikipewa dawa hazisaidii.

Msaada wenu wakuu wa JF.
 
Anza kucheki mazingira yako. Vumbi sana? Sabuni unayotumia?n.k.
 
utakuwa na alregy.nenda kapime ujue ni alregy ya nini . inaweza kuwa ya vumbi .perfime. moshi. harufu .maganda ya machungwa.na hata vyakula ilinisumbua sana wakati niko mdogo nikatumia dawa za kihindi nikapata nafuu ila duka lenyewe limefungwa kitambo wapo watu wengine lilikuwa dar clock tower maeneo ya posta linaitwa tropicana
 
do this usikalie viti vya sofa, usilalie shuka yyte bila kupasi, usile korosho wala karanga. usitumie zulia ndani usivae nguo za sufu, usiwe na petties ndani kwako. usitumie blanket lisilokuwa na foronya usilalie mtu usiokuwa na foronya. anika matandiko kwenye jua atleast once after every 2 wks. usirudie shuka hata kidogo. hakikisha chumban kako hakuna tandabui, pako well ventilated na pasafishwe kwa kitambaa chenye maji.

usitumie deodorant, wala perfumed soaps. kama unafanya kazi viwandani ni pm
 
Ninajaribu kufikiria mwanakijiji mwenye mafua chronic atafanyaje na masharti haya au tu niseme mwananchi wa kawaida wa Kikwete. Nahisi wengi wanayafanya kuwa sehemu ya maisha yao.
 
Anza kucheki mazingira yako. Vumbi sana? Sabuni unayotumia?n.k.

Pia kama ni mtumiaji sana wa perfume...kuna wengine huwa wanaathirika na perfume na hivyo kusumbuliwa na mafua kwa muda mrefu.
 
Pole sana.watakupa ushauri wa kuacha hiki mara kile lakini haikusaidii.mie nilikuwa na tatizo hilo we acha toka naanza kujitambua adi leo hii nina mtu mzima.Na tambua unapokuwa na mafua mdomo nao unatoa harufu pasipo wewe kujijua mana cell za pua zinakuwa zimekufa uwezi kujihisi.

Ilifika wakati nikawa hata kupumua siwezi.hali mbaya sana.nikajipeleka mwenyewe mhimbili kitengo cha koo na pua.
Nikapewa nasonex hii imenisaidia yani sina cha kusema na vidonge ukitaka zaidi ni PM nikupe na maelekezo zaidi.
 
mbano Hakuna hapa cha Ku P.M. wala nini mkuu Kama unajuwa Dawa ya Mafua itowe hapahapa.

jaman nisaidien nina mafua yasiyopona kwa miaka kumi sasa .....pia na chafya mara kwa mara mpaka nadhoofika kila nikipewa dawa hazsaidii msaada wenu madaktar wa jf
dogodogo91 Pole sana kwa kuumwa na Mafua Mkuu dogodogo91 Hebu fuata ushauri wangu mimi MziziMkavu hauchimbwi Dawa.Tiba ya mafua makali

kunywa maji ya limau na glasi moja ya maji ya uvuguvugu yaliyochemshwa kijiko kimoja cha asali Tumia kwa mara mbili hadi mara tatu kwa siku kwa muda wa siku 7 Kisha unipe mimi FeedBack.
 
naumwa mafua mepesi yananisumbua sana nakunywa dawa za hospital ila naona zinanichelewesha naombeni mnisaidie dawa asilia ya kutibu mafua
 
Chemsha maji weka mchuz wa machungwa kwa wingi na sukari na itumie kama chai yako.na unywe maji mengi.
 
naumwa mafua mepesi yananisumbua sana nakunywa dawa za hospital ila naona zinanichelewesha naombeni mnisaidie dawa asilia ya kutibu mafua
@nkowowo Dawa ya Mafua:Meza tembe za kitunguu Saumu baada ya chakula pamoja na juisi ya kitunguu Saumu iliyochanganywa na juisi ya limau pamoja na kuvuta moshi wa kitunguu Saumu. tumia hiyo dawa kwa muda wa siku 3 au siku 7 kisha unipe feedback.
 
Lemon tea is the best. Unatengeneza chai (yenye tangawizi mbichi). Kamulia limao kidogo na weka sukari kiasi. Ikiwa na slices za limao ambalo halikumenywa, utapenda dawa kuliko msosi.
 
1) Machungwa kwa wingi sana.

2) Kata kata malimao pamoja na maganda yake, chembe chembe unazokata ziwe ndogo sana na unakula kama salad na chakula chochote cha chumvi.

3) Juice ya ubuyu kwa wingi.
 
Back
Top Bottom