CHADEMA ondoeni pembe mbili na RANGI nyekundu katika bendera yenu, mtafanikiwa

Rabbon

JF-Expert Member
Apr 16, 2022
15,155
22,655
Salaam, shalom,

Mheshimiwa Mnyika amewahi kuhojiwa na kusema kuwa, Mh Mbowe ndiye aliyeshauri RANGI nyekundu iongezwe katika RANGI za Bendera ya CHADEMA, kwamba RANGI nyekundu inaashiria Upendo.

Mara kadhaa, viongozi wa CHADEMA wamewahi kunukuliwa wakidai, RANGI nyekundu katika bendera Yao, ni kuwaenzi wanachama wote waliofariki katika harakati za kudai HAKI.

Tanzania, upande wa Zanzibar yamewahi kufanyika MAPINDUZI ya kumwondoa sultani Kwa mtutu wa bunduki, jiulizeni kwanini waasisi waligoma kuingiza RANGI hiyo katika bendera ya Taifa letu?

PEMBE MBILI KATIKA BENDERA YA CHADEMA.

Vidole viwili, yaani kidole Cha kwanza baada ya dole gumba na kidole kinachofuata kilicho kirefu kuliko vyote, vidole hivyo vinaashiria katika Ulimwengu wa Roho ushawishi, ndio maana chama Cha CHADEMA, HOJA zake Zina nguvu sana na ushawishi Kwa wananchi, kinachokosekana ni utawala.

DOLE GUMBA ndicho kidole kinachohusika kuvipa nguvu vidole vyote,

Unapolima au kufanya shughuli yoyote, dole gumba ndilo huunganisha na kusababisha nguvu ya kufanya KAZI. Chama Cha MAPINDUZI CCM hutumika dole gumba kujitambulisha, wao hawahangaiki na HOJA, huhangaika na utawala, kushika Dola basi.

USHAURI:

1. Tumieni alama ya ngumi ✊ambayo mmekuwa mkiitumia msalimiapo Kwa kusema Pepoooooooz!! Alama hiyo ya ngumi iingizwe kwenye bendera Badala ya alama ya pembe mbili au ✌️.

2. Ondoeni RANGI nyekundu kwenye bendera yenu, rudisheni bendera iliyokuwepo awali.

3. Hakikisheni mnakuwa karibu na familia za wote waliopoteza maisha katika harakati, mf Chacha wangewe, Alphonce Mawazo na wengineo maana Damu Yao Bado inasema ila haisikiki.

Hakikisheni pia mawazo na sauti ya TUNDU lisuu inasikilizwa vikaoni Kwakuwa Damu yake ilimtoka ingawa hakupoteza uhai katika uanaharakati kupigania HAKI.

4. Viongozi jiepusheni kuvaa makaniki au kushika mikuki mnapofika katika miji mbalimbali, Jitahidini kusimama na Mungu pekee, msichanganye Mungu na miungu na Ibada za sanamu. Ibada za sanamu, uchawi wa moto utembezwao nchini kote, ni mojawapo ya vitu vinavyofunga fikra za Watanzania.

5. Viongozi epukeni kufanya matambiko, viongozi wachaga, epuka Mila za kumwaga Damu ya wanyama kama Ibada za matambiko, asema BWANA Mungu.

Huu ni ushauri tu.

Mungu ibariki Nchi yangu nzuri niipendayo TANZANIA 🇹🇿

Mungu ibariki CHADEMA.

Karibuni 🙏
 
Mkuu huu ushauri wako unaamini una maana yoyote? Kwahiyo simba ili ichukue makombe inabidi iachane na rangi nyekundu?
Uliwahi kuona bendera ya CHADEMA ya 1995?

Iweke hapa tuone Ina upungufu Gani?
 
Uliwahi kuona bendera ya CHADEMA ya 1995?

Iweke hapa tuone Ina upung kwufu Gani?
Narudia tena, Ili Simba iwe inashinda inabidi iweke rangi nyeupe? Mkuu utanisamehe kama nitakukwaza, kwa asilimia kubwa inaonekana umeathiriwa na imani za kishirikina. Fanyia kazi eneo hilo utanishukuru.
 
Nimewashauri viongozi waache kuvaa kaniki na kushika mikuki ya kimila.

Mungu hataki kuchanganywa na miungu.

Mwisho wa siku ushauri ni ushauri, maamuzi yabaki Kwa mshauriwa!!
 
Narudia tena, Ili Simba iwe inashinda inabidi iweke rangi nyeupe? Mkuu utanisamehe kama nitakukwaza, kwa asilimia kubwa inaonekana umeathiriwa na imani za kishirikina. Fanyia kazi eneo hilo utanishukuru.
Argue zako ni duni sana katika angle hii.
 
Argue zako ni duni sana katika angle hii.
Ni kweli mkuu, kwenye ushirikina sipo maana maana sijazaliwa na kukulia huko vijijini kwenye imani za ushirikina. Ndio maana sioni hatari ya rangi hasa hiyo nyekundu maana simba sports pia wanatumia rangi hiyo, na bado ina mashabiki kibao, na mafanikio tele.
 
Basi sawa.
 
✌ humaanisha V-Victor ushindi.

Rangi nyekundu -humaanisha uhai wa kuishi kwa mnyama au MTU.
 
✌ humaanisha V-Victor ushindi.

Rangi nyekundu -humaanisha uhai wa kuishi kwa mnyama au MTU.
Hiyo RANGI vijijini wanatafsiri kuwa ni chama kinachopenda vurugu. Na Iko hivyo Kwa watu aged.

Bendera ya zamani ilikuwa poa sana.

PEMBE Mbili hizo nazo Si nzuri, alama ya ngumi ni njema zaidi kimkakati, inaashiria UMOJA.
 
Nawashauri waweke matunguli na hirizi mana bila hvy Ikulu watakuwa wanaisikia kwa tv
 
Back
Top Bottom