Ushauri: Nijenge nyumba kubwa kwa muda mrefu au nijenge ndogo uani, kiwanja 20:30

Kiremba

Member
Apr 23, 2020
10
31
naombeni ushauri wenu ndugu, ninakiwanja cha 20:30 square meter, uwezo wa kujenga nyumba kubwa kwa haraka sina na maisha ya kupanga siyapendi, je mnanishauri nini? nijenge ndogo tu kwa nyuma kwanza nihamie au nivumilie nijenge kubwa ingawa itanichukua muda mrefu kutokana na hali ya kipato, na je kiwanja hicho nilichosema kitatosha?
 
based na kiwanja ulichonacho, unaposema kubwa au ndogo unamaanisha ukubwa gani na udogo gani!

binafsi, napendelea kuishi nyumba kubwa sana, so priority yangu ni nyumba kubwa hata kama sina hela, najenga tarartibu
 
Umeoa? Unafamilia? Kama unafamilia nadhan mdogo itakua ngumu ila kama huna au uko na mke tu( na- assume ww ni me) jenga ndogo kwanza
 
Wewe ndiye unaeijua hali yako namna ilivyo.
Itakua kheri, iwapo utafanya maamuzi kulingana na hali yako namna ilivyo. Umekiri kwamba, maisha ya kupanga huyapendi, na wakati huo huo unataka nyumba kubwa lakini itakuchukua muda kuikamilisha. Huna budi kujenga inayoendana na budget yako kisha baadae utakapokua sawa, ujenge kubwa.

Kumbuka, hata m'buyu ulianza kama mchicha.
 
based na kiwanja ulichonacho, unaposema kubwa au ndogo unamaanisha ukubwa gani na udogo gani!

binafsi, napendelea kuishi nyumba kubwa sana, so priority yangu ni nyumba kubwa hata kama sina hela, najenga tarartibu
naposema kubwa naamisha yenyevyumba kama vitu, living room, jiko na sehemu kama ya kusomea,
ninapomaanisha ndogo namaanisha labda chumba kimoja tu cha self na living room(sebure bas)
 
Jenga nyumba ndogo vyumba 2 na sebule weka ukubwa wa wastani mf chumba kiwe na ukubwa wa 12ftx10ft na sebule 12ftx12ft unaitenga pembeni kabisa kiasi hata kama ukijenga nyumba kubwa hiyo unaipangisha
 
Jenga nyumba ndogo uhamie mapema mkuu, ukihitaji ramani pamoja na muonekano wa nyumba zote mbili zikikamilika waweza Ni pm mkuu
 
naombeni ushauri wenu ndugu, ninakiwanja cha 20:30 square meter, uwezo wa kujenga nyumba kubwa kwa haraka sina na maisha ya kupanga siyapendi, je mnanishauri nini? nijenge ndogo tu kwa nyuma kwanza nihamie au nivumilie nijenge kubwa ingawa itanichukua muda mrefu kutokana na hali ya kipato, na je kiwanja hicho nilichosema kitatosha?
Kama umeanza majukumu ya kifamilia hasa ya kusomesha bora ujenge ndogo hiyo ila jua chance ya kuja kujenga kubwa itakuwa ndogo
Kama hujaanza majukumu jenga kubwa kwa kukadilia mda wa hadi unapoanza majukumu yako.Nimeona watu wengi walioanza na hizo mnazoita nyumba za uani hadi leo wako hivyo hivyo wamekosa pesa za kujenga nyumba za ndoto zao au wamefariki.Binafsi nimeanza hiyo nyumba kubwa mdogo mdogo but within 5 years nikianza majukumu ya kusomesha nitakuwa nimehamia finishing nitaendelea nayo mdogo mdogo
Tahadhari kama hujui vipimo mtafute mtaalamu akushauri,fundi atakuingiza chaka uchukue ramani kubwa ambayo itakuumiza
 
Back
Top Bottom