Baadhi ya maudhi yasiyoepukika kwa mhamiaji au mpangaji mpya katika mtaa

Undava King

JF-Expert Member
Aug 11, 2017
3,181
5,321
Ebu tujaribu kuvi - vaa leo viatu vya mpangaji au mhamiaji mpya yeyote yule anayeamua kuishi mtaa fulani alikopata kiwanja na akaamua kuyaweka makazi yake hapo au kapata chumba na akaona ni vyema akipanga na kuishi hapo.

Kama tulivyo binadamu wote huwa tuna-expectations kubwa tunapoanza jambo fulani lakini mara zote reality huwa ni tofauti kabisa na kile tulichowazia kabla.

Hivyo basi nimeangazia baadhi ya maudhi madogo madogo ambayo kwa baadhi yetu yamekuwa na madhara ila hayawezi zungumziwa na jamii kwa kuwa ni sehemu ya maisha ya jamii:-

1. Kesi za mipaka na viwanja,
Kama kuna kesi ya kwanza utakayokumbana nayo katika mtaa wowote ule ulioamia hii ni moja wapo na wahusika wakuu ni aliyekuuzia, dalali, jirani au serikali. Kesi hizi zikianza ni majaliwa kuisha kwa mwisho mwema.

2. Kujikuta makazi yako jirani na msikiti au Bar, nadhani mnajua adha yake hivyo sitoelezea sana.

3. Kukaa nyumba moja au kuishi jirani na mlokole au muislamu mwenye mapepo au majini yaani ni full chafya, usiku hulali ni kelele za mizuka imepanda,mara nyimbo za kusifu na maombi,mara unajihisi yanapokemewa na wewe yatakuvagaa au umerushiwa na wewe mazaga yaani ni full kuishi ila moyoni huna amani.

4. Kung'ang'aniwa kimapenzi na jirani, mke wa mtu au single mother- hiki ni kisanga kwa vijana wanaoanza maisha ya ghetto au mume wa mtu upangajini ukishaonekana unakamwelekeo au kazi, mzee baba utang'ang'aniwa hata kama utaki na hauna stori nao ni visa kwa kwenda mbele utadhani una mkataba nao watazusha, watakuchukia, watakuchomesha kama haitoshi utologwa.

5. Majungu- kuna mitaa si wanaume au wanawake watu wanapepesa midomo ukiwa na moyo mdogo wa kuvumilia kusemwa unajikuta umeama siku inayofuata.

6. Nzengo- Ni jambo la faida kwa jamii kushirikiana kwenye maafa kama misiba lakini amini usiamini hii si hiari inavyoonekana kwa jicho la nje bali ni lazima ushiriki na shughuli ya kutoa kamchango hapa ni kitu kisicho koma daima, sasa leta ubishi usitoe kisa kipato hakiruhusu au uoni faida ndo utajua wananzengo ni akina nani misibani (case study-jijini mwanza)

7. Ushirikina- unaweza jikuta umeangukia kwenye mtaa wenye mambo ya kiswahili yaani uchawi kwa kwenda mbele, mara wamepita kwako wameokota nyayo, mwanao kaamka na chale mwilini, jioni nyau wote wameamia kwako na vilio vya vichanga mpaka usingizi unakata n.k

8. Miziki mpaka usiku, kama kuna kero nyingine basi ni hii ujikute una jirani asiyemstaarabu au unakaa jirani na ilipo senta au vijana wabani nyimbo, makanisa yenye mahubiri usiku kucha,kumbi muda wote ni miziki mpaka unajuta ulifata nini hapo

9. Kiwanja chako kugeuzwa njia ya miguu- unaweza kuwa ulipata site nzuri na ukajenga kweli ila ukaacha kanafasi aidha mbele au nyuma ya nyumba yako kwa ajili ya matumizi yako mwenyewe aidha kukaa, maegesho ya gari n.k lakini ghafla inageuzwa mdogomdogo kimatumizi watu wanaanza kukatisha hatimaye ni njia na ukiwakataza au kuifunga tambua kuwa una roho mbaya au utaitwa mbinafsi.

10. Kutakiwa ufagie barabara na uweke vifusi vya michanga, tena usiombe mtaani hapo uwe mmoja wapo wa wale wenye magari mchango wa magunia na wapakiaji unakuhusu wewe kabla ya wengine wote.

11. Michango isiyoisha, yaani kuna mitaa michango nikama laana kila baada ya muda wamefika, mara shule,mara za maendeleo ya mtaa, mara misiba, mara wagonjwa, zahanati n.k.

12. Vifo vingi visivyokoma kila baada ya muda haipiti wiki hujasikia tangazo la msiba mtaani kwako na idadi ya watu wengi wanaofariki ni katika eneo hilo hilo moja kila mara inakubidi kughahirisha shughuli za utafutaji kuhudhuria misiba kila uchao.

13. Biashara kufanyikia mbele au nyuma ya nyumba yako, imetokea ulipojenga ni jirani au katika eneo linalovutia watu wa mtaa kufanyia shughuli zao za kibiashara, hapo ukubali ukatae hakina mama watakuzingira na mbogamboga na matunda ujakaa sawa saluni na maduka yashakufata hauna budi kukubali kuwa utulivu ulioutarajia na mandhari ya nyumbani kwako lazima yabadilike tu.

14. Kuishi na watu unaowazidi kipato au hadhi kwenye nyumba ya kupanga, kama kuna kitu kinatesa ni pale watu wanapokuona wewe ni taita wao, hata wakikwepa majukumu yao kama malipo ya bili n.k unasubiriwa ni wewe waone utachukua hatua gani, Je utakubali walale gizani au utawanunulia umeme, achilia mbali utegemezi kwako kwa mambo mengi.

15. Kuishi mtaa ambao hauna genge au senta unapoweza fanya shopping ya mahitaji madogomadogo yaani mahitaji hadi mtaa wa pili, ikitokea njiti za kiberiti au umeishiwa chumvi ghafla ukiona uvivu kutembea bila shaka option nikulala na njaa.

16. Kuzingirwa na Makaburi, kuna wakati unajikuta unapoishi au ulipojenga ni jirani au pamefanywa hivi karibuni kuwa eneo la makaburi na hivyo haipitishi muda mrefu kabla ujaona kundi la watu na majeneza wanajongea kwako kuja kumpumzisha wapendwa wao.

17. Vibaka, walevi,wazurulaji na vijana wa vijiweni kujazana kila mahali ndani ya mtaa unaokaa- kwa mzazi au mlezi ambaye unategemea wanao wakike na wakiume wawe na malezi mema na future njema hii ni alarm kuwa hauko mahali sahihi.

18. Ulinzi shirikishi, kuna baadhi ya mitaa hii ni kero kubwa wakati mwingine unaweza lazimishwa na wewe upangwe kwenye zamu ya ulinzi hata kama ujaridhia, ukomo wa muda wa kutembea, kujielezea kila ukikamatwa ukiwa umekaa au unakatisha mtaa, kuhusishwa na wizi au upotevu hata kama uhusiki n.k

19. Kutokuwepo na huduma muhimu za kijamii karibu au mahali unapoishi mfano shule, zahanati, barabara, maji,umeme na miundombinu mingine.

20. Kuomba kuteka maji kwa jirani- unajikuta wakati mwingine pesa unayo ya kuvuta maji lakini kila ukienda mamlaka ni kuzungushwa tu, hivyo unaamua kushare bili na jirani uwe unateka maji kwake baadae jirani anakugeuza chuma ulete wewe ndo wakutoa bili kila mwezi yeye anaegeshea na chakumfanya huna maana akifunga bomba maji utatoa wapi.

21. Bili ya umeme na maji kwenye nyumba za kupanga, hapa kuna tizi unaweza ukawa ni wewe tu ndiye mtoaji na wengine wanazinda au kuna wasumbufu mpaka hela itoke basi na tarehe ya malipo imekwisha pita.

22. Kuwa na jirani omba omba- hakuna anayejenga mahali huku akitegemea atakutana na jirani wa namna hii ila inatokea unakutana na jirani asiyeishiwa matatizo ye muda mwingi ni kuomba na huwezi mkatalia kwa kuwa utavuruga uhusiano mwema baina yenu.

23. Majirani au watoto wa majirani kujenga mazoea ya kuja mara kwa mara kwako iwe ni kucheza, kupiga soga,kula au kuangalia TV mfano mpira, siku ukichoshwa na hii hali na ukataka uhuru kwa kuyakatisha mazoea hayo ndiyo utajua umeyakanyaga.

24. Mikopo, kuna mahali suala la watu kuja kukukopa wakiwa na sababu rundo wengine hadi machozi wanamwaga nikugusa tu tatizo malipo na kuna mahali hata kama umeishiwa vipi uoni wakumkopa na hata huko madukani ukitaka mkopo wa mchele pia ni tizi kila mtu ni mchumi a.k.a wasaga kunguni.

Haya ni baadhi tu naamini yapo mengi wanaojua mengine wachangie pia.
 
Hiyo namba 15 inanihusu kabisa, nikitaka kununua kibiriti tu nakifuata mbali huko, kuna siku nilikunywa juisi tu nikalala
 
1
Ujakutana tu na majanga mkuu, watu wanakupangia kafumanizi ka mchongo na mtoto wao aliyekosa mume na kachezea sana ujana wake, mtaa mzima unaamia mlangoni kwako, upende usipende unafungishwa ndoa ya mkeka.
14,22 na 24 n balaa kwny nyumba za kupanga
 
MZEE WANGU HACHANGIAGI MICHANGI TOKA ZAMANI

SIJUI HELA YA TAKA,ANAWAJIBU KUWA ANACHOMA TAKA ZAKE

HELA YA ULINZI ANAWAJIBU KUWA ANAJILINDA MWENYEWE

WAMEMSHINDWA MPKA LEO,NA MIMI NIKMALIZA UJENZI KWENY MJI WANGU SICHANGIII
 
MZEE WANGU HACHANGIAGI MICHANGI TOKA ZAMANI

SIJUI HELA YA TAKA,ANAWAJIBU KUWA ANACHOMA TAKA ZAKE

HELA YA ULINZI ANAWAJIBU KUWA ANAJILINDA MWENYEWE

WAMEMSHINDWA MPKA LEO,NA MIMI NIKMALIZA UJENZI KWENY MJI WANGU SICHANGIII

utakuja kubananishwa siku moja au kupigwa bonge la tukio na kamati ya roho mbaya usiamini
FB_IMG_16817165345427179.jpg
 
Kuna nyumba za kupanga ni changamoto wacha kabisa.
Ukute mwenye nyumba kimeo ana masharti usipime na hata kama huna haelewi, wapangaji vijicho na viswaswadu muda wote nikufuatiliana na majirani zenu hapo mtaani ni vimeo na umbea kwa kwenda mbele na kwa bahati mbaya mwenzangu kipato chako kiwe ni tia maji tia maji utakufa siku si zako.
 
Ukute mwenye nyumba kimeo ana masharti usipime na hata kama huna haelewi, wapangaji vijicho na viswaswadu muda wote nikufuatiliana na majirani zenu hapo mtaani ni vimeo na umbea kwa kwenda mbele na kwa bahati mbaya mwenzangu kipato chako kiwe ni tia maji tia maji utakufa siku si zako.
Ase mi nikikutaga ivo yani kodi ikiisha nikuhama hamna namna mtu umelipa hela yako bado huna uhuru
 
Duuuh, mwezi ujao itanilazimu kuishi upangajini ila nina hofu na walimwengu haswa....maana nina hasira za karibu...🤔🤔🤔🤔
 
Ase mi nikikutaga ivo yani kodi ikiisha nikuhama hamna namna mtu umelipa hela yako bado huna uhuru
Ukute nyumba yenyewe ni ya geti halafu umepangiwa na masharti ya muda na kwa bahati mbaya muhuni ujaoa halafu shughuli zako ni zakurudi usiku ndio utajua hujui.
 
Back
Top Bottom