NetMaster
JF-Expert Member
- Sep 12, 2022
- 1,454
- 4,853
huyu ni mama mdogo wangu na nipo karibu sana na mtoto wake ambae huwa ananiambia vitu vingi.
Ni kwamba mtoto wa mama mdogo alipokuwa mdogo akiwa na umri wa miaka 9 aliumwa malaria, hali yake ilikuwa mbaya sana ikabidi apigwe sindano za quinine (kwinini)
Hii dawa kama mtakumbuka hapo zamani kwa waliowahi kutumia hii dawa ilikuwa inaziba masikio kwa kiasi flani lakini kesho yake yanarudi, ila kwa wengine hasa wale wanaochoma sindano edapo kipimo kikizidi hii kwinini ishafanya wawe viziwi kabisa ama kuwa na usikivu hafifu unaozidi kufifia kadri miaka inavyoenda.
ndicho kilichomkuta mtoto wa mama mdogo, akiwa na miaka 9 ndio alipigwa hizo sindano, alipofika darasa la saba tukaanza kuona hasikii fresh, na hapo ndipo napowaletea mkasa wangu.
ni tangu kipindi hicho hadi sasa kwa miaka takribani 10 mama mdogo anaamini kijana wake kaaminishwa kwamba kijana wake karogwa na kapitia mengi sana akiwa kama mama na hili nami naujua uchungu wa mama lakini imefika steji kwamba na mimi nmeamini wanawake ni rahisi sana kudanganyika.
Hopitalini huko alishaambiwa chanzo walimpa dawa lakini hazikumsaidia - Muhimbili, Kcmc, nairobi, india, Uingereza
yeye mtoto kashakubali hali yake, wana vikundi vyao vya wenye tatizo hilo na ana shughuli zake lakini shughuli ipo kwa mama yake.
Wachungaji feki
Mama mdogo akisikia tu kuna mchungaji mkubwa kaja mkoa anaoishi anaenda kwa wachungaji kuwapa hela hizi laki 2 hadi laki 5 kwajili ya kumuombea mtoto wake,, nilikuwa siamini haya mambo lakini hapo mwaka jana tu kuna mchungaji maarufu kabisa alikuja huo mkoa, kuna maombi maalum ya mtu moja moja ndani ya hema ni shilingi laki 4 kwa mtu moja.
Wachungaji baadhi yao wanafanya mazingaombwe ya wazi wazi nae mama mdogo anaamini kirahisi, kuna mmoja alienda nyumbani kwao huwa inasemekana anatembea na kemikali flani anachovyakwenye vidole, akianza kukuosha sehemu yoyote ya mwili maji yanabadilika rangi yanakuwa ya zambarau, yani hapa mama mdogo akili zilimruka akiamini ni uchawi unatoka, mme wake alipoona hivyo akardi chumbani kumwambia hayo mazingaombwe lakini wapi.
Mashehe wanaopandisha majini
Hapa ilibidi wasafiri kabisa kwenda huko Tanga, huyo shehe ni mshirikina anapandisha majini anaanza kumshirikisha Mungu kwenye tabibu zake, niliambiwa kila ikifika jioni kuna kufushwa dawa, hii ilikuwa kwa wiki nzima,
Waganga wa kienyeji:
Hapa palishafanyika hadi tambiko kkupigia magoti mizimu ilhali ni watu hao hao wanaenda nyumba za ibada
...............................................................
MUHIMU: Kijana kaniomba wazo la biashara, nipeni mawazo yenu >> hapa <<