Kibosho1
JF-Expert Member
- Dec 12, 2017
- 2,491
- 3,998
Wachumba, Marafiki nawapa salaam kwenu.
Kwa wakristo nashauri tusome Luk 14:28 ili twende sawa. Kwa dini nyingine na wasiokuwa na dini twendeni na msamiati huu.
"Ukitaka cha uvunguni sharti uiname"
Nimehudhiria baadhi ya harusi nyingi sana hasa mwaka huu lakini mambo siyo ya kuridhisha kabisa.
Mambo yanaenda enda tu bila mipango kutokana na mambo sio powa kwa raia kwenye swala la kiuchumi changanya na covid-19 tena.
KASORO KASORO ZA KUKUMBUKWA
1. Unaenda kwenye harusi, ukumbi mzuri,mapambo mazuri lakini chakula kimeisha😬😬
2. Wanandoa wamependeza chakula cha kutosha,Bia zimeisha (kila mtu 1 tu)😔😔
3. Vinywaji vya kutosha,vyakula vyote mc& music vya kuunga unga🙄🙄
4. Maandalizi yote yako sawa lakini pesa ya Video shooting na picha haitoshi "atakopwa🙈"🤔🤔
Kukosekana kwa kimojawapo kati ya hivyo ni rahisi sana kuharibu shughuli yote na kukumbukwa na wahudhuriaji.
MASWALI YA KUJIULIZA KABLA YA MIPANGO
Bajeti yangu inatosha kufanya sherehe hii?
Jiangalie wewe kama wewe je nina shilingi ngapi?
Kama kuna michango je itanitosha?
Kama isipotosha nawezaje kufanikisha hii?
Kuboronga kwa shughuli nyingi kunatokana na mipango mibovu na tamaa ya waandaaji bila kuzingatia kiasi halisi kinachoweza kupatikana.
Kutokana na tamaa hiyo inapigwa bajeti kubwa na wakati vikao vikiendelea baadhi ya mahitaji yanaanza kutolewa malipo ya awali. Mpaka kufika kwa shughuli hela haijapatikana yote na malipo ya awali yaliyolipiwa hayawez kurudishwa. Nini kinachofuata? KASORO KASORO
NB. Sikupangii jinsi ya kuandaa shughuli yako lakini si lazma ifanane au izidi ya mtu fulani. Shughuli ikiharibika hakuna anajua wanakamati! Bwana na bibi harusi ndio mnajulikana kwa hiyo lawana mtapewa nyie.
Ni hayo tu