Ushauri wa bure kwa wanaotarajia kufunga ndoa

Nickson Swai

JF-Expert Member
Sep 5, 2018
548
475
Habari zenu natumaini wazima wa afya.

Najua wapo watu wapo kwenye mipango ya kufunga ndoa, mimi kitu ambacho nimekiona mambo ya kuzingatia kabla ya harusi;

1. Uwe na akiba yako binafsi kabla ya harusi, ili inapotokea bajeti imepungua mzee unajiongeza.

2. Wengi wanategemea michango ya watu, hili ndilo limetawala kwa wahusika yaani katika kitu ambacho watu wanafeli ni hapo, endapo wasipochanga kwa kiasi itakuyumbisha.

3. Usitegemee kamati ya watu mbalimbali.

4. Wengi wanataka kuonyesha ufahari wa matumizi ya pesa yanayozidi uwezo, mfano ukumbi wa milioni 5-10 kwa siku. Wanasahau sherehe ni siku moja na ndoa ni ya muda mrefu. Hivyo mkija kuachana daah, mbwembwe zote zinakwisha.

5. Fanya kitu ambacho uwezo wako unaendana nao.

Yangu ni hayo tu, ahsanteni.
 
Uko sahihi lakini baadhi ya makabila hayo uliyoandika hayana mashiko kabisa.....sijasema kabila gani Mr. Nickson Swai.
 
Uko sahihi lakini baadhi ya makabila hayo uliyoandika hayana mashiko kabisa.....sijasema kabila gani Mr. Nickson Swai.
Sijakataa mkuu ila kinachotugharimu watu wengi kutaka harusi ilihali anategemea michango ya watu wengi nimeliona limeleta shida ni hayo tu.
 
Hivi usipofanya harusi Ni kipi kinaongezeka au kupungua kwenye mahusiano au ndoa yako?

Hata mi nashangaa!. Ndoa ikishafungwa kanisani au sheikh akishafungisha tu basi inatosha kurudi nyumbani kwa amani na kuanza maisha bila stress za ukumbi.
 
Back
Top Bottom