Maandalizi ya shughuli au sherehe ya Engagement: Nahitaji Ushauri Wenu

night_shadow

Member
Aug 4, 2022
11
34
Nina mpenzi wangu ambaye natarajia kabisa kufunga naye ndoa, lakini kuna mambo ambayo naona yanakwenda kinyume na matarajio yangu. Kibinafsi, sipendi kufanya sherehe za harusi zenye gharama kubwa ambazo mara nyingine huwa ni israfu. Hata hivyo, mpenzi wangu ni mtu ambaye anathamini na kupenda mambo ya kifahari na ya kifani. Hali hii imedhihirika wazi wakati nilipokuwa katika hatua za maandalizi ya uchumba wetu(sherehe za engagement).

Gharama za sherehe ya engagement, kama ilivyokadiriwa, inaonesha itapita milioni tatu, na hii ni kiwango kikubwa sana kwangu. Gharama ya mavazi anayotaka kuvaa kwenye sherehe kisio lake ni takriban laki nne, na pete ya engagement inahitaji angalau laki nne ndio minimal cost.

Wakati nikijaribu kumshauri tupunguze matumizi yasiyo ya lazima kwenye sherehe, mpenzi wangu amekuwa na majibu yasiyofurahisha. Mara nyingine, amejisikia kuumizwa na kusema kuwa ninaonyesha kutomjali. Kwa hakika, sina tatizo na uwezo wa kifedha wa kugharamia mahitaji haya yote, lakini nashawishika kuwa ninaweza kutumia fedha hizi vizuri zaidi, hasa kwa kuzingatia kuwa hatujakomaa sana kiuchumi na tunahitaji kujiandaa kwa maisha yetu ya baadaye.

Naja kwenu kwa ushauri; naamini kuna wengi miongoni mwenu ambao wamewahi kukabiliana na changamoto kama hizi katika mahusiano yenu au maandalizi ya ndoa. Je, mnashauri vipi katika kushughulikia hali hii? Je, ni sahihi kwangu kupunguza gharama hizi kimyakimya bila mpenzi wangu kujua au bila kumuumiza mpenzi wangu kihisia? Au mpenzi wangu yupo sahihi kusimamia maoni na matarajio yake? Najiuliza iwapo uamuzi wangu wa kumwacha ni wa busara, au kuna njia bora ya kutatua tofauti zetu hizi.
 
Don’t ever disappoint an engagement, huo ni mfumo mwingine wakuonyesha kujali, ya kwamba kweli una nia ya kuoa. Yaani ni approach ya pili.

Iwe unafanya na marafiki au ndugu, cost lazma iwepo. Maana vitu vizuri, maua dinner vinahitaji gharama.
Ukiweza kafanye engagement na wazazi wake hotelini tenga milioni. Waite wao tu mle dinner umstukize then over, (au hapo hapo utatoa mahari?)

Kama sio watoe out kamvishe pete huko.

Kwa kwenda kwao Cost huwezi ikimbia. Na nadhani ikiwa kwao shughuli inakua yao. Wewe unaenda tu kuvisha pete. Hii yako imekaaje? Yaani wewe ndio utoe cost?
 
Engagement ni sherehe ya muolewaji na ndugu zake. Wewe haikuhusu.

Nenda kalipe mahari kwao then kula ubwabwa wao kisha mvishe pete.

Engagement huwa zinafanyika siku ya mahari nyumbani kwao mwanamke.

Hivyo Wewe sherehe za nyumbani kwao mwanamke hazikuhusu.
 
Natoa na mahari kabisa shukrani nashukuru kuna mahali nimejiona kweli huenda mimi ndio namkosea
 
Nina mpenzi wangu ambaye natarajia kabisa kufunga naye ndoa, lakini kuna mambo ambayo naona yanakwenda kinyume na matarajio yangu. Kibinafsi, sipendi kufanya sherehe za harusi zenye gharama kubwa ambazo mara nyingine huwa ni israfu. Hata hivyo, mpenzi wangu ni mtu ambaye anathamini na kupenda mambo ya kifahari na ya kifani. Hali hii imedhihirika wazi wakati nilipokuwa katika hatua za maandalizi ya uchumba wetu(sherehe za engagement).

Gharama za sherehe ya engagement, kama ilivyokadiriwa, inaonesha itapita milioni tatu, na hii ni kiwango kikubwa sana kwangu. Gharama ya mavazi anayotaka kuvaa kwenye sherehe kisio lake ni takriban laki nne, na pete ya engagement inahitaji angalau laki nne ndio minimal cost.

Wakati nikijaribu kumshauri tupunguze matumizi yasiyo ya lazima kwenye sherehe, mpenzi wangu amekuwa na majibu yasiyofurahisha. Mara nyingine, amejisikia kuumizwa na kusema kuwa ninaonyesha kutomjali. Kwa hakika, sina tatizo na uwezo wa kifedha wa kugharamia mahitaji haya yote, lakini nashawishika kuwa ninaweza kutumia fedha hizi vizuri zaidi, hasa kwa kuzingatia kuwa hatujakomaa sana kiuchumi na tunahitaji kujiandaa kwa maisha yetu ya baadaye.

Naja kwenu kwa ushauri; naamini kuna wengi miongoni mwenu ambao wamewahi kukabiliana na changamoto kama hizi katika mahusiano yenu au maandalizi ya ndoa. Je, mnashauri vipi katika kushughulikia hali hii? Je, ni sahihi kwangu kupunguza gharama hizi kimyakimya bila mpenzi wangu kujua au bila kumuumiza mpenzi wangu kihisia? Au mpenzi wangu yupo sahihi kusimamia maoni na matarajio yake? Najiuliza iwapo uamuzi wangu wa kumwacha ni wa busara, au kuna njia bora ya kutatua tofauti zetu hizi.
We bwana weee.....mbn gharama ya kawaida sana.....kiatu na gauninkwa laki nne kawaida saaana,mi nilivaa gauni la laki saba cku ya uchumba wng,Pete laki nne kawaida sana hapo kagold mix kidani Cha silver,mapambi ukimbi simple home laki tano,mc na mziki laki tatu inayobaki msosi na vinywajo.....mi sherehe nzima ilinicost milion tano na kidogo,pambana bhana
 
Kama umeamua kufanya sherehe, obviously gharama huwezi kuziepuka, Cha msingi ni kujitahidi kuminimize izo gharama, na hakuna mwanamke kwenye siku yake Muhimu kama iyo anakubali kuvaa kawaida lazima anataka aonekane mana wanasema Huwa haijirudii.
Cha msingi
Hakikisha humalizi na madeni au acha kabisa usifanye sherehe.
 
Kwa sababu wewe ndio mtoaji lazima shuguri yoyote iendane na bajeti yako, akitaka zaidi mwambie ajazie. Ukishindwa kudhibiti Sasa hivi atakupa shida mbeleni. Ikifanya zaidi ya uwezo wako ndoa utaona chungu kwani badala ya kuufurahia fungate itakuwa unapambana kulipa madeni ambaya yatakuwa hayaishi.
 
Zingatia ushauri huu!
 
Engagement ni sherehe ya muolewaji na ndugu zake. Wewe haikuhusu.

Nenda kalipe mahari kwao then kula ubwabwa wao kisha mvishe pete.

Engagement huwa zinafanyika siku ya mahari nyumbani kwao mwanamke.

Hivyo Wewe sherehe za nyumbani kwao mwanamke hazikuhusu.
Soma ushauri huu kwa makini, ufanyie kazi!
 
Engagement ni sherehe ya muolewaji na ndugu zake. Wewe haikuhusu.

Nenda kalipe mahari kwao then kula ubwabwa wao kisha mvishe pete.

Engagement huwa zinafanyika siku ya mahari nyumbani kwao mwanamke.

Hivyo Wewe sherehe za nyumbani kwao mwanamke hazikuhusu.
Duuh hii kwa wapare naona ni Tofauti... sherehe unagaharamia muoajiii
 
Nina mpenzi wangu ambaye natarajia kabisa kufunga naye ndoa, lakini kuna mambo ambayo naona yanakwenda kinyume na matarajio yangu. Kibinafsi, sipendi kufanya sherehe za harusi zenye gharama kubwa ambazo mara nyingine huwa ni israfu. Hata hivyo, mpenzi wangu ni mtu ambaye anathamini na kupenda mambo ya kifahari na ya kifani. Hali hii imedhihirika wazi wakati nilipokuwa katika hatua za maandalizi ya uchumba wetu(sherehe za engagement).

Gharama za sherehe ya engagement, kama ilivyokadiriwa, inaonesha itapita milioni tatu, na hii ni kiwango kikubwa sana kwangu. Gharama ya mavazi anayotaka kuvaa kwenye sherehe kisio lake ni takriban laki nne, na pete ya engagement inahitaji angalau laki nne ndio minimal cost.

Wakati nikijaribu kumshauri tupunguze matumizi yasiyo ya lazima kwenye sherehe, mpenzi wangu amekuwa na majibu yasiyofurahisha. Mara nyingine, amejisikia kuumizwa na kusema kuwa ninaonyesha kutomjali. Kwa hakika, sina tatizo na uwezo wa kifedha wa kugharamia mahitaji haya yote, lakini nashawishika kuwa ninaweza kutumia fedha hizi vizuri zaidi, hasa kwa kuzingatia kuwa hatujakomaa sana kiuchumi na tunahitaji kujiandaa kwa maisha yetu ya baadaye.

Naja kwenu kwa ushauri; naamini kuna wengi miongoni mwenu ambao wamewahi kukabiliana na changamoto kama hizi katika mahusiano yenu au maandalizi ya ndoa. Je, mnashauri vipi katika kushughulikia hali hii? Je, ni sahihi kwangu kupunguza gharama hizi kimyakimya bila mpenzi wangu kujua au bila kumuumiza mpenzi wangu kihisia? Au mpenzi wangu yupo sahihi kusimamia maoni na matarajio yake? Najiuliza iwapo uamuzi wangu wa kumwacha ni wa busara, au kuna njia bora ya kutatua tofauti zetu hizi.
Hakuna investment mbovu kuwekeza kama kuwekeza kwenye mapenzi..
 
Back
Top Bottom