USHAURI: Mdogo wangu amekataa shule, nataka nimtafutie fani ya ufundi asiwe mzigo mbeleni

Phdum

JF-Expert Member
Apr 15, 2019
812
1,667
Naombeni ushauri kuhusu mdogo wangu wa kiume ambaye hajamaliza hata shule ya msingi na sasa amekuwa mzigo, kwani mawazo ya kusoma hana. Nataka nimtafutie fani (ufundi) ili mbeleni asijekuwa mzigo, kumbuka ni miaka 18+.

Naombeni ushauri wa fani inayoweza kumfaa na labda pia kama mnajua chuo cha veta kinachotoa fani husika.

Location yake ni Mwanza, Shinyanga, Simiyu, Musoma au Geita.

Nawasilisha
 
Huyo kama kusoma hataki hata usimpeleke VETA, mtafutie gereji akajifunze maisha huko. Au mtafute fundi ujenzi mkabidhi afundishwe kazi apige na vibarua vya zege.
VETA siku hizi hawapokei Tena course ndefu mtoto ambaye hajamaliza sekondari na kufaulu

Hiyo aende tu course fupi kama udereva wa magari au bodabida Kisha badala ya kupoteza Hela kusomesha kamnunulie bodaboda atajijua mwenyewe huko bodaboda haifiki hata milioni mbili nunua mpe achana naye
 
Hizi course za udereva si huwa zina mitihani ili kupata cheti na leseni? Kama hataki kusoma atatoboa kweli?
 
Muulize yeye mwenyewe kua anataka kufanya nini kwenye maisha yake? Unaweza kumpeleka sehemu kisha huko napo asiweke bidii,

Kama hajui anataka nini,mpeleke sehemu ambayo itakua na kazi ngumu na mateso,fanya mpango na muhusika kua ampe shuruba ya kuchapa kazi ili ajue maisha ni nini,

Akikulalamikia kua kazi ni ngumu,mwambie kua hiyo ndio kazi ya level yako coz huna elimu,huenda akili ikamkaa sawa,

Lengo la elimu sio tu kuajiriwa bali ni kupata maarifa ya maisha.
 
Huyo kama kusoma hataki hata usimpeleke VETA, mtafutie gereji akajifunze maisha huko. Au mtafute fundi ujenzi mkabidhi afundishwe kazi apige na vibarua vya zege.
Kuna watu watakuona umeandika ujinga Ila huu ndio ukweli veta ni chuo cha ufundi sasa mtu hataki kusoma unampeleka chuo akabebeshwe madaftari tena wewe beba msogeze kwa mafundi wa mtaani aanze kuchukua ujuzi kidogo kidogo na kuzoeshwa kwa wateja akizoea basi anafungua workshop yake maisha yanaendelea
 
Back
Top Bottom