Ushauri kuhusu ndoa kwa wanaowaza kuoa mke mmoja au kuoa mke zaidi ya mmoja. Uzoefu ni mwalimu mzuri

Azizi Mussa

JF-Expert Member
May 9, 2012
9,172
7,428
Declaration of interest:
========
mleta mada hii ana wake watatu ambao ni marafikiri na wanashirikiana na kusaidiana kwa karibu sana.
======÷==

Facts 15 kuhusu ndoa ukizitumia zitakusaidia.

1. Ndoa japo ya mke mmoja, kwa mwanaume ni kujivika majukumu. Kama haupendi majukumu usioe, kama unapenda oa.

2. Usioe ( japo mke mmoja ) kwa kutegemea starehe. Kama unapenda starehe, unaweza kupata starehe zaidi bila ndoa kuliko ndani ya ndoa. Oa kwa malengo ya kuwajibika na sio kustarehe, ukikutana na starehe mbele ya safari chukulia kama bahati tu(bonus).

3. Usioe mwanamke ukikusudia akusaidie kwa namna yoyote ile. Ukifanya hivyo unajiandaa kuwa disappointed. Oa mwanamke/ wanawake ukiwa umejiandaa kisaikolojia kuwa wewe ndio utam/utawasaidia, kwa lugha nyingine utakuwa mtumishi wake/wao kwa 100℅ . Hapo ndoa haitakuangusha kwa kuwa utakuwa huna cha kupoteza.

5. Usioe ili upate sex. Hiyo ni sehemu ndogo sana ya ndoa na baada ya muda mwanaume akishamzoea mwanamke anamuona wa kawaida. Kumbuka pia kuna kuzeeka na kupoteza mvuto. Aidha, siku hizi sex ni soo cheap. Kwa hiyo kuoa kwa lengo hilo ni kuanza kwa mguu wa kushoto.

6. Usioe kama una asili ya uchoyo. Ukishaoa ni kama unakuwa umejicommit kugawa vitu vyako kwa watu wengine. So kama una roho ya ubinafsi utaishi kwa shida sana.Ili ndoa isikupe stress oa kama wewe ni "giver" .ila kama ni "taker" au "matcher" ndoa waachie wenzio au ujiandae kuishi kwa mateso maisha yako yote.

7. Kama una wivu sana usioe. Ukioa ili uweze kuishi kwa amani, unatakiwa usiwe na wivu sana kwa sababu unayemuoa pia alikuwa na uhusiano na watu wengine kwa namna mbalimbali na huko anakopita anakutana na mengi.Kuwa na imani na mke/wake zako maadam hujaona jambo la kukudhuru.

8. Usimchunguze sana mwanamke. Maadam hajakudhuru na anakuheshimu na hujamuona akifanya kitu kisichokuwa cha kawaida. Vinginevyo unachokitafuta utakipata.

9. Watoto wa mke wako, amini ni wako bila kutaka ushahidi wa ziada. Usichunguze wala kuhoji. Aidha, hata ukibaini si wako, usipaniki, wapende na uwaleee kiroho safi kwani watoto ni watoto tu.

9. Ukioa mke/ wake, usiwe laizess affair sana. Demokrasia haifanyi kazi kwa hawa wenzetu. Wakati fulani kuwa na misimamo mikali. Wakibaini wewe ni tia maji tia maji, wanachukua uongozi wa familia wao, na wao wana option moja tu; Kukutawala kidikteta.Na

10. Usioe mke zaidi ya mmoja ukilenga kustarehe bali oa ukilenga kujiongezea majukumu ya ziada. Hautajuta kwa namna yoyote na ikitokea wakiwa wa msaada kwako, itakuwa added advantage.Aidha, hao wanawake wajue kabisa kuwa hujawaoa ili kuwatumia bali kuwatumikia/kuwajenga. Hapo ni rahisi ku maintain nidhamu.

Bonus

11. Sio kila mwanamke anayefaa kuoa, usikimbilie kuoa bali kuwa makini sana unamuoa nani au unawaoa kina nani. Tumia zaidi akili kuliko hisia pia epuka mashinikizo ya watu.

12. Ukiona unamfuatilia mwanamke na haziivi, usioe hata iwe vipi. Hiyo ni red light. Wewe jenga uhusiano mzuri tu na watu unaoona ni watu wema halafu mke/wake watakuja bila kutumia msuli.

13. Usioe kama huna uchumi wa kuweza kupata mahitaji ya msingi. Utaishia kujiona umelogwa kumbe ni mazingira tu.

14. Kuwa bahili sana wakati wa uchumba. Aidha, ukiona mwanamke hana huruma na hela yako, huyo hafai kuwa mke. Utalia. Mwanamke anayefaa kuwa mke anakuonea huruma na anaonea huruma mali/fedha zako kupotea ovyo.

15. Familia ni taasisi. Lazima taasisi iwe na mkuu wa taasisi mmoja na vision moja. Huyo ni mwanaume. Sikiliza ushauri ila anayetakiwa ku conclude ni wewe. Vinginevyo hamtoboi mwaka.

Niishie hapo kwa leo.
 
Sasa faida ya Kuoa ni ipi Kwa Mwanaume?
Unapenda majukumu?
Hata usipooa majukumu yapo tu?
Usitegemee Ngono? Sasa kama Nyapu ni ya kipimio niingize ndani ili awe nini? Awe nani? Na raha yake ipoje?

Dunia hii na hekaya za kushangaza?
 
Tunatamani demokrasia lakini CCM anatumia polisi kututawala kidikiteta huku akitunyonya kwa rushwa..

Mapenzi hayana mwenyewe..
Oa ukiwa unataka kuoa .
 
Kwa maoni yangu na experience binafsi ( silazimishi watu wengine wakubaliane nami) Ndoa ipo kwa ajili ya kuwanusuru wanawake na watoto. Kwa kufanya hivyo, kizazi cha binadamu kinaweza kunusurika, kuendelea na kustawi. Kinyume chake wanawake na watoto watapoteza muelekeo na hivyo dunia kupoteza muelekeo.

Mwanaume kaumbwa kama kiumbe wa kuvaa majukumu. Hivyo ndoa ni sehemu ya kuvaa majukumu kwa mwanaume. Hata hivyo jukumu hilo ni muhimu sana ili dunia iweze kuwa stable.

Hata hivyo kwa sababu mbalimbali, kwa kiasi sasa mambo yamepinduka na kuna mazingira ambapo wanaume ndio hutegemea wanawake. In the future, hili ni janga kubwa linalokuja kuikumba dunia.
 
Tunatamani demokrasia lakini CCM anatumia polisi kututawala kidikiteta huku akitunyonya kwa rushwa..

Mapenzi hayana mwenyewe..
Oa ukiwa unataka kuoa .
Mkuu, ishu sio kuoa. Ishu ni kile kitakachokuja kukupata baada ya kuoa kama hukuzingatia hivyo hapo juu.

Ijapokuwa kuna dynamics za hapa na pale, lakini angalau hayo hapo juu tanaweza kuleta matokeo yanayofanana kwa ℅ kubwa.
 
Namba 15 ndio usahihi wenyewe.
Ukifuata ushauri wa mwanamke utapotea.
Labda awe kakuoa yeye na unafuata anayotaka yeye.
 
Unatakiwa unakandamiza 70℅-80℅ udikteta halafu 20 ℅ demokrasia. Vinginevyo hutoboi ndugu yangu. Hii ni mujarab!.

Ndio maana ndoa za dot.com hazidumu kama za samani kwa sababu sahizi hakuna kiongozi wala msemaji wa familia. Kila mwanaume ni mwamba mwanamke mwamba, na miamba miwili haikai pamoja na hata ikikaa ujue moto unawaka.
 
Sasa faida ya Kuoa ni ipi Kwa Mwanaume?

Dunia hii na hekaya za kushangaza.
Unapofikiria kuoa, fikiria utakavyomnufaisha unayemuoa na usifikirie yeye atakavyokunufaisha wewe.

Kama itatokea mbele ya safari akakunufaisha, utaichukulia hiyo kama bahati tu.

Mtizamo huo utakusaidia usiwe dissapointed. Vinginevyo uwezekano wa kuwa dissappointed ni zaidi ya 99.99999℅ unayoyatarajia hayatatokea unavyofikiria.
 
Bado nina miaka 15 ya kujipima kwenye hivyo vipengele kama naweza au lah ndo nipate jibu naingia au napolea kwa nje.
 
Declaration of interest:
========
mleta mada hii ana wake watatu ambao ni marafikiri na wanashirikiana na kusaidiana kwa karibu sana.
======÷==

Facts 15 kuhusu ndoa ukizitumia zitakusaidia.

1. Ndoa japo ya mke mmoja, kwa mwanaume ni kujivika majukumu. Kama haupendi majukumu usioe, kama unapenda oa.

2. Usioe ( japo mke mmoja ) kwa kutegemea starehe. Kama unapenda starehe, unaweza kupata starehe zaidi bila ndoa kuliko ndani ya ndoa. Oa kwa malengo ya kuwajibika na sio kustarehe, ukikutana na starehe mbele ya safari chukulia kama bahati tu(bonus).

3. Usioe mwanamke ukikusudia akusaidie kwa namna yoyote ile. Ukifanya hivyo unajiandaa kuwa disappointed. Oa mwanamke/ wanawake ukiwa umejiandaa kisaikolojia kuwa wewe ndio utam/utawasaidia, kwa lugha nyingine utakuwa mtumishi wake/wao kwa 100℅ . Hapo ndoa haitakuangusha kwa kuwa utakuwa huna cha kupoteza.

5. Usioe ili upate sex. Hiyo ni sehemu ndogo sana ya ndoa na baada ya muda mwanaume akishamzoea mwanamke anamuona wa kawaida. Kumbuka pia kuna kuzeeka na kupoteza mvuto. Aidha, siku hizi sex ni soo cheap. Kwa hiyo kuoa kwa lengo hilo ni kuanza kwa mguu wa kushoto.

6. Usioe kama una asili ya uchoyo. Ukishaoa ni kama unakuwa umejicommit kugawa vitu vyako kwa watu wengine. So kama una roho ya ubinafsi utaishi kwa shida sana.Ili ndoa isikupe stress oa kama wewe ni "giver" .ila kama ni "taker" au "matcher" ndoa waachie wenzio au ujiandae kuishi kwa mateso maisha yako yote.

7. Kama una wivu sana usioe. Ukioa ili uweze kuishi kwa amani, unatakiwa usiwe na wivu sana kwa sababu unayemuoa pia alikuwa na uhusiano na watu wengine kwa namna mbalimbali na huko anakopita anakutana na mengi.Kuwa na imani na mke/wake zako maadam hujaona jambo la kukudhuru.

8. Usimchunguze sana mwanamke. Maadam hajakudhuru na anakuheshimu na hujamuona akifanya kitu kisichokuwa cha kawaida. Vinginevyo unachokitafuta utakipata.

9. Watoto wa mke wako, amini ni wako bila kutaka ushahidi wa ziada. Usichunguze wala kuhoji. Aidha, hata ukibaini si wako, usipaniki, wapende na uwaleee kiroho safi kwani watoto ni watoto tu.

9. Ukioa mke/ wake, usiwe laizess affair sana. Demokrasia haifanyi kazi kwa hawa wenzetu. Wakati fulani kuwa na misimamo mikali. Wakibaini wewe ni tia maji tia maji, wanachukua uongozi wa familia wao, na wao wana option moja tu; Kukutawala kidikteta.Na

10. Usioe mke zaidi ya mmoja ukilenga kustarehe bali oa ukilenga kujiongezea majukumu ya ziada. Hautajuta kwa namna yoyote na ikitokea wakiwa wa msaada kwako, itakuwa added advantage.Aidha, hao wanawake wajue kabisa kuwa hujawaoa ili kuwatumia bali kuwatumikia/kuwajenga. Hapo ni rahisi ku maintain nidhamu.

Bonus

11. Sio kila mwanamke anayefaa kuoa, usikimbilie kuoa bali kuwa makini sana unamuoa nani au unawaoa kina nani. Tumia zaidi akili kuliko hisia pia epuka mashinikizo ya watu.

12. Ukiona unamfuatilia mwanamke na haziivi, usioe hata iwe vipi. Hiyo ni red light. Wewe jenga uhusiano mzuri tu na watu unaoona ni watu wema halafu mke/wake watakuja bila kutumia msuli.

13. Usioe kama huna uchumi wa kuweza kupata mahitaji ya msingi. Utaishia kujiona umelogwa kumbe ni mazingira tu.

14. Kuwa bahili sana wakati wa uchumba. Aidha, ukiona mwanamke hana huruma na hela yako, huyo hafai kuwa mke. Utalia. Mwanamke anayefaa kuwa mke anakuonea huruma na anaonea huruma mali/fedha zako kupotea ovyo.

15. Familia ni taasisi. Lazima taasisi iwe na mkuu wa taasisi mmoja na vision moja. Huyo ni mwanaume. Sikiliza ushauri ila anayetakiwa ku conclude ni wewe. Vinginevyo hamtoboi mwaka.

Niishie hapo kwa leo.
Maneno kuntu sana, huu uzi umetulia vyema.
 
Tutakuwa na rais wetu wa awamu ya 8 nafikiri sio mbali sana kutoka 6, pia nina makombe ya dunia matatu mbele yakutazama nikiwa bado natafakari, pia nina sensa moja tu nimebakiza maybe ndo itakuwa ya mwisho nikiwa single. Dah! kiukweli muda unakimbia tuombe uhai.
 
Hehehehe, kama hufiti kwenye mambo angalau 12 hapo juu, fanya ishu nyingine bro.
 
Back
Top Bottom