Ndoa ya mke mmoja ni maagizo potofu ya mwanadamu, sio Mungu. Ukweli huu hapa

tpaul

JF-Expert Member
Feb 3, 2008
21,859
18,277
Naingia kwenye mada moja kwa moja bila kuchelewa. Kuoa wake wengi ninaamini ni sawa kwa utamaduni wa mababu zangu na kwa dini zote za asili ya Abraham maana hakuna ilipozuiwa. Nitakuwa mwendawazimu sana nimezalizaliwa na mke wa pili kwa baba na kisha nimezeshwe dhana ya uongo tu na mchungaji au pastor kuwa mke wa pili ni kosa na hivyo nami nijione haramu bila hata kutafiti.

Moja, nimefanya utafiti nimegundua dini haizuii na mwanzo wa jambo hilo ni tamaduni ya Urumi (Roman Empire) ambapo wao utamaduni wao ulikuwa mke mmoja tu. Hivyo sioni haja ya kuamini utamaduni wa Kirumi na kuacha utamaduni wa mwafrika.

Pili, kama Mungu anaamini nyumba ndogo ni haramu asingeruhusu Yesu azaliwe katika uanadamu wake atokee nyumba ndogo.

Historia ya dunia hii nimejaribu sana kuisoma kila sehemu. Mwanzilishi wa jambo hili kuliweka kwenye sheria ya kirumi kabisa na kuhakikisha siyo utamaduni pekee bali sasa liko kwenye sheria ya kirumi dhama hizo anaitwa emperor Augustus! Na kwa msaada tu huyu ni mtoto wa emperor Julius Ceasar (mnaita Julius Kaisari).

Wakati mitume wa yesu wanakimbia Rome baada ya yesu kufa walikuta hii sheria ni kali sana, mke mmoja na mume mmoja. Na wakristo wanaanza kuuliza vipi hili mbona linakingana na torati mnasemaje? Soma kitabu cha Tito ambapo wanaorodheshwa ambao wamezuiwa kuoa zaidi ya mke mmoja. Tena kinasema kabisa kwamba "wafuatao wawe waume wa mke mmoja". Sasa wametajwa. Sisis katika hao waliotajwa hatumo, inakuwaje mchungaji atumezeshe hiyo imani tuikubali?

USHAURI WANGU
Nawashauri wanaume wenye uwezo wa kuoa mke zaidi ya mmoja wafanye hivyo mara moja kwani hakuna kifungu cha biblia hata kimoja kinachowazuia kufanya hivyo. Watu waoe mitala wazae na kuijaza dunia. Hili ndilo agizo la Mungu Baba Mwenyezi. Maagizo mengine yoyote yale ni ubatili kwani yametokana na utashi wa wanadamu!
 
Kwa hiyo sheria ilitaka tuwe na wake wangapi?
Wewe ungependa kuoa wake wangapi?

Note:
Andiko la Tito umelitumia vibaya, umeshindwa kuelewa context. Suala la maaskofu kutakiwa kuwa na sifa ya kuoa mke mmoja lililenga kuwazuia watu ambao kabla ya kuwa wakristo walikuwa na wake wengi (na kwa kuwa ukristo usingeweza kufuta historia zao za nyuma za kuoa) basi kanuni ya kupewa uaskofu ikawazuia ili kulinda heshima ya kanisa machoni pa watu.
 
Nature hujieleza je kuna mwanamke anataka mke mwenza??
 
Naingia kwenye mada moja kwa moja bila kuchelewa. Kuoa wake wengi ninaamini ni sawa kwa utamaduni wa mababu zangu na kwa dini zote za asili ya Abraham maana hakuna ilipozuiwa. Nitakuwa mwendawazimu sana nimezalizaliwa na mke wa pili kwa baba na kisha nimezeshwe dhana ya uongo tu na mchungaji au pastor kuwa mke wa pili ni kosa na hivyo nami nijione haramu bila hata kutafiti.

Umeskika kiongozi sema sasa tujibebeshe wangapi?
 
Naingia kwenye mada moja kwa moja bila kuchelewa. Kuoa wake wengi ninaamini ni sawa kwa utamaduni wa mababu zangu na kwa dini zote za asili ya Abraham maana hakuna ilipozuiwa. Nitakuwa mwendawazimu sana nimezalizaliwa na mke wa pili kwa baba na kisha e mitala wazae na kuijaza dunia. Hili ndilo agizo la Mungu Baba Mwenyezi. Maagizo mengine yoyote ni ya wanadamu tu!
Huo ni mtazamo wako wewe oa kadri uwezavyo lakini usijaribu kutumia maandiko kupotosha Imani.
 
Ushapata kibanda hasara mzee mwenzangu, kishakufinyia kwa ndani unatafuta sababu ya kutengua sheria kisheria.😂🤣

Fanya mpango hii sheria ife, mie nakuwaje na mke mmoja🤣😂😂
Sheria hiyo imeandikwa wapi mkuu? Acha kutetea sheria za wanadamu bila ushahidi mkuu.
 
Mungu angetaka hio polygamy system, angemuumbia Adam mke zaidi ya mmoja.
Ila hakufanya hivo, alimuumbia Adam mke mmoja tuu na Adam akarithika na kukaa naye maisha yake yote na hakuongezewa mke.
Hii ni ASSUMPTION yako mkuu. Huu ulikuwa uamuzi wa Mungu kuumba pair moja ya ke na me. Angependa angeweza kuumba pair nyingi tu. Hata hivyo, baada ya kuwaagiza Adam na Hawa wazae na kuiongeza dunia hakuna mahali alielekeza (kwenye biblia takatifu.....neno la Mungu) kila mwanaume aoe mke mmoja tu. Nipe kifungu walau kimoja kinachosema hivyo. Otherwise uache kuwapotosh watu kwa maneno ya kufikirika/kudhania
 
Mungu angetaka hio polygamy system, angemuumbia Adam mke zaidi ya mmoja.
Ila hakufanya hivo, alimuumbia Adam mke mmoja tuu na Adam akarithika na kukaa naye maisha yake yote na hakuongezewa mke.
Mkuu hujasoma maandiko vizuri, huijui biblia na desturi za wayahudi!

Kwa taarifa yako mke wa kwanza wa Adam alikuwa Lilith, Eva ni mke wa pili baada ya Lilith.

Na pia Adam sio binadamu wa kwanza kuumbwa.

Adam ni mtu wa kwanza kuumbwa kwa udongo shambani Eden.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom