Usaliti na Unafiki unavyoangamiza Taifa - Lema

Usaliti na Unafiki unavyoangamiza Taifa - Lema

Status
Not open for further replies.
Lema huna lolote, wewe ni mnafiki tu, wewe si mtetezi wa wanchi, wewe huna uchungu wa wananchi, unachokipata sasa n kwa kuwa wanchi wameichoka CCM na bahati mbaya hawana uwezo mkubwa wa kupambanua mambo.

Kudhihirisha wewe ni mnafiki, kwa nini usimtaje huyo kiongozi???? Hata TANU walikuwa na ahadi zao na ahadi mojawapo ni NITASEMA KWELI DAIMA, FITINA KWANGU MWIKO, sasa wewe kama washindwa kumtaja kiongozi wa juu wa CHADEMA kuna tofauti gani na kufanya fitina na kuleta unafiki????

Ni aibu kwa kiongozi kama wewe kujitokeza hadharani nyakati kama hizi ambazo chama chako kimetoka kumsimamisha Samsoni Mwigamba kwa tuhuma za kuwasema viongozi wake, kwenye mitandao, je wewe unachomkifanya sasa kina tofauti gani na cha Mwigamba??

You are just pathetic MP!! Na kama ukombozi tunaoutafuta ni kuja kuongozwa na watu opportunists kama wewe, ni aheri tusiupate kabisa!!

So sad, so sad, so sad, kusoma huu utumbo wako Mheshimiwa, tafadhali anua nguo zako chafu ulizoanika kwenye kamba!!!

Punguza hasira...jadiliana.....Kazi mnayo leo>

Cha kushangaza asilimia kubwa ya wale maadui wa CHADEMA ndiyo wanaomsuta Lema.Songa mbele kamanda.Hapa Hakuna kurudi nyuma
 
NCCR mageuzi ilianzaga hivi hivi....kuwapa matumaini makubwa watanzania, just to find out kuwa ilikuwa a bunch of traitors na wote tunawajua. More than a decade ya serious politics za CDM, naona tunataka kurudishwa kule kule kwa 1995!

Kaizer ni kweli mambo haya anayo yafanya lema yana turudisha tulipo toka.

Hivi kama lema ni jasiri kwa nini asipeleke ushahidi kwenye vikao vya chama?

Godbless J Lema kwa hili unachangia kuivuruga chadema na hapa una saidiana na maadui wa chadema kabisa..

Hivi kweli kama kuna ushahidi usio tia shaka kwanini asiupeleke kwenye chama.

Kwa kweli tuungane kukataa hili swala na njia hii ya lema.
Amepotoka.
 
Last edited by a moderator:
It has gradually started peeling itself off.

But ,I better remain with coyness till when get ratified officially.

This time last year,if not mistaken, I spoke of the devil that he is not a part and parcel of the party movements cause of his personal interests.

Now, as I can see beyond an enclosed and darkened cave, people are getting so serious over the issues.

hope it will get known asap!!
 
Mwgamba alilalama hapa akapgwa na kusimamishwa. Lema anasema chamani kuna wasaliti na wamepoteza ndoto za wengi ataachwa tu. Najua lema anamaansha zitto kabwe sababu amepinga posho.

Mwigamba alitumia ID fake, Lema ametumia Id yake mwenyewe. Tabia na akili yako ni za kipimbi
 
Na ili tusirudi huko ni lazima tuchukue different approach ku-deal na elements zinazofanana na zile zilizoiua NCCR-Mageuzi.Ndiyo falsafa ya kumtoa nyoka mdogo ndani

yeah mkuu Ben Saanane nadhani tukumbuke historia. Acts of omission (failure to take action) zina hasara kubwa sana. Natambua kwamba kwa namna moja au nyingine inainvolve risk taking, ila ikifanyika riska analysis na namna ya kuzimitigate it should be possible to move foward baada ya kuwaweed out wasaliti, ambao kwa mujibu wa mifumo ya kiintelijensia ya kichama wanafahamika.

CCM wameachana na Mansour Yusuph Himid majuzi.......CUF walijaribu sana kupambana na Hamad Rashid, NCCR na Kafulila wao. CDM should "get serious" now....si kuna mambo ya BRN!
 
Last edited by a moderator:
Wazo lako ni zuri sana ndugu mh.

Lakini kwanini umeamua kuleta hoja hii katika jamiiforums ilihali kuna vikao halali vya chama.

Good and sensible commentary! Bwana Lema anataka kutuambia nini? Anataka kusema humo ndani ya vikao hakuingiliki? Anataka kusema uvumilivu na hekima vimetoweka Chadema na kwamba angepeleka haya hakuna wa kumsikiliza? Anataka kuhalalisha njia ile ile aliyotumia Mwigamba kukikosoa Chama, yaani kupeleka manunguniko ndani ya JF!

Naamini Lema hajapenda kufanya hivyo lakini amesukumwa na ule unaso wa ujana, labda niseme 'infatuations' ambazo zimeshamfanya na kuamini kabisa kwamba yeye yuko sahihi na wengine sio, kwamba Chadema itaunda serikali 2015 na si wengine, kwamba njia ni nyeupe sasa kwa nini watu wengine wanataka kuweka visirani barabarani wakwame?

Bw Lema, punguza munkari, tunajua una weledi mkubwa katika tasnia hii ya siasa, mvuto kwa vijana na nadiriki kusema hata wazee na wamama. Nenda taratibu! Soma ujumbe huu kutoka tuzo muruwa ujifariji, uendelee kutumikia watu wako kama ulivyokwisha kufanya nao waone fahari ya kuwa na wewe, uwe mvumilivu, mnyenyekevu, msikivu- wasikilize hata mapunguani nao wana mchango wao katika jitihada zako: haya tembelea hapa: Desiderata - Desiderata Poem by Max Ehrmann - Desiderata Prints
 
What is the correlation?Lema hajataja jina la mtu.Huyo Mwingine alitumia Fake ID kuchafua viongozi na chama kwa ujumla.Ni wapi Lema alikochafua?Ametoa general knowledge na angalizo.Ni kanuni zipi zinazombana hapa kikatiba?Leteni kanuni hizo hapa na vifungu vya katiba vilivyovunjwa badala ya kufuata mkumbo tu.JF si Home of Great thinkers?

Endeleeni kuumbuana kwenye mitandao alafu mje muone athari zake hapo baadae.

Itafika wakati itakuwa "it is already too late".

Namsifu sana Dr.Slaa kwani anautumia huu mtandao kujibu tuhuma tuu na si kuanzisha tuhuma na kuwapa watu faida.
 
Last edited by a moderator:
Lema, maelezo yako ni mazuri sana na ni ya kizalendo kabisa isipokuwa umeyaleta mahali pasipohusika.Hapa JF ulipoleta hoja hii, hapatasaidia kutatua tatizo hili bali pataongeza mpasuko kwa sababu macho yote ya maccm yanaangalia Jf kuona kama kuna jambo chadema,ili walivalie njuga na maccm ndiyo yatajitokeza sana kuchangia humu jf kwa nia ya kuibomoa cdm kwa sababu umewatengenezea mlango wa kuingilia.

Mimi nakushauri,kwa sababu mtu huyu anajulikana kwa nini usifikishe suala hili katika ngazi za juu ili litatuliwe? Bahati nzuri mwakani kuna uchaguzi wa chama,kamati kuu ya chadema ikiridhika na tuhuma hizi, kazi yake itakuwa ni kulifuta jina lake ktk nafasi atakayoomba.Madhara yake yatakuwa ni madogo kuliko kumfukuza kama unavyoshauri.

Kwa sasa kabla ya uchaguzi kufika, nashauri, kama tuhuma hizi ni kweli, basi uongozi wa chama umfanyizie mtu huyu kama unavyomfanyizia Shibuda.

Naamini tutafika salama, kumbuka katika msafara wa mamba, kenge hawakosekani.
 
Kaizer ni kweli mambo haya anayo yafanya lema yana turudisha tulipo toka.

Hivi kama lema ni jasiri kwa nini asipeleke ushahidi kwenye vikao vya chama?

Godbless J Lema kwa hili unachangia kuivuruga chadema na hapa una saidiana na maadui wa chadema kabisa..

Hivi kweli kama kuna ushahidi usio tia shaka kwanini asiupeleke kwenye chama.

Kwa kweli tuungane kukataa hili swala na njia hii ya lema.
Amepotoka.

Mkuu Ruttashobolwa, another way of looking at this ni kwamba si ajabu ni kweli Mh Lema anajua kwamba chama kinafahamu, lakini pia ako aware na the fact kwamba chama kinaweza kusita sita kuchukua hatua stahiki kwa muda stahiki, sasa anachofanya hapa (kwa maono yangu) ni advocacy kwa maana ya kulet people know what he think should be taken, na hii ina put pressure kwa party structures to act.....ni kama maandamano flani hivi ya kudai haki, sema ya leo ameyachukua "solo" LOL
 
Last edited by a moderator:
Huyu mnafiki kwa kuendeleza unafiki wake na kuwaharibia future vijana aliendelea kugawa ruzuku kama ifuatavyo:

Tarehe 26/3/2012 saa 11:12 asubuhi, MNAFIKI kupitia namba yake ya simu +2557568..53. aliwatumia shilingi 150,000/= wafuasi wa kundi lake, Juliana +255756.5..73, Habi+255.6217.6.., Mtela +2557.5..89.7, Burton +25571..167.., Eddo +25575..49..3, Grey +255755.2..0., Deo +2556.50..60., Adam +2557..137..1, Exaud Mamuya +2557671606.., Ben Saanane +255768078...(CISS),

Baada ya hapo saa 11:43 asubuhi hiyohiyo MNAFIKI kupitia namba yake ya simu +25575.8.9.3. alimtumia shilingi 200,000/= John Shibuda +2557544655..

Mkuu umezidi kunikumbusha namna anavyoivuruga chama letu aondoke tu, tumemchoka...
 
Mkuu Lema, pengine utusaidie kutupatia maana halisi ya 'Usaliti', 'Unafiki' na 'utu' kwa namna uelewavyo wewe.

Maneno haya kutoka kwako yananishangaza kidogo, kwa vigezo kuwa kwa yale unayofanya nawewe unaweza fuzu kuitewa Mnafiki na Msaliti asie na utu. Labda kama unatumia hii njia kujikosha baada ya wewe pia kutambua kuwa umeonyesha Usaliti mkubwa kwa Watanzania unaowawakilisha.

Lema inatakiwa uelewe haya;

Unatakiwa kujua kuwa hata kina KUBENEA wameshamchoka, yeye si mmoja wa hao anaowasema? (Au woga ambao siku zote unashabikia ni sumu leo si sumu tena?), pitia hii https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/547535-mh-lema-anaivuruga-chadema.html

Watanzania wengi washakushtukia, unakiruvuga chama kwa siasa zako za kishabiki na kitoto wenzetu wanaita 'armature' (an insult ukiichukulia undani wake) pitia hii https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...gwe-gavana-rahisi-kusababisha-mitafaruku.html

Inawezekana unawashambulia Shibuda na Zitto kwenye bandiko hili, vipi ni kwakuwa wewe Lema unapenda sana Posho hivyo umeamua liwalo na liwe? pitia hii https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...bungeni-zitto-lema-katika-vita-ya-maneno.html

Au unataka kusema hizi posho zinamaanisha Uzalendo na Utu kwa Taifa? (Are you serious??). Zitto alisha litabiri hili na kueleza wazi (hakutumia unafiki) kuwa Siasa za Posho zitasababisha mjenge chuki na mmwite majina yote mabaya! www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/299635-zitto-sijahongwa-ni-siasa-za-urais-na-hasira-za-posho.html

Au hii ndiyo step ya kwanza ya kufanya Zitto aondoke Chadema? Maana inajulikana wazi kuwa kuna mkakati wa kumkatisha tamaa Zitto aondoke CHADEMA mapema kabla mwaka haujaisha ili mpumue ndani ya chama cha watu wa Kaskazini (viongozi wa juu). Inaturudisha kule kule mnako kukataa siku zote (Udini/Ukabila).

Pole zako Lema, watanzania wa leo si mabwege!

Mimi si mshabiki wa magwanda lakini nakufagilia kwa ulichokiainisha hapo.

Swadakta.
 
Lema,maelezo yako ni mazuri sana na ni ya kizalendo kabisa isipokuwa umeyaleta mahali pasipohusika.Hapa JF ulipoleta hoja hii, hapatasaidia kutatua tatizo hili bali pataongeza mpasuko kwa sababu macho yote ya maccm yanaangalia Jf kuona kama kuna jambo chadema,ili walivalie njuga na maccm ndiyo yatajitokeza sana kuchangia humu jf kwa nia ya kuibomoa cdm kwa sababu umewatengenezea mlango wa kuingilia.
Mimi nakushauri,kwa sababu mtu huyu anajulikana kwa nini usifikishe suala hili katika ngazi za juu ili litatuliwe? Bahati nzuri mwakani kuna uchaguzi wa chama,kamati kuu ya chadema ikiridhika na tuhuma hizi, kazi yake itakuwa ni kulifuta jina lake ktk nafasi atakayoomba.Madhara yake yatakuwa ni madogo kuliko kumfukuza kama unavyoshauri.
Kwa sasa kabla ya uchaguzi kufika,nashauri,kama tuhuma hizi ni kweli,basi uongozi wa chama umfanyizie mtu huyu kama unavyomfanyizia Shibuda.
Naamini tutafika salama,kumbuka katika msafara wa mamba,kenge hawakosekani.

Mkuu swala kama hili chama wana lifahamu ila wana mlea lea tu tangu siku nyingi sijui ni kwanini.....
 
Ninacho pingana na yeye ni kuja kulalama humu, hivi huyo msaliti kamjua leo?
Hivi kwa nini asipeleke ushahidi hili achukuliwe hatua?
Mimi naamini lema ana nafasi kubwa ya kupeleka malalamiko yake kwenye chama si humu.
Mungi lazima tukubali njia anayo hitumia lema si sahihi, hizi ni vurugu.

Mungi kwa pamoja tuseme hapana kwenye hili lema amepotoka.
Lawyer,

It is unfortunate wewe siyo mhudhuriaji sana wa hili jukwaa, ama we ni msomaji zaidi ya mchangiaji. Kama unavyoelewa kuna mada nyingi dhidi ya Lema siku za hivi karibuni, ambayo ilitaka kugeuza taswira sahihi na watu wakauamini uwongo kuwa ukweli.

Lema hajamtaja mtu, bali ametoa hili kama angalizo kwa chama akiwa verified. ni kweli kwamba hakumjua leo huyu msaliti.

Kwa kufanya alichokifanya Lema jamii inajua Lema ni mtu wa namna gani. Kukaa kimya wakati mwingine jamii inaweza kuaminishwa tofauti na ukweli.

Alichokifanya Lema ni kutoa elimu kwa jamii kuwa wanafiki na wasaliti siyo wakuvumiliwa hata kidogo. wanatakiwa kuondolewa kabla hawajaleta madhara. Ni jukumu la chama sasa kuchukua hatua.

Kuleta hii mada humu inasaidia jamii hasa GTs kutoa maoni yao juu ya hatua inayotakiwa kuchukuliwa dhidi ya wasaliti mahali popote siyo tu chadema, bali hata kwenye taasisi zingine za kujamii
 
Unafiki hauondolewi kwa unafiki, bali ukweli na uwazi. Mnamsingizia tu, hamna ushahidi wa kumtia hatiani
 
Huyu mnafiki kwa kuendeleza unafiki wake na kuwaharibia future vijana aliendelea kugawa ruzuku kama ifuatavyo:

Tarehe 26/3/2012 saa 11:12 asubuhi, MNAFIKI kupitia namba yake ya simu +2557568..53. aliwatumia shilingi 150,000/= wafuasi wa kundi lake, [/oB]Juliana +255756.5..73, Habi+255.6217.6.., Mtela +2557.5..89.7, Burton +25571..167.., Eddo +25575..49..3, Grey +255755.2..0., Deo +2556.50..60., Adam +2557..137..1, Exaud Mamuya +2557671606.., Ben Saanane +255768078...(CISS),

Baada ya hapo saa 11:43 asubuhi hiyohiyo MNAFIKI kupitia namba yake ya simu +25575.8.9.3. alimtumia shilingi 200,000/= John Shibuda +2557544655..



Game over!!!!!!
 
Lazima ifike muda watu watambue kuwa akili na busara zinahitajika sana ili kufanya nchi yetu isonge mbele. Chadema chini ya hawa akila Lema they dont seem kuelewa upinzani ni nini hasa na unatakiwa uwe vipi??

Lema, pole sana ukidhani umeandika kitu cha maana sana hapo juu kumbe pumba zile zile za akina slaa na mbowe na akina ben saa nane ( the puppet)

Kwanza, taja jina na weka wazi msaliti ni nani? maana inajulikana hauna ushirikiano na urafiki mzuri na zito zuberi kabwe, inajulikana

wewe , salaa, mbowe na wenzenu mmejitahidi kuwafanya wanachadema wengine waonekane mbumbumbu na hamnazo simply kwa sababu wamewaaamini mno, na kuwapenda, kwani CCM imewachosha, lakini mmekaa ki-NGO zaidi, kikanda, kikabila kila kukicha chuki na asilimia 90 ya mazungumzo yenu ni ugomvi wa chama chenu na si kuiondoa ccm inaleta nini?

1. ugomvi wa chama chenu unapoonekana kwa watu wa nje unawavunja moyo hasa wakichukulia historia za cuf na nccr mageuzi

2. ugomvi wa ndani unawarudisha nyuma na kuleta sintomfahamu nyingi kiasi cha kuwa vitani kila mmoja anarudi nyuma maana unaweka viulizo nani wa KUAMINIWA??

3. Unaendeleza ugonjwa wa yaleyale ya mwigamba ya kusemea mtandaoni hivyo basi inaonyesha kuwa

a/. hauna ubavu wa kuwa face hao unaowaita wasaliti ndani ya chama simply kwa sababu UNAOWAITA WASALITI SIO WASALITI ILA WANASIMAMIA HAKI NA UKWELI

b./ umekuja na hoja za wasaliti ukijua JF itaku support kwani JF wengi ni wanachadema, umesahau kuwa ni sehemu ya ukweli na uwazi, WEWE MBUNGE UKILIA HIVI, mwita maranya afanyaje????

c/. mnaowaita wasaliti hamuwezi kuwaondoa kwenye vikao vya chama maana watawashinda kwa hoja za katiba ya chama, kwa mfano HAIWEZEKANI KIJANA KAMA WEWE, SMART, NA AKIL ZAKO unakuwa wa KWANZA KUCHEKEA KUTOFANYA UCHAGUZI NA KATIBA YA CHAMA KUBAKWA kisa uonekane mzuri kwa mbowe na slaa?? mkipewa nchi mtafanyaje??

Hii dalili ya kusemea mitandaoni kwa mtu mkubwa kama wewe ni UDHAIFU na kwa akili zenu mnajua wengine hatuoni vile...na ndio maana mtaishia kutukuzwa na kupigiwa makofi na washabiki na sio umma......utasifiwa na vilaza na waliopofushwa na mahaba yaliyotokana na chuki kwa ccm na sio reality za kuwa nyie ni wakombozi

Lema, SOMA KWA NGUVU HAPA, HATA ZITTO MKIMTOA LEO NDANI YA CHADEMA, ATABAKAI KUWA ZITTO, zitto ni rais anayeishi mioyoni mwa watu, anapendwa, anaogopwa na mafisadi, anasimamia hoja zake, ana uthubutu NDIO YUKO HIVYO, nyakati zile unaendesha ujambazi arusha yeye alikuwa anasoma degree, anaendesha siasa chuo kiku...hajaanza leo....certainly ndani ya chadema watu wa caliber ya zitto hamna na wengine mmewaua au kuwafukuza

Zitto ni bright, tough na focused, hategemei siasa wala CDM yenu ambayo kila wakati mmepaka majina yote mabaya...Lema ,zitto angekuwa fisadi au msaliti hao CCM wangeisha muumbua.........hoja za uswis, hesabu za mashirika ya umma, buzwagi, kutaka kumtoa waziri mkuu, kutaja mishahara ya viongozi, na hoja zingine ndio zinazoifanya sio zito tu CHAMA KIZIMA CHA CDM KIONEKANE KINA WATU makini, lakini kuna uozo wa wewe, sugu na mtei ambao akili zenu mnazijua wenyewe

Yesu alisema, ikiwa ufalme utajifitini hautasimama...kamwe

we have plenty of problems IN THIS COUNTRY which need your attention and your solutions…. wewe UNAONGELEA WASALITI NDANI YA CHAMA??? Hao wasaliti umewajua lini?? wanaogopwa nini mpaka leo hii wasitolewe??

Hivi lema unajua chadema kinapendwa na hata wasio wanachadema?? fanyeni kitu kuwaaminisha watanzania mnaweza Zitto anafanya hivyo, Lissu anafanya hivyo, hata Slaa alivyokuwa mbunge alifanya hivyo...nyie wengine mnafanya nini??? HATUONI

Leo Lema ukifa utakumbukwa kwa lipi?? kuchukua jiwe na kumponda nalo mwigamba?? kufungwa jela?? kutukana matusi kuwa ile mimba ya Lowassa?? why u guys dont evaluate urself ila MNAOGOPA KIVULI CHA ZITTO?? where is nassari where is msigwa, wabunge woooooooote wa CDM ambaye ana international status, anayeweza kuongea kitu akaeleweka na kukubalika ni Zitto peke yake ndani ya CDM...................yet is your no. 1 enemy

utasema hooo sijataja hilo jina Lema, YOU ARE INFERIOR na ukiwa INFERIOR UTAJIONA UKO CHINI NA UTATAFUTA SUPPORT YA INFERIOR WENZAKO kumtafuta mchawi ni nini??

Kama aliyoyasema Mwigamba juzi ni usaliti, wenye akili tuna majibu………………kama post hii umeituma ukiwa na akili timamu, jiuzulu ubunge mkuu.

Lema, kila kitu kina mwisho wake, endeleeni na haya mnayoyafanya nakutakia maisha marefu ila UTAONA MWISHO WAKE, sio mzuri kwa chama.

Zitto kama hamumtaki amueni muondoeni kwenye NGO yenu, ATAISHI HE IS GRADUATE na anaweza kujisimamia. Lema ukiondolewa hapo kwenye siasa za chadema unazobebwa na wenye ufahamu mdogo na nguvu za akina mbowe, huna pa kwenda na hakuna atakayekuelewa.

Chadema, mliamua kwa pamoja hamtaki Posho ( sitting allowance) mmeanda bungeni Zitto katekeleza mliyoyaamua WENGINE, akiwem o wewe na Mbowe mmeshindwa……..Then ZITTO M'BAYA???????

Watchin u​
 
nimeanza kuamini kuwa ndani ya chadema hakuna uhuru wa kutoa maoni ndo maana wanachama na viongozi wake wanakuja kutolea malalamiko yao jf Lema wewe ndo uliyemwadhibu mwigamba kwa kufanya hivi leo hii na wewe umerudi humu humu kusema yale yale kwa nini haya huyasemi kwenye vikao halali? https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...ma-na-kichaka-cha-vikao-halali-vya-chama.html

mh JF is the place where we dare to talk openly sasa mbona unaficha ficha unaonekana huyu mtu unamjua lakini kwa nini kwa hutaki kumtaja siku zote umekuwa ukijipambanua kuwa wewe ni mtu jasiri na huogopi chochote sasa mbona huyu msaliti hutaki kumtaja moja kwa moja au na wewe siku hizi umekuwa mtu wa Taarabu
 
Huyu mnafiki kwa kuendeleza unafiki wake na kuwaharibia future vijana aliendelea kugawa ruzuku kama ifuatavyo:

Tarehe 26/3/2012 saa 11:12 asubuhi, MNAFIKI kupitia namba yake ya simu +2557568..53. aliwatumia shilingi 150,000/= wafuasi wa kundi lake, Juliana +255756.5..73, Habi+255.6217.6.., Mtela +2557.5..89.7, Burton +25571..167.., Eddo +25575..49..3, Grey +255755.2..0., Deo +2556.50..60., Adam +2557..137..1, Exaud Mamuya +2557671606.., Ben Saanane +255768078...(CISS),

Baada ya hapo saa 11:43 asubuhi hiyohiyo MNAFIKI kupitia namba yake ya simu +25575.8.9.3. alimtumia shilingi 200,000/= John Shibuda +2557544655..

Mungi mtu uhukumiwa kwa ushahidi usio tia shaka na kama una ushahidi kama huu kwanini usimsaidie kumpa Godbless J Lema aupeleke kwenye vikao vya chama uangaliwe?

Haya mambo anatakiwa kuwaachia watu wengine si kwa hadhi yake.

Niambie tofauti ya mwigamba na lema.

Mungi kwa hili tuseme hapana kwa kwa lema.
 
Last edited by a moderator:
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom