Huyo msaliti ni nani? Vp umeshndwa kuongea hayo kwenye vikao vya chama unakuja hapa hadharani.
Wewe una mentality ya ajabu na ya kimaskini. Yani unategemea kikao kikae kujadili ujinga? Hii ndo maana CCM ipo jinsi ilivyo kwa sababu wao wanategemea sana mwenyekiti wao kumaliza matatizo kwenye vikao vyao. Hata ujangiri ambao unafanywa na viongozi wengi wa CCM, wanasubiri kutajana majina mbele ya mwenyekiti. Matokeo yake ni jinsi unavyoona chama chao kilivyo. Wote wezi. Sasa sijui mwenyekiti atamkaripia nani.
Chadema ni nguvu ya umma, sio mwenyekiti. Hivyo lazima mimi na wewe tuwe na sauti. Hatuwezi kusubiri serikali kuja kuosha vyombo vichafu ndani ya chama. Tutaviosha wenyewe.
Nina wasi wasi na njia inayotumika kuwaondoa wasaliti. Hivi Mh. Lema, tukiwaacha wao wenyewe wakajimaliza? After all wao ni kama tone la maji baharini. Hawana effect yoyote.
Kumbuka hata Mandela wakati wa ukombozi, mzungu alitumia watu weusi kumkatisha tamaa. Wengine kumsaliti kiasi cha kutembea na mke wake wakidhani atakata tamaa. Lakini walishindwa kujua kwamba maovu yalofanywa na wazungu ni mabaya zaidi ya usaliti walokuwa wakipandikiza.
Nchini Marekani, Martin Kingi naye alitumiwa timu ya wasaliti. Walokuja na mtazamo wa kumpinga na kuona anachotafuta, yaani usawa, ni njia ndefu na haitawezekana. Walimchosha mpaka dakika za mwisho alitaka kwenda Africa.
Wasaliti wa Chadema sponsor wao mkuu ni CCM. Wanatumia umaskini wa mtanzania, njaa na tamaa zao hili kupunguza kimbunga kinacjokuja 2015. Hivi si CCM ni chama? Kwa nini Zitto na Shibuda msihamie huko moja kwa moja, mnaogopa nini? Wanaowatuma (CCM) wanasahau kwamba dhambi walofanya kwenye taifa letu ni kubwa sana kuliko vituko tafrani mnayotaka kuleta ndani ya chama. Hapa namaanisha ni bora watanzania waangalie pambano la ngumi kati ya mwenyekiti wa Chadema Arusha na Mbowe, Lema au yeyote ambalo litaisha siku moja kuliko kukaa kwenye umaskini, ujangiri, wizi na mikataba mibovu vinavyoua taifa letu kabisa. Hata nyie mkipewa kuchagua najua mtachagua ngumi. Tatizo lenu ni umaskini. Mmevaa ngozi tu ya kondoo lakini sio kondoo. Mnavaa magwanda lakini ndani mna mawazo yenu binafsi. Chadema ikishinda lolote, mnashangilia ila mission yenu ni kubomoa chama hili mwende vyama vyenu vingine, mjiite wenyeviti (hii ndo shida ya Zitto, yaani kuitwa mwenyekiti).
Pendekezo;
Hawa watu tuwaache wajimalize wenyewe. Siku zote ukitaka kumtafuta kichaa kwenye mkusanyiko wowote, mpe microphone. Hivyo hivyo tuwape microphone hawa watu. Waache wafanye interview na magazeti, TV na waje kwenye mikutano...wapeni microphone.
Akiwa na microphone, Zitto amejiua yeye mwenyewe kuliko anavyotaka kukifanyia chama. Oh, sitagombea tena...ntaenda Somalia kufundisha, mara Sudan kusini...oh, umaskini wa watu wa Tabora umenifanya nigombee tena....hii misimamo, hata mke huwezi kukaa naye. Sijui private life yake lakini kwa undumila kuwili huu, naweza kusema huyu mtu hajaoa. Kama ameoa, anao wengi au ndoa yake ipo kitanzini.
Sasa huyu ndo anataka kupewa uenyekiti kwenye chama? Come on Zitto! Si utakiuza? Kiongozi bora ni mwenye msimamo. Anaongea neno and he mean it. Sio kubadirisha rangi kama kinyonga.
Tuwaache hawa watu wajimalize. Tusije tukawapa sababu ya kujustify usaliti wao. Mpaka sasa hivi, sababu yao ni njaa na tamaa. Tusiwaongezee sababu nyingine.
Mtu kama Zitto anajiona akiwa kiongozi wa chama, anaweza kuwa Rais. Jaribu uone Mr. Zitto. Hapo ndo utaona thamani yako kwa taifa. Sivyo unavyodhania.
Tukiamua kupambana nao jino kwa jino, nashauri hiyo kazi waifanye vijana wadogo. Sio Mbunge au mwenyekiti wala katibu. Waachie hii kazi vijana, tena wadogo tu kwa sababu akiri za hawa watu ni ndogo, hivyo ipambanishe na akiri ndogo. Zoezi hilo lisichukue muda mrefu.
Mwisho, nina wasi wasi huyu Zitto aishaanza kutumiwa na mtarajiwa wa CCM 2015. Hizi safari za Uswiz zisizoleta habari yoyote, ziangalieni kwa makini. Juzi tuliambiwa Mh. Mbowe ana nyumba Dubai. Hivi ni watanzania wangapi wenye nyumba nje ya nchi? Mwenyekiti wa CCM mbona ana nyumba nne Marekani? Hii inawezekana ni part of the game plan ya Zitto. Kuweni makini naye na achana naye. His worth is nothing.