Usaliti na Unafiki unavyoangamiza Taifa - Lema

Usaliti na Unafiki unavyoangamiza Taifa - Lema

Status
Not open for further replies.
Wameamua kuja huku mitandaoni kwa kujua wanachokifanya mkuu, wasilolijua tu ni namna wanavyochimbia kaburi lao kwa namna yapekee kabisa. Mihemuko inaanza kuongoza watu na wao wanaongoza watu wengine.
Naandaa makala ambayo nitaimwaga hapa hapa ukumbini!

Yaani mkuu, kila nikilisoma hilo bandiko la Mheshimiwa Lema natamani kuhisi kuwa labda ID yake hapa JF imekuwa hijacked lakini yaelekea ni yeye mwenyewe. Sadly, baadhi ya viongozi/wanaharakati wa Chadema (nimewaona kama wawili hivi kwenye bandiko hili) wanaonekana kushabikia uamuzi huu usio na manufaa kwa Chma chao Hofu yangu si kusambaratika kwa Chadema kwani hata kwenye Biblia tunafundishwa kuwa "Kila mtu atabeba mzigo wake mwenyewe na "acheni wafu wazike wafu wenzao." Kinachonitatiza ni kuona chama ambacho angalau kilianza kuonekana kama mbadala wa keli didi ya CCM kikiingia kwenye utoto mbaya zaidi ya tunaoushuhudia huko CCM.

Kwa hakika inasikitisha sana
 
Lema acha utoto.
Chama hakijengwi kwa style hiyo. Nakusihi usilete hiyo thread hapa. Acha
tafadhali

hakuna kuacha kitu! Lema tafadhali leta hiyo mada, na usipoleta tunakusurubu wewe lema, maana wewe ndio utakuwa mnafiki.!
 
Huyo msaliti ni nani? Vp umeshndwa kuongea hayo kwenye vikao vya chama unakuja hapa hadharani.[/
Msaliti hatajiki kwa sasa,ni sawa na kumuambia Mh.Zitto atutajie majina ya walioficha fedha zetu Uswisi japo aliahidi mwenyewe kuwataja,ni ngumu kumesa hiyo.Wanasiasa wetu uchwara mtupu.Sasa hivi nd'o kwanza pesa zetu zishageuka deal kwa wengine hutaji majina ya watu 12 wanaohujumu uchumi wa watu zaidi ya milioni 45,huu ni wenda wazimu wa viwango vya vya juu japo in secret wanajifanya wajanja kugeuza ufisadi huu sehemu ya kupatia umaarufu na migao ya pesa chafu hizi.Hii haitofautiani sana na Lema kutomtaja huyo msaliti kiongozi.
 
lema anaungwa mkono na Wauni Zito anaungwa mkono na watu wenye busara
 
Last edited by a moderator:
post zako zinaonesha hofu na 'mahaba' uliyo nayo kwa zitto ingawa unajitahd kuficha! na hicho ndicho wengi kinatupa shaka iweje adui ampende 'askari' wetu kiasi hiki??
Hizo ni fikra zako humjui Ritz
 
Last edited by a moderator:
Lakini umeelewa ? Lema hajawahi kusema anataka Urais wala Uenyekiti kwa hiyo hapa hakuna Ugomvi wa masilahi isipokuwa unafiki vs ukweli , tusubiri kesho


Lema anamsaidia mchaga mwenzake ( Mbowe).

Zitto ni jeshi la mtu mmoja.
 
lema anaungwa mkono na Wauni Zito anaungwa mkono na watu wenye busara


Zitto anafanya phd wakati Lema anapaswa kurudia kidato cha nne.

Zitto anafikiri kuwa muhadhiri wakati Lema anawaza siasa za kibabe mitandaoni.

Zitto anapinga Posho wakati Lema anashauri Posho iongozwe.

Zitto anajitambua wakati Lema hajitambui.
 
Last edited by a moderator:
Exceedingly saddened to witness competing factions within Chadema rushing to press a 'self-destruct' button. CCM must be busy preparing a massive party (can't really blame them, can we?)
 
Nimefuatilia mjadala sana leo ukizingatia ilikuwa ni Jumamosi kwamba hatukuwa na kazi nyingi sana za Kibunge hasa baada ya kuanzisha mjadala unaosema " Usaliti na Unafiki unavyoliangamiza Taifa " na nimeona mjadala na nimejifunza mambo mengi sana sikumtaja Mtu ila Watu wengi wametaja majina ya Watu , sijui kwanini ? ila naendelea kutafakari , kesho nitaandika kuhusu mada inasema " UNAFIKI WA ZITTO KUHUSU POSHO " na mpaka saa nane mchana nitakuwa nimewasilisha na jambo hili halina mgogoro na kanuni za Chama kwani ni jambo liko wazi kwenye vyombo vya habari .

Asanteni

Unadhani ukifanya hivo utakuwa unamwangusha zitto? Unakata mti ulioukia? Unategemea nini mh Lema.

Mtazamo wangu:
Tangia PAC ikiumbue Chama Chama chama chenu juu ya matumizi mabaya ya Ruzuku basi mmehamishia mashambulizi kwa mwenyekiti wa kamati mh zitto.Hii haitasaidia hata kidogo isipokuwa itakushushia heshima ww mwenyewe kma mbunge na mAtOkeo Yake utayAona baada ya post yako Hiyo kesho uliyoahidi.

Kwa taarifa, tunatambua namna ambavo ww na kundi lako mnamchukia zitto lkn unasahau Kuwa boss wako mbowe linapokuja suala la zitto Yuko mguu mmoja ndan mwingine nje kwa hyo Kuwa makin sanA.zitto atakuaibisha nakwambia hyo maana mbowe anatambua mchango wake sio km ww unAyekuja kumshitaki boss wako kwenye jf
 
Nilichogundua lema anatumika kumshambulia Zitto ili,Zito apaniki aondoke Chadema,ili wawe huru kuwalubuni watanzania,Zito Zito Zito usiondoke Chadema wewe ndo mlinzi wa watanzania wanyonge na wale tunaotaka mabadiliko,ukiondoka Chama cha CDM kitakuwa Saccos,Usiondoke wanakubuguzi kwa Malengo yao,Je zito akileta mada JF kumtuhumu Dr Slaa au Mbowe,Lisu je viongozi wakuu wa CDM wataelewa
 
Last edited by a moderator:
Nilichogundua lema anatumika kumshambulia Zitto ili,Zito apaniki aondoke Chadema,ili wawe huru kuwalubuni watanzania,Zito Zito Zito usiondoke Chadema wewe ndo mlinzi wa watanzania wanyonge na wale tunaotaka mabadiliko,ukiondoka Chama cha CDM kitakuwa Saccos,Usiondoke wanakubuguzi kwa Malengo yao,Je zito akileta mada JF kumtuhumu Dr Slaa au Mbowe,Lisu je viongozi wakuu wa CDM wataelewa

tunaongelea unafiki dada
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom