Usaliti na Unafiki unavyoangamiza Taifa - Lema

Usaliti na Unafiki unavyoangamiza Taifa - Lema

Status
Not open for further replies.
Kijana, naamini wewe umenifahamu katika mjadala wangu na Mohamed Said,


Soma hii niliandika huko nyuma kabisa,

Na nimuumini wa chadema pekee niliyeeleza uzandiki na ufedhuri wa Zitto hadharani, nashukuru sasa watu wamenielewa,

Ni nyinyi tu wa ccm ndio mnajitoa ufahamu,

Haya pambazuka hapa:




September 2011

Share this:

Like this:

3 Comments

Kazi ya kuihujumu Chadema aliyotumwa Zitto Kabwe inapokuwa nzito kwake.

Binafsi naitafakari kauli ya Zitto Zuberi Kabwe na ninafurahi kuona kuwa kile nilichoonya kuwa kijana mwenzangu anatumiwa vibaya na ccm sasa kimetimia.

Wakati akihojiwa katika kipindi kiitwacho, Exclusive interview na Millard Ayo cha Clouds FM Amesema hivi nanukuu “Wazee wetu walitusaidia kutupatia maendeleo ya kisiasa, sasa ni jukumu letu kuleta maendeleo ya kiuchumi. Ila naomba nisisitize, jukumu hili haliwezi kutekelezwa na mtu yeyote aliyezaliwa kabla ya uhuru, na ninatangaza kuwa nitagombea urais mwaka 2015″

Naunga mkono kwamba vijana tujitokeze kuleta maendeleo kwa taifa letu, lakini napingana vikali kauli “jukumu hili haliwezi kutekelezwa na mtu yeyote aliyezaliwa kabla ya uhuru”

Kwanza mimi nasema amewatukana wazee wote Tanzania, huku ni kukosa busara heshima na hana sifa ya Uongozi kwani ni mbaguzi. Wapo Wazee waliozaliwa kabla ya uhuru na wanailetea Tanzania maendeleo na wapo wapuuzi waliozaliwa baada ya uhuru ni wapuuzi wa kutisha yeye akiwemo. Zitto hana busara kwa hili

Amejisemea bila kufikiri. Ana maanisha hata kama mtu ni msomi kama akina Dr Slaa, Dr Gharibu Bilali mtaalamu wa nyuklia na Prof Lipumba hawawezi kusaidia isipokuwa wale waliozaliwa baada ya uhuru? Huu ni uhuni wa kawaida wa Zitto ambaye hujitahidi kujionyesha kama thinker wakati siyo hasa ikizingatiwa hata akiwa shule alipita hivyo hivyo.

Nadhani kwa thinker mzuri hana haja ya kuwatenga watu kwa umri wao bali tabia zao hasa linapokuja suala zima la ujenzi wa taifa. Mbona tuna vijana waliozaliwa baada ya uhuru kama yeye mwenyewe Zitto na wengine lakini bado ni mafisadi???

Kitendo cha kutangaza nia ya kugombea urais 2015 sio kibaya kwakuwa ni haki yake kikatiba, lakini kutangaza nje ya ya utaratibu wa chama chake huu ni uhaini kwa chama. Zitto anajua anachokifanya, na anajua matokeo yake lakini ni jambo la kusikitisha kuwa hajui madhara yake kwake.

Katika tafakuri yangu kwa mapana ya nera, nikamkumbuka mwalimu wangu pale Moscow Urusi, Prof Radav Metbarg aliyenifundisha uhandis wa umeme, huyu alinidokeza aina ya binadamu, hakika ilikuwa muhimu sana ndio maana leo imenijia akilini nikalazimika kuzama kimang’amuzi zaidi, nimefanya hivyo ili nimtambue huyu mtu aitwae Zitto Kabwe kiundani zaidi, Katika aina za binadamu Zitto ni wa aina ya Sanguine, hii ni kwamujibu wa tabia zake za kisiasa. Hakika naamini watu wa aina hii ni hatari hasa ukiwasogeza jirani na uongozi popote pale basi wanaouwezo na msukumo mkubwa wa kukupindua. Hiyo ni sehemu ya sifa ya watu wa aina hiyo na kwa ujumla ni waroho wa madaraka.

Lakini najiuliza kwani Magharibi mwa Tanzani ndiko aina hii ya watu inapatikana kweli au yeye ni chipuzi tu? Nikiangalia wenye tabia zake nawaona kama Kafulia, Mkosamali na Shibuda. Lakini sitaki kujikita katika dhana hiyo ya ukanda bali nasimamia kuwa hao ni chipuzi la aina hiyo ya tabia za binadamu ambao ni hatari hasa uwasogezapo katika vyeo vya juu basi huutaka ufalme hata kwa njia ya uasi tu. Muono wangu ni kuwa Zitto hautaki urais na anajua fika kuwa kwa mujibu wa katiba iliyopo yeye hastahili kugombea URAIS, ila kwa gharama kubwa amejichimbia msituni kukihujumu chama chake kilichomlea na kumfanya leo ajione fahali la masika.

Ninarudia tena Zitto hana nia ya urais, nasema hana hata chembe za kuutaka urais ila analengo moja tu nalo nikukivuruga Chama chake tu. Mwili wa Zitto upo Chadema ila moyo wake upo ccm palipo panono, kweli pesa mwanaharamu.

Lakini wadadisi wa siasa za Afrika tunapaswa kulaumiwa sana, tulipopokea mageuzi ya siasa za kidemokrasia na kuziacha siasa zetu za kiimla lakini tulishindwa kupokea hata miundo ya siasa hizo, mathalani vyama vya siasa vyenye ukwasi wa kidemokrasia huwa na utaratibu wa kutengeneza viongozi wa chama, kitaifa na viongozi wa kimataifa. Hili nadhani hata Hayati Mzee Nyerere alifanikiwa kuliasisi lakini baada ya kufariki mabaka demokrasia wamebaka na kubuni mifumo ya kuzalisha watawala sio kuzalisha viongozi tena.

Hili lisiwe turufu kwa Zitto, naamini anatambua njia aipitayo na madhaifu ya muundo huu wa vyama vyetu vya siasa. Ningefurahi na ninaamini wadadisi wote wa siasa za Afrika wangefurahi pia kama Zitto angeanzisha harakati za kuboresha muundo wa vyama vyetu vya siasa hususani Chama chake cha Chadema kilichobeba tumaini kuu la wazalendo na wengi wa nchi hii. Je ccm ya leo bado inautaratibu wa kuandaa vijana kwaajili ya siasa za kesho? kwaajili ya urais? kwaajili ya wanadiplomasia wa kimataifa wakesho? Chadema je? UDP je? NCCR je?

Jambo la kumshukuru Mungu nikuwa Chadema wanajua kila anachokifikiria kufanya, anachokifanya, anakolalia, anakoamkia, anakokutania na wafadhiri wa uasi huu na kila kitu. Kwaujumla chama kinamjua utosi hadi unyayo.

Chadema wamekuwa wakipigana vita mbili kwa mda mrefu, vita hiyo ni ya nje (ccm) na ndani (Zitto, Shibuda na mamluki wengine) lakini mda wote chadema imeshinda na itashinda na itaendelea kushinda daima kwakuwa ni vita kati ya wema na ubaya kumbuka na elewa kuwa kwenye wema Mungu yupo.

Ninachoamini katika siasa duniani ni kuwa hakuna aliyejuu ya chama chake

Sawa bwana leo umeamua eehhh Ben jina la Zitto analiogopa mshauri na yeye aweke mambo hadharani.
 
Karibu sana Comrede.
kwanza nikupongeze kwa kutokuwa mnafiki wa kufanya mambo kwa kificho, ni lazima umma ujue unafiki wa watu wanaojiita wazalendo huku waki wazandiki na ambao wapo tayari kufanya jambo lolote lile ili majina yao yaendelee kubaki huku wakiangamiza taasisi

Hata mimi hivi karibuni nitakuja Naunafiki wa Zitto na uwepo wangu Magereza na kesi yangu ya ugaidi.

kilewo, mnaifanya CHADEMA kuwa cheap sana. Mnaishusha kwa kasi sana, vita vya wenyewe kwa wenyewe. Naona kuna wanachadema wana free entrance access to Uongozi wa juu na wengine wana restricted access.
 
salaam wana jf.
amma baada ya salam
ningependa nitangulize
maneno ya mw.NYERERE.
nukuu "dhambi ya ubaguzi haifi
ni sawa na kula nyama ya mtu" mwisho wa kunukuu.
tunayoyaona leo ndani ya
chadema ni mazao yalio chipua
baada ya shutuma na tuhuma
juu ya ubaguzi uliokuwa
ukilalamikiwa kwa muda mrefu.
leo ndani ya chadema chama
kilichojipa sifa ya umakini
kumekuwa na sisi chadema wao
wasaliti.
binafsi sioni usaliti balinaona umimi na uwao
alioutaja mw.nyerere kama
mwanafalsafa.
ikiwa dhambi hii itadumishwa
imma katika misingi ya
udini,ukanda,ukabila au ukoo basi baharia mkombozi atazama
yeye.
nikirudi nyuma kidogo
nakumbuka viwanja vya
furahisha mwanza mbowe alipo
wauliza watu mbele ya vyombo vya habari kuwa
wangapi wanataka tz iwe kama
libya (wakati huo mauwaji
libya yalikuwa yamepamba
moto).kisha narudi leo hali
inavyowasuta. aibu tupu kiongozi mmoja
kuwaita wengine ni wasaliti
na sisi tunauliza maadili ya
chama katika hili yako wapi?.
sisi na wao ni hatua ya kwanza
ya ubaguzi na dhambi hii haita kufa.
 
Ni usongo tu walionao kwa Zitto. Kawashinda kwa kila kitu, uelewa, uana siasa, kupendwa na watu.

Mimi nawaambia wamfukuze Zitto chadema kama wanao ubavu.


Wawache porojo za JF, eti wana siasa wanaendesha chama kupitia JF. Hii mijitu ya ajabu sana.
 
Mmh Nakumbuka mwaka Jana miezi kama wakati wa masalia. Sie ngoja tuandae Popcorn za kesho... Mambo hadharani.
 
Kwi kwi kwi kwi lol!!!! Hizi ni dalili za kukosa hoja yenye nguvu. Kama huna cha maana cha kuandika kaa kimya.

Nimekubali Zitto

wanamuogopa Chadema wote wamekuja kulia lia JF swali la kujiuliza nani atakaweza kumfukuza.
 
Sasa kulikuwa na haja gani kuandika haya si ungesubiri kesho.

mbona umepanic mkuu? Hiki ndicho kinachotufanya hata sisi wananchi wa kawaida tumtilie mashaka zitto! Kwanini zitto akiguswa lazima ccm muinuke na kumtetea kwa "gharama yoyote ile"!
 
hivi ndo wewe mkeo alikuja hapa na kukufanansha na mwalimu nyerere? Unataka kujitaftia umaarufu kupitia zitto wakati hata kimara hujulikani! Tunawasubiri kesho ila msikimbie kama leo

Kwani leo Zitto alitajwa na Lema ?
 
kilewo, mnaifanya chadema kuwa cheap sana. Mnaishusha kwa kasi sana, vita vya wenyewe kwa wenyewe. Naona kuna wanachadema wana free entrance access to Uongozi wa juu na wengine wana restricted access.

Wote sawa ila mnafiki ni kiumbe hatari sana, ukweli ukisimama ulo hujitenga tuache ukweli usimame.
 
Last edited by a moderator:
Liwalo na liwe, Zitto amekuwa na jeshi lake, na amekuwa na ID nyingi sana humu jf tunazifaham..angalia thred ya Lema mchana utaziona. Tumalizane hapahapa jf ili tukishindana yeye aende zake nasi tubaki na chama, amefanya dhuruma na kutuhujum vya kutosha, mara aende na Mwigulu RFA...too much

Na wanaompiga Lema kuyaanika hapa ni masalia ndani ya chadema na mambulula kutoka ccm

Tuta wafundisha siasa za haki na ukweli zisizokuwa na unafiki...
 
Nimefuatilia mjadala sana leo ukizingatia ilikuwa ni Jumamosi kwamba hatukuwa na kazi nyingi sana za Kibunge hasa baada ya kuanzisha mjadala unaosema " Usaliti na Unafiki unavyoliangamiza Taifa " na nimeona mjadala na nimejifunza mambo mengi sana sikumtaja Mtu ila Watu wengi wametaja majina ya Watu , sijui kwanini ? ila naendelea kutafakari , kesho nitaandika kuhusu mada inasema " UNAFIKI WA ZITTO KUHUSU POSHO " na mpaka saa nane mchana nitakuwa nimewasilisha na jambo hili halina mgogoro na kanuni za Chama kwani ni jambo liko wazi kwenye vyombo vya habari .

Asanteni
mhhhhhhhhhhh kwa style hiii napata na kushikwa na mashaka why mgombanie fito wakati wote mwajenga nyumba 1?

hapa kuna kitu kimejificha idadi ya member jf ni ndogo sana ukilinganisha na wananchi wanaokuunga mkono na kukusaport.
lkn idadi hiyo hiyo ya jf ni kubwa sana zaidi ya wananchi waliopo woteee wa vyama vya upinzani.humu ndimo magazeti wanamochukua habari na kuziandika kwenye magazeti yao ambayo husomwa na kusambaa nchi nzima tena mpaka nje ya nchi hivyo ndugu kuwa makini sana na chunga hilo domo lako .
kwataarifa yako unayotaka kuyafanya na mnayoendelea kuyafanya hakika ni mambo ya kupanga na yanawapa ushindi wapinzani wenu ccm kwani mipango na malengo yao yanakamilika kiulaini before 2015.
naona mmeruka vihunzi vyooote lakini hichi cha kubwekeana wenyewe kwa wenyewe kinawatafuna bila kujijua.

acha kuropoka mitandaoni mkuu? utapoteza uelekeo kama saa mbovu
 
Karibu sana Comrede.
kwanza nikupongeze kwa kutokuwa mnafiki wa kufanya mambo kwa kificho, ni lazima umma ujue unafiki wa watu wanaojiita wazalendo huku waki wazandiki na ambao wapo tayari kufanya jambo lolote lile ili majina yao yaendelee kubaki huku wakiangamiza taasisi

Hata mimi hivi karibuni nitakuja Naunafiki wa Zitto na uwepo wangu Magereza na kesi yangu ya ugaidi.

Naona hii ni operesheni maalum
 
...


.....Ni Gwaride la utambuzi wa makamanda WAAMINIFU watakao peleka maangamizi ccm 2014 - 2015!!!!

kabisa mkuu! Mwaka huu lazima tujue true colours za huyu jamaa, ametuzuga mda mrefu sana, ametulaghai mda mrefu sana, ametuhujumu sana
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom