Usaliti na Unafiki unavyoangamiza Taifa - Lema

Usaliti na Unafiki unavyoangamiza Taifa - Lema

Status
Not open for further replies.
Safari yetu ya kubadilisha utawala inaonekana kufika ukingoni na nifuraha ya kila Mtu mwenye hisia ya ukweli katika maisha na ninapotazama mbali sana ninaona jinsi ambavyo Usaliti na Unafiki unavyoangamiza Taifa ni bahati mbaya sana uwezi kuwaepuka katika harakati hizi lakini tukiwa makini tunaweza kuwathibiti .

Kama Chadema leo itashindwa kuwachukulia hatua wasaliti wa wazi wa kazi hii njema ni vipi Chadema itaweza kuitaka Serikali na Rais iwajibishe Viongozi wake katika ufisadi na wizi wa mamilioni ? Na Wananchi lazima wajue lengo kubwa na muhimu la Chadema kwanza liwe kubadilisha fikra na mitazamo na kuupa UMMA elimu na mamlaka na nguvu ya kusimamia Taifa lao katika kuhoji ,kudadisi na kukemea , kwani UMMA usipojua wajibu wake katika kusimamia rasilimali na Taifa lao , ukweli utabaki kuwa Nchi itabadilishwa na kufanikishwa na Jamii iliyoamua kuishi matendo dhahiri ya ukweli na haki na sio unafiki na usaliti .

Viongozi wote wa Siasa wanatokana na Jamii kwa hiyo jamii Thabiti inayo furahia UTU ni Nchi bora tutakayoijenga lakini Jamii yenye woga na hofu na Sifa itazaa Taifa lenye usaliti na Wanafiki . Usaliti na Unafiki unaliangamiza Taifa sana . Maombi na Dua za Watu wengi kuelekea 2015ni kutaka kuona Chadema inachukua Nchi , lakini Dua na Sala hizi zina Imani kubwa na Viongozi wa Chadema na sio rangi ya Chadema , hivyo ni muhimu Chadema kuchukua hatua sasa ya kusafisha Chama na kama hatua hiyo muhimu ya kuondoa Watu wenye rangi mbili italeta madhara katika Uchaguzi Mkuu wa 2015 kwamba tunaweza tusishinde dola basi madhara hayo ni muhimu kwani lengo letu lisiwe tu kwenda Ikulu bali kubadilisha fikra ya utawala katika kutenda na kuamua .

“ Ni bora Simba wakali mia moja walioko Nje kuliko nyoka mdogo mmoja aliye ndani “ Chadema lazima ifanye maamuzi sasa ya kusafisha Nyumba yake la sivyo itakuja kujuta katika siku za mwisho , wasaliti wote waondolewe hasa yule Kiongozi wao kwani hakuna genge la usaliti lisilokuwa na Kiongozi , kuna Watu wengi Vijana wamekuwa wahanga na ndoto zao kupotea katika Siasa kwa sababu waliongozwa vibaya na Kiongozi mkubwa anayeratibu usaliti ndani ya Chama .

Mtu huyu wote tunamjua ni matumaini yangu Usaliti wake sasa utafika kikomo kama Chama kitaamua kuwa na busara za kutosha katika kujenga siku njema zinazokuja . Mtu huyu amefanya mambo mengi mabaya katika Chama yanayohusu usaliti na amewaponza Vijana wengi na kuangamiza ndoto zao kwa sababu ya mambo yake binafsi .

“ To me, the thing that is worse than death is betrayal. You see, I could conceive death, but I could not conceive betrayal.” Malcolm X


Lema Godbless - Mp

1. Kumbe hampo makini?
2. Sasa kinaishinda nini?
3. Hivyo ni kichafu?
4. Ukubwa umewazidi nguvu?
5. Imani bila matendo?
6. Busara hazitoshi chamani?
7. Chama kinakaribia kufa?
 
Chadema yakumbwa na mgogoro mkubwa chama kinakatika vipande vipande.
 
Obama Katika Kitabu chake kimoja alisema ...... Kiongozi wa kweli na sahii ni yule anayechukua hatua hata kama hatua haziwafurahishi wananchi , kuna kitu kinapikwa hapa lakini najua kabisa CDM kuna msaliti nandiye amekuwa mfano mbaya na muharibifu , ... Mpaka Lema ameamua kusema hivi pengine Mbowe amekuwa mpole sana kwa huyo msaliti
 
Mkuu Lema kila mtu anafahamu juhudi zako za kuwapigania wanyonge kwa kupitia katika chama au kwa njia maandiko matakatifu. Nasema asante kwa yote ambayo umefanya na unaendelea kuyafanya.
Ombi langu kwanza ninaomba unijibu katika huu mtandao kwa hli tafadhari!
Swala la usaliti na unafiki ktk mapambano yoyote yenye kutaka kuwakomboa wanyonge linaweza kulinganishwa na njia mojowapo itumiwayo na adui anaye taka mapambano yasifanikiwe: Hivyo ninaomba tena tafadhari kama hali imefika hapo hakuna short cut bali ni kuitisha kikao chenye maumuzi ya mwisho ktk CDM ili kitoe uamuzi wa hili tatizo. Wapenda CDM labda na wanachama hawataki haya mambo ktk mitandao hat kidogo kabisa. Tafadhari fanya emergency kikao ili mkazungumze halafu mje na lugha moja kwenye huu mtandao. Tafadhari tumia busura na umakini wa CDM!!!!!!!!!
 
Jamani maCDM wenzangu, sasa nashindwa kumuelewa nani haswa ni msaliti ndani ya chama, i wouldnt expect this would come from someone like Lema, jamaani, hivi kila mtu anataka kukisaliti chama! Ni hela au utashi?
 
Kwa CCM ukweli na ujasiri=Uchochezi.

Chadema ukiwa mkweli na jasiri eti Wewe ni Msaliti.

Siasa za sasa hakuna kuabudiana wala msijifanye miungu watu..eti Mtu akisimamia ukweli na kuhoji mnamuita Msaliti.


kwa style hii ya Uroho wa madaraka na kutaka kuhodhi kila kitu..CCM itaendelea kuwaburuza.

Chadema imeanza kujipunguzia nguvu na kukubalika...hadi 2015 chadema itashiriki uchaguzi ilimradi wamesimamisha mgombea ila ushindi bado ni ndoto ya mchana.

eti Lema anaongea usaliti wakati Mwenyewe amesaliti wananchi juzi tu. kwa tamaa za pesa.

Halafu Kamanda acha woga wa kitoto kwani CDM nayo CCM hakuna wa kumfunga paka kengele?
 
Chadema ni wajanja sana hapa katika hili andiko hajatajwa mtu isipokuwa watu katika uchangiaji unaona kabisa wanajua tatizo lipo na yawezekana ni ZZk
 
Jamani maCDM wenzangu, sasa nashindwa kumuelewa nani haswa ni msaliti ndani ya chama, i wouldnt expect this would come from someone like Lema, jamaani, hivi kila mtu anataka kukisaliti chama! Ni hela au utashi?

Mkuu huhitaji eli ya juu sana kujua nani msariti ndani ya chama cetuu na tumemvumilia sana...
 
Ngoma ikivuma saaana mwisho hupasuka! CDM maji yanayoifanya meli kuelea ndio hayo hayo huizamisha! Words are enough for the wise!
 
Godbless J Lema,
Mimi nakukubali katika harakati za ukombozi wa taifa hili. Lakini naomba kukushauri kitu kimoja: Katika siasa kubali kutofautiana na watu fikra. Na sio kila mara unaotofautiana nao fikra basi ni maadui zako. Ni wazi kabisa kwamba Mwenyekiti wetu Mbowe angesema nawachukulia kama maadui wale wote anaotofautiana nao kifikra, CHADEMA isingekuwa hapo ilipo.

Kila shilingi ina pande mbili. Sio sahihi kumjudge mtu kwa kuangalia weakness zake peke yake. Naamini CHADEMA imefika hapo ilipo kwa juhudi kubwa za viongozi wake WOTE na wanachama wake. Na ninaposema wote nina maana ya WOTE. Sio vyema mtu mmoja au kikundi cha watu kujiona kuwa wao ni bora zaidi ya wengine. Kila mtu anayo madhaifu yake kama alivyo na mazuri yake. Hakuna mtu aliyekamilika, sio CDM, sio CCM na sio popote.

Wanasema mbwa ukishamjua jina hakusumbui Lema.... Tafakari braza...

siasa, kazi kwelikweli!
 
Last edited by a moderator:
Magazeti ya kesho Chadema vipande viwili. Mgogoro waikumba Chadema, vita kati ya Lema na Zitto.

Nimefurahi sana kuona hii bifu ya Chadema.

teh teh teh
If wishew were horses......
For god's sake please you stop this...munavuana nguo na kukiaibisha chama tegemeo la ukombozi halisi sisi watanganyika wa hali ya kati na chini...jamani imetosha. Mwenye namba ya mbowe ampigie amwambie vijana wake huku wanakivua.chama.nguoo awakataze maramoja wao na wapambe wao coz hata wakifika 2015 watakuwa hawafai tena kusafishika uchafu wao.
Wamevuana wapi nguo hadharani?Yaani statement ya Lema imewavua wasaliti nguo,unawahurumia?Hata Mwenyekiti alionya juu ya usaliti,katibu Mkuu alisema chama kimebaini mbinu za kuuvuruga uchaguzi wa ndani wa chama kwa kupandikiza mamluki.Ni bora wajue kuwa wameshabainika sasa.
this time zito kabwe asipofukuzwa chadema hatoondoka milele na kwa mtazamo wangu binafsi tusibiri DAMAGE kubwa chadema maana naona imekuwa mbaya sana...
kuna vitu viwili na vitizama
CHAUMA kupata nguvu..2014 TREND hii ikiendelea
kupoteza wanachama wengi hasa vijana ...
chukueni hatua mapema
CHAUMMA kimeshajifia.Makakati wowote wa kukihujumu CHADEMA hautafanikiwa.CHADEMA ni taasisi yenye watu wengi wenye uwezo.Lema hajataja watu ila kataja sifa na mipango ya wasaliti na kutoa angalizo

Nadhani Lema hakumtaja Zitto. Ila kwa sababu umemtaja, basi ngoja tumuongelee. Wewe ukimtizama unaona shujaa, right? Mimi naona msaliti, ndumila kuwili, mtu asiye na msimamo na ana uchu na madaraka. Pia nadhani ni mjinga. Rejea story zake humu humu JF utafikia conclusion kama yangu. Pengine unaweza kumwona amechanganyikiwa.

International status? Come on...JK anazo nyingi. Hata leo yupo nje. Kama hiyo ni sifa, liko wapi taifa la "international status?" Sijui wewe ila nikipewa nichague kati ya kina Nyerere, viongozi waliokaa nchini mwao na kulijua taifa na wale wanaosafiri kila siku kwa million 300 kila safari, ntachagua kina Nyerere.

Where is Msigwa?, where is Nassari?...wewe una akiri kama ya Zitto. Maana yeye uwasaliti wenzake kwa kujiona aishatembea dunia nzima. Ebu tuangalie akitembea anafanya nini. Niliudhulia mkutano wake miaka ya 2008 au 2004 huko Texas. Maongezi yake ni haya, "naachana na siasa hivyo kipindi kijacho sitagombea." Hivi hii ndo international status? Nakupa challenge, nenda mwamshe Nassari au Msigwa usingizini, muulize kama ataacha kupigania watanzania leo au kesho. Sijui atakujibu nini lakini kati ya hayo majibu, mojawapo litakuwa ni hapana.

Msigwa, Nassari, Lema, na wote ulowataja, they are our heroes. Hawa ni mashujaa. Wamepigwa mabomu karibu kila mkutano, Nassari kapigwa, juzi tu ametoka hospitali. Msigwa huyu jina lake lipo kwenye mswaki wa kamanda wa polisi Iringa. Hawa wakivua mashati yao, miili yao ina vidonda, mioyo yao ina majeraha walopata sababu ya kupigania watanzania, mimi na wewe wakati wewe na shujaa wako mkitafuta "international status" kwa kuwambia watu kwamba hamtawapigania tena. Hii si aibu?

Zitto anajua mabomu yanafananaje? Mwambie ajiunge na Chadema, then atajua ushujaa ni nini.

Nakubaliana na maudhui haya kwa asilimia kubwa
 
Kama na wewe Godbless J Lema humtaji msaliti, na wewe kwangu ni mnafiki tu. Unaposema kila mtu anamjua unamaanisha nini, kama kila mtu anamjua na hamjafanya lolote, basi tatizo ndani ya CHADEMA ni kubwa kuliko hii thread!
 
Last edited by a moderator:
" Umasikini sio Uadilifu " uzalendo wa Mbunge na viongozi hautakuwa na maana kama sifa ya kwanza ya kiongozi itakuwa ni kutamani umasikini nataka kuona Watu wanalipwa vizuri mishahara na maisha yao yanakuwa mazuri , na niseme kujipambabunua kwa kukataa kulipwa posho ya laki kwa siku ni kutafuta umaarufu , kwanini Zitto hakukataa ongezeko na posho ya mshahara iliyoongezwa mwaka jana mwezi wa saba takribani milioni nne , lakini vile vile mbona masisha yake binafsi haya reflect hii tabia mfu anayopigia kelele
 
Hayo ni maneno ya Lema. Historia inaonyesha maneno yake huwa anaongea kujisafisha na kutoa maneno ambayo anahisi ni matamu kwa wajinga wachache ambao wanaweza kuyaamini. Lema ama wewe msipime uwerevu kwa idadi ya watu wakushabikio. Watambuzi wanakwambia ni kheri uwe na followers wachache ambao ni intelligent, kuliko ukawa na followers wengi ambao ni stupid. Ukifanya ujinga mtu anakusifia, ukichemka mtu anakusifia, pale inapokuwa umeweza una sifa za kweli zinastahili huwezi tofautisha.

Matendo na maneno wa wanao msimamia na kuchekelea Lema Upuuzi wake ni kioo cha jinsi Lema alivyo na uongozi wake unasimamia yepi.

Sasa hapo Posho si dhambi sababu ya Uroho wa Pesa? Hizo posho ndogo hajaziona zilivyo ndogo kwa wafanyakazi wa chini wa Serikali? Kwa misingi hiyo maneno yake katika bandiko hilo ni irrelevant kwa namna yeye alivyo kwa rangi zake asili.
Unataka kusema nini maana naona unahara tu..
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom