Usaliti na Unafiki unavyoangamiza Taifa - Lema

Usaliti na Unafiki unavyoangamiza Taifa - Lema

Status
Not open for further replies.
nilitegemea ben saanane angemkemea lema,kwa kuleta mashitaka mitandaoni badala kupeleka kwenye vikao.

yani una matumaini na ben sa8? Huyu ni mramba viatu vya dr slaa na yupo tayari kumponda zzk hata bila sababu!
 
Wahenga walisema " lisemwalo lipo" hivi ni kwanini kila inapokuja issue ya usaliti inamhusisha ZZK ? Inamaana yeye ndo hapendwi tu kwenye CDM? Mie nadhani kuna haja ya kuanza kuwa na doubt na huyu mtu maana amesemwa sana kuhusu kukisaliti chama.

Unajua hata katika maisha ya kawaida ukiona kila jirani anakwambia mkeo ana tabia fulani mbaya usiishie kusema wanafiki tu hawa! Hasa ukiona kila mtu anamtuumu.

Hivyo naanza kuwa na mashaka makubwa kuwa ZZK ni nyoka ndani ya CDM

Hoja zinakuja au zinaletwa?????!!!! Why reifying????!!!
Kuweni makini na waleta hoja kwanza then mpime hoja!!!!!!
 
Mkuu Lema, pengine utusaidie kutupatia maana halisi ya 'Usaliti', 'Unafiki' na 'utu' kwa namna uelewavyo wewe.

Maneno haya kutoka kwako yananishangaza kidogo, kwa vigezo kuwa kwa yale unayofanya nawewe unaweza fuzu kuitewa Mnafiki na Msaliti asie na utu. Labda kama unatumia hii njia kujikosha baada ya wewe pia kutambua kuwa umeonyesha Usaliti mkubwa kwa Watanzania unaowawakilisha.

Lema inatakiwa uelewe haya;

Unatakiwa kujua kuwa hata kina KUBENEA wameshakuchoka, yeye si mmoja wa hao anaowasema? (Au woga ambao siku zote unashabikia ni sumu leo si sumu tena?), pitia hii https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/547535-mh-lema-anaivuruga-chadema.html

Watanzania wengi washakushtukia, unakiruvuga chama kwa siasa zako za kishabiki na kitoto wenzetu wanaita 'armature' (an insult ukiichukulia undani wake) pitia hii https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...gwe-gavana-rahisi-kusababisha-mitafaruku.html

Inawezekana unawashambulia Shibuda na Zitto kwenye bandiko hili, vipi ni kwakuwa wewe Lema unapenda sana Posho hivyo umeamua liwalo na liwe? pitia hii https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...bungeni-zitto-lema-katika-vita-ya-maneno.html

Au unataka kusema hizi posho zinamaanisha Uzalendo na Utu kwa Taifa? (Are you serious??). Zitto alisha litabiri hili na kueleza wazi (hakutumia unafiki) kuwa Siasa za Posho zitasababisha mjenge chuki na mmwite majina yote mabaya! www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/299635-zitto-sijahongwa-ni-siasa-za-urais-na-hasira-za-posho.html

Au hii ndiyo step ya kwanza ya kufanya Zitto aondoke Chadema? Maana inajulikana wazi kuwa kuna mkakati wa kumkatisha tamaa Zitto aondoke CHADEMA mapema kabla mwaka haujaisha ili mpumue ndani ya chama cha watu wa Kaskazini (viongozi wa juu). Inaturudisha kule kule mnako kukataa siku zote (Udini/Ukabila).

Pole zako Lema, watanzania wa leo si mabwege!

Wewe ni mchangiaji husiye na aibu kwani hujui nini Cha kuchangia,hapa tunaongelea mstakabali Wa taifa wewe unaleta U CCM WAKO,kama huna la kufanya nenda ksaidie kinana kukusanya .....lager
 
Karibu sana JF Kamanda.

Hakuna jambo baya katika mapambano kama usaliti.CHADEMA kiliposhambuliwa katika kesi fake za Ugaidi kuna waliosimama na chama kidete katika kushinda vita ile lakini ilikua ni mpango wa Mungu kuwafichua wasaliti.Tukiendeleza harakati hizi za kupambana na CCM basi hata wale wasaliti miongoni mwetu tuwapimie kwa vipimo vile vile tunavyowapimia CCM na watawala dhalimu maana adui aliyejipenyeza ndani ya kambi ya mapambano ni hatari kuliko adui aliyeko nje

Siku hizi kuna silly excuse ya uhuru wa kutoa maoni katika kutimiza matakwa ya usalaiti.Mstari radical kabisa ndio utakaotenganisha wapambanaji na wasaliti kwa Doctrine radical.It's either you are with us or against us.No middle ground.Hata kama Dunia ni three dimension

Vijana tuungane na tusimame kidete.Anayepoteza na kuua ndoto za vijana wengi katika safari ya mapambano ni adui mkubwa wa vijana. Tumaini kubwa ni kuwa katika mapambano yoyote ukiona usaliti unazidi kuibuka ujue ukombozi unakaribia.Mitume na Manabii walisalitiwa katika harakati za ukombozi

"A nation can survive its fools and and even the ambitious but it cannot survive treason from within. An enemy at the gates is less formidable... The traitor moves amongst those within the gate freely, his sly whispers rustling through all the alleys, heard in the very halls of government itself... He rots the soul of a nation, he works secretly and unknown in the night to undermine the pillars of the city, he infects the body politic so that it can no longer resist." (Cicero)

Naunga Mkono hoja hata Mungu mwenyewe amedraw line kwa Binadamu kwamba lazima aamue upande atakao kuwa aamue kuwa moto au kuwa baridi. Amesisitiza wazi kwambi Ukiwa Vuguvugu atakutema. Mwanasiasa yeyote anaye jaribu kubalance katikati ya Dhuluma na Haki na Mwenye kutoa statement zenye kuzungukazunguka ambaye anapo zungumza hasiti kuonyesha mahaba yake kwa watawala na hakitaji Chama kama taasisi isipokuwa pale tu anapotaka kuonesha kwamba bila yeye chama kisingekuwepo au amejitolea sana katika kukijenga Chama au yeye anabusara na mjenga hoja mzuri kuliko wenzake wote walioko mahali fulani... wakati hata eneo analotoka mjengaji Chama kiuhalisia kiko hoi bin Tabani ukiangalia idadi ya wabunge na madiwani kwa uchaguzi wa mwaka 2010 ... ni dalili za wazi za Unafiki,Usaliti na kutokujiamini. LETS OUR PARTY DISCPLINARY MATCHINERY RUMBLE FOR THE LAST is now or never .

Wasaliti watoswe tu liwalo na liwe...NI upumbavu usiomithilika kujaribu kuwapatanisha shetani na Mungu...CHADEMA ni taasisi siyo Mtu na kama Taasisi lazima viongozi wajuu wote wawe na msimamo wa pamaoja katika masuala yote yanayohusu mustakabali wa Chama anaye kuwa Kinyume ni msaliti na dawa ni kumuondoa Kuna Fredom OF Expression na siyo Fredom From expression kama wanavyo fanya wasaliti na kulazimisha watu wawaelewe kama watu wenye busara na maono mapana ya Taifa kumbe nima pretender.

I REPEAT ITS NOW OR NEVEER
 
yani una matumaini na ben sa8? Huyu ni mramba viatu vya dr slaa na yupo tayari kumponda zzk hata bila sababu!

Leta uthibitisho hapa kama unataka kuchukuliwa serious.Unadhani kila mtu ni mnafiki kama wewe na wenzako?
 
Yes kwa kuwa ni kundi lao na kwa kumtetea wakaweka (CISS) kwenye mabano, eti yeye mtoto wa nyumbani kizabizabina.

Ha ha haaa kwa hiyo lingekuwa shambulio la mambo yetu saa hizi marhum!!!!
Alikaa nyuma ya target kwa mujibu wa maelezo yao ili aone mlengaji!!!!!!!
 
well said mkuu......lakini wewe kama kiongozi mmechukuwa hatuwa gani dhidi yake....? hata hatuwa za mwanzo!
si wamempiga na kumsimamisha uwenyekiti! Hizo ndo hatua za kwanza. Mchakato unaendelea.
 
Lema unajifanya una uchungu na Chadema wakati wewe unapambana na interpol kwenye kazi zako wala Chadema hawakujui, mwenzako Zitto anakijenga chama.
 
anachofanya hakuna tofauti yake na Mwigamba wote wanafanya ujinga hule hule.[/QUOTE]
KWELI ILA KUNA MSUKULE UNAITWA ZINC UNASEMA ETI LEMA KAJA NA REALY ID SO HANA KOSA! NAJISIKIA VIBAYA KUA CHAMA K1 NA WATU KAMA ZINC NA MUNGI ILA NTAZD KUWAPA ELIM
 
Unatia huruma kijana. Post yote hiyo uwezo wako wa kufikiri umekomea hapa?

Unajua maana ya aibu? Kama hujui maana yake ni wewe kudhihirisha ni kwa namna ipi ambavyo wanakufikiria, wanakuyumbusha, wanakuendesha, na kukufanyia maamuzi yote hadi kukufanya ukose soni kwa kuonyesha ni kwa namna upi ubongo wako haujishughulishi kufikiria wala kuelewa vilivyo andikwa. Kalale.

Wewe ni mchangiaji husiye na aibu kwani hujui nini Cha kuchangia,hapa tunaongelea mstakabali Wa taifa wewe unaleta U CCM WAKO,kama huna la kufanya nenda ksaidie kinana kukusanya .....lager
 
Tatizo kubwa linalomcost Lema ni kuwa aliingia bungeni akiwa ns Lengo la kumfunika ZZK lkn kajikuta akaachwa umbali wa Dar-kigoma.Maana hana IQ ya lema ni bellow 20.
Sasa kila walipokubaliana kama chama juu ya msimamo flani,wapo waliokubali kwa moyo mmoja lkn lema ni sawa na mwsnafunzi anaekubali kwenda discussion kwa shinikizo,huyu siku zote atakuwa anasinzia tu. Hivyo Lema alilazimishwa na hoja ya kutochukua posho iliyoibuliwa na Zitto.lkn mara baada ya hoja hii kuibuka ni kuwa mh.Shibuda alipinga palepale na wananchi tukajua msimamo wake.lkn wanafiki wote akiwemo Lema alijifanya karidhika wakati nafsi yake ikitukutia.
Hivyo Zitto huwa ni mkweli ktk mission anazozianzisha,hafanyi mambo kujionyesha mbele ya watanzania bali ni Mzalendo wa keli mwenye uchungu wa kweli juu ya matatizo yanayotukabili.ndio maana wasaliti na wanafiki wanaanza kuonyesha jinsi walivyo.
Lema ni kama mwanamke anaeficha udhaifu wake kama vile uzinzi,ulevi, na roho mbaya wakati wa kumchumbia lkn baada ya ndoa na kuanza maisha ndipo huanza kuzua jipya kila kukicha.
Lema ni mtu hatari kwa future yavijana,Zitto ulitujengea msingi mzuri wa vijana kuanza kuaminiwa na wananchi,ulifanya vizuri ktk historia ya ubunge wako,vijana wa nchi nzima tukatumia jina lako ili kuungwa mkono na wapiga kura,uliwanadi wengi ktk majimbo yao na wajaungwa mkono na wananchi kwa sababu ya umakini na uadilifu wako.sasa wameingia wadaliti bungeni badala ya kufuata mwebendo mwema wa Zitto kabwe wao wameharibu taswira ya vijana,sasa vijana twaonekana walevi,wagomvi na wavuta bangi.
Vijana tumedhalilishwa vya kutosha kwa vijana wenzetu kwenda kufanya madudu bungeni na sada kwenye chama kilichojengwa kwa nguvu kubwa.
Lema hatutakusahau ktk historia ya usaliti Tanzania.
 
Mheshimiwa Lema,
Kutokana na ujumbe wako huu, ni wazi ndani ya CHADEMA kuna matatizo ambayo ili chama kisonge mbele, kinahitaji kuyashughulikia.

Kwa mtu yeyote anayejua demokrasia ya kweli, matatizo yatokanayo na misimamo tofauti ndani ya vyama, hutatuliwa kwenye sanduku la kura.

Kama ndani ya CHADEMA kuna wasaliti, basi njia bora kuliko zote na ambayo historia inatuonyesha ndio mwarobaini mzuri, ni kuitisha uchaguzi ili wanachama waamue kama hao watu ni wasaliti au ni wakombozi. Ni wanachama tu wana mandate ya kuamua nani awe kiongozi kwenye vyama vinavyofuata misingi ya kidemokrsia.

Waziri mkuu wa Uingereza, Thatcher, alipokuwa challenged na wasaliti ndani ya chama mwaka 1989, aliitisha uchaguzi wa wa chama na akashinda na wasaliti wakapotea.

Mwaka 1990 ukatokea usaliti mwingine na safari hii Tatcher akashindwa na wasaliti wake na Major akachaguliwa kuwa PM.

Kwa maoni yangu mimi, kama ndani ya CHADEMA kuna usaliti, basi ni kuwaambia hayo makundi kukutana kwenye kisanduku cha kura ili wanachama wawaondoe wale ambao wanachama wanaona hawafai.

Lakini hii yakuitana wasaliti kwrenye mitandao, sidhani kama itakisaidia chama hata kidogo. Kibaya zaidi mtawatisha hata wale watu wazuri ambao wangependa kuungana na CHADEMA 2015. Hakuna mtu makini anayependa kwenda chama ambacho kutofautiana mawazo unageuka kuitwa msaliti.
 
Mkuu Lema, pengine utusaidie kutupatia maana halisi ya 'Usaliti', 'Unafiki' na 'utu' kwa namna uelewavyo wewe.

Maneno haya kutoka kwako yananishangaza kidogo, kwa vigezo kuwa kwa yale unayofanya nawewe unaweza fuzu kuitewa Mnafiki na Msaliti asie na utu. Labda kama unatumia hii njia kujikosha baada ya wewe pia kutambua kuwa umeonyesha Usaliti mkubwa kwa Watanzania unaowawakilisha.

Lema inatakiwa uelewe haya;

Unatakiwa kujua kuwa hata kina KUBENEA wameshakuchoka, yeye si mmoja wa hao anaowasema? (Au woga ambao siku zote unashabikia ni sumu leo si sumu tena?), pitia hii https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/547535-mh-lema-anaivuruga-chadema.html

Watanzania wengi washakushtukia, unakiruvuga chama kwa siasa zako za kishabiki na kitoto wenzetu wanaita 'armature' (an insult ukiichukulia undani wake) pitia hii https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...gwe-gavana-rahisi-kusababisha-mitafaruku.html

Inawezekana unawashambulia Shibuda na Zitto kwenye bandiko hili, vipi ni kwakuwa wewe Lema unapenda sana Posho hivyo umeamua liwalo na liwe? pitia hii https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...bungeni-zitto-lema-katika-vita-ya-maneno.html

Au unataka kusema hizi posho zinamaanisha Uzalendo na Utu kwa Taifa? (Are you serious??). Zitto alisha litabiri hili na kueleza wazi (hakutumia unafiki) kuwa Siasa za Posho zitasababisha mjenge chuki na mmwite majina yote mabaya! www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/299635-zitto-sijahongwa-ni-siasa-za-urais-na-hasira-za-posho.html

Au hii ndiyo step ya kwanza ya kufanya Zitto aondoke Chadema? Maana inajulikana wazi kuwa kuna mkakati wa kumkatisha tamaa Zitto aondoke CHADEMA mapema kabla mwaka haujaisha ili mpumue ndani ya chama cha watu wa Kaskazini (viongozi wa juu). Inaturudisha kule kule mnako kukataa siku zote (Udini/Ukabila).

Pole zako Lema, watanzania wa leo si mabwege!

Huu ndio uhuru wa kutoa maoni na yapasa tuheshimu mtzamo wako though ni vigumu kukubaliana na baadhi ya unazoamini kuwa ni facts. Ila tujue kuwa kila mtu ana strengths na weaknesses zake. Hivyo kwa wakati Fulani ni vizuri kujua kuwa unapo jaribu kuanika weaknesses zamtu itakuwa vizuri pia uka-acknowledge strengths zake.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom