Usalama wa Taifa: Mpo likizo?

Status
Not open for further replies.
Wamiliki wa makampuni haya ni watu wa karibu na Mkurugenzi Mkuu wa Zamani wa Usalama wa Taifa. Exellent Services Limited-- Emil Samaya Peter Sabas na Elisifa Ngowi na Clyton Marcketing Ltd ya Edwin Mtoi na Elisifa Ngowi.... Huyu Elisifa yuko karibu mno nna Cornel Apson na makampuni haya mawili yamo katika list ya EPA

Mungu wangu....
 
Ahh Nimechoka sasa, Nitasema haya na litakalokuwa liwe:

Hawa jamaa wa usalama wa taifa (TISS) wamezidi sana na inabidi tuanze kuwashikia bango nao. Niliwapa breki kidogo maana ile hofu ya agents kunitafuta na kuitafuta familia yangu ilikuwa inanisumbua lakini sasa gloves are off. Nitaanza kuweka vitu vyenu hapa nyie wezi na mafisadi wa usalama wa taifa na lolote mnalotaka kufanya mfanye tu. Ni mimi na JF against nyie:

Katika unafiki wa hali ya juu, Raisi Kikwete juzi ametangaza kumfuta kazi Balali (ambaye alishatangaza kujiuzulu) na kutoa amri ya kuendelea kufanya uchunguzi wa BOT. Cha kutia hasira ni kitendo cha Kikwete kutangaza makampuni 22 ambayo anadai kuwa ndiyo yamehusika na upotevu wa pesa BOT huku kwa makusudi kabisa akiacha kuzitaja kampuni za DeepGreen na Tangold. Cha kutia hasira tena ni kitendo cha ikulu kukataaa kuweka wazi report ya ukaguzi wa BOT iliyofanywa na E&Y kwa masingizio kwamba hiyo report inahusu mambo ya usalama wa taifa.

Huu usalama wa taifa kwa sasa umezidi. Tangold inahusiana moja kwa moja na usalama wa taifa. Jamaa wanahusishwa na wizi mkubwa sana kwa kupitia kampuni hewa. Hebu kumbuka hii iliyotolewa na Dr Slaa:



Hebu angalia hapo mkondo wa pesa kutoka benki kuu kwenda Tangold na kuishia TISS.

What the f......k with this TISS, hawa ni kina nani na mbona hawaguswi?


Kwenye ile thread ya Jamaa mwengine nilieleza wazi kwamba hawa jamaa TISS wapo ku-facilitate wizi wa hao mafisadi
 


BILA KUSAHAU KUWA MTOTO WA APSON NDIYE ALIYEPEWA TENDA YA KUJENGA BENKI KUU ZANZIBAR

na kuonyesha kuwa like Father like son

walitaka kutapeli kwa kuimport POLISH LABORERS toka UK ili ionekane kuwa kazi inafanywa na wazungu professional!

Kwa kuongezea tu hapo MKUU,
huyu mtotot wa Apson na mkewe wanatumia mapesa hayo kwa kufanya mibiashara ya hela ndefu bila ya kufanya research zaidi zaidi kutumia nguvu ya vitoto vina vyojiunga na TIss kuwatembeza juani mchana kutwa kuwatafutia miashara(marketing)
 
Hawa TISS -NI WAO , KWANI WANATAFUTANA HUMO NDANI KWA NDANI NA HILO LILIKUWA NI KOSA LA KIUFUNDI WALILIFANYA KWANI WALIKUWA HAWAJUI KUWA KUNA SIKU YATAKUJA KUDHIHIRIKA HAYA MAMBOP YAOP WALIFIKIRI WANAFANYIA KIZANI KUMBE WAPO SASA PEUPE.

KAZI ITAENDELEA TENA MWAKA HUU UTAKUWA NI MWAKA MGUMU ZAIDI KWA MAFISADI KWANI WENGI WAO WALIKUWA WANASUBIRIA MGAWO MWINGINE PALE BOT ILA UMEGONGA MWAMBA NA HAPAO NDIPO WATAJIJUA.

BOT KUNA KITENGO CHA TISS KINAITWA DIGESTION ROOM NA HUWA WANAPITIA MALIPO NA KUONA KAMA YAPO SAHIHI SWALI KWA NINI HAWQAKUONA UFISADI HUUU.....
 
Nimejaribu kutafakari yote yanayozungumzwa kuhusu rushwa[bribery], ubadhirifu [mismanagement] na ufisadi[corruption] nchini mwetu, asilimia 80 mikasa hiyo ingeweza kutibuliwa[interception], kuzuiliwa[prevention] na kudhibitika[control].

Nasema "ingeweza" kama Idara ya Usalama wa Taifa na nyinginezo nyeti, zingekuwa zikifanya kazi zao kwa manufaa ya taifa na bila kuingiliwa na wanasiasa ambao kwa kiasi kikubwa wamekuwa wakizingatia mislahi yao binafsi au vikundi vya watu[grand scale corruption].


Njama

Mathalan, watanzania wenzangu mnatambua ni vigezo gani hutumika kupindua serikali ya nchi?Jibu ni vingi, lakini kimojawapo ni fedha!Je kwa mtu mwenye dhamira akawa na bilioni 133[japo zilizoibiwa ni nyingi zaidi] angeshindwa kuipindua serikali?Mapinduzi ninayozungumzia siyo lazima yawe ya kijeshi.....

Sasa basi, endapo kuna Idara ya serikali inagharamiwa kwa kodi ya wananchi kutumia kiasi kikubwa cha fedha kisicho na ukaguzi [auditing], inakuwaje kuwe na watu wanaweza kutorosha matrilioni ya shilingi bila wao kushtuka na kuchukua zile hatua muhimu nilizoorodhesha hapo juu[red flag]?

Hitimisho langu ni kwamba, Idara ya Usalama wa Taifa, sasa imegeuka kuwa Idara ya Usalama wa CCM.Miaka hii kuna vitisho vingi kwa usalama wa nchi, ikiwa ni pamoja na ugaidi.Kwa mtindo huu wa usalama tulionao, hamkubaliani nami kwamba jamaa wanatuangusha?

Hujuma

Lakini, usisahau kuwa linapokuja swala la kuwabana na kuwahujumu wapinzani[political sabotage] jamaa wako smart kuliko intelligence ya mataifa hata yaliyoendelea.Hawawapi fursa ya kupumua, japo katika miaka miwili iliyopita, wameanza kuonyesha kuzidiwa -wakubwa wanafanya blunder nyingi mno kiasi kwamba counter-attack inawashinda.Assets au agents walionao, wengine wana-leak information kwa wapinzani, sababu wanaona ni kinyume na maadili na mafunzo waliyopewa.

Imagine wanawafuatilia wanasiasa wa upinzani hata wanapokuwa ziarani mataifa ya magharibi, kujua wanaongea nini na kukutana na nani, wakati kazi ya kuziba matundu ya wizi BOT, RICHMOND, BUZWAGI na kwingineko wanajifanya hawakuona na hawahusiki.Halafu, jambo moja watanzania hawalizungumzii, katika miradi ya kutafuta mafuta, hiyo mikataba wanayosaini inasema Tanzania kama taifa itapewa mgao kiasi gani endapo mafuta yatapatikana katika ardhi yake -- ulizeni muambiwe ndipo mtasema hatuna viongozi sisi Tanzania.

Kwa maana hiyo basi, idara hii ya usalama wa taifa inachangia kuididimiza Tanzania katika matatizo.Inatumia vibaya asili ya ukimya na usiri wa shughuli zake kuangamiza jitihada za wachache wanaoitakia nchi maendeleo.

Ndumilakuwili

Pia inachekesha kuona eti Waziri mkuu Edward Lowassa akiwa mstari wa mbele kukemea rushwa, kwa mtizamo wangu mimi, katika serikali ya Kikwete, ukitoa Dr Shein, wengine wote waliobaki ni mchwa wa kutafuna mali ya wananchi.It's like watching a drama episode.
 
Usishangae nako huko kuna ajira za kujuana maana ni kitengo cha kuzuia sisi wanyonge tusiseme, ukisema unaambiwa huyo ni mtu wa usalama wa taifa unaufyata kimya.
 
Usishangae nako huko kuna ajira za kujuana maana ni kitengo cha kuzuia sisi wanyonge tusiseme, ukisema unaambiwa huyo ni mtu wa usalama wa taifa unaufyata kimya.

.......Usalama wa Taifa wako kwa ajili ya misafara na ulinzi wa mafisadi.Leo Rais au waziri mkuu akialikwa kuhudhuria hafla basi ni tafrani wala hamna raha,vizuizi kila kona.Mbona hata hao nao wataonja mauti..Wanatenda masilahi ya yule aliyewaapisha wala si kwa ajili ya Taifa...
 
hawa mbwa wanusaji miongoni mwao nao nimafisadi piA WAPO AMBAO HAWAPENDI KUFANYA HAYO LAKINI WANALAZIMIKA KUTOKANA NAMASHINIKIZO KUTOKA KWA VIGOGO FISADI.
naungana namwandishi kuwa HII NI IDARA YA USALAMA WA CCM(CHUKUA CHAKO MAPEMA)
 
despite the fact kwamba intelligence yetu inaweza kuwa incompitence in one way or another lakini lets think rational kwanza, kazi ya kimsingi na ya kikatiba ya int. nyingi duniani, ikiwemo yetu ni KUISHAURI SERIKALI, asa inapokuja swala na last decision hio sio kazi tena yake, so sometimes it depends na political will ya pol. leaders tulionao icluding na uwezo wa ushawishi wa int. yenyewe kwa serikali.Dont tell me kuwa ufisadi kama wa BOT awa jamaa walikuwa hawajui,am sure walikuwa wanajua A to Z, sasa why didnt they take serious action?,asa frm there unaweza kupata picha ni aina gani ya viongozi tulionao ikichukuliwa kuwa they were well informed.
 
kazi ya kimsingi na ya kikatiba ya int. nyingi duniani, ikiwemo yetu ni KUISHAURI SERIKALI, asa inapokuja swala na last decision hio sio kazi tena yake

Hoja ya msingi! Usalama wa Taifa kazi yao kubwa ni kufanya uchunguzi na kutoa ushauri. Ni jukumu sasa kwa vyombo husika kuchukua hatua zinazostahili.

Kama nilivyowahi kusema huko nyuma, suala la BOT ni mchezo wa kuigiza, kwa kuwa wanaotakiwa kuchukua hatua ndio wahusika katika sakata lenyewe.
 
Ni hivi ndugu yangu, naomba uwaangalie hawa watu wa usalama wa Taifa ambao wako kule bandarini kwa ajili ya kuangalia mali inayoingia na kutoka yaani 'import and Export' ili serikali isije ukahujumiwa kwa namna mojqa au nyingine. Lakini wapi !. Wale wamekuwa very rich kwa sababu ya kujihusisha na rushwa wakishirikiana na maafisa wa TRA. WENGINE NI VIJANA WADOGO TU WAMETOKA SHULE JUZI HWANA MUDA KAZINI LAKINI WANA MAHEKALU HUKO MIKOCHEN,MBEZI BEACH NK. Hawa ndo wanawezesha magogo kuuzwa nje na hata madawa ya kulevya kupita hapa.Nataka nikuambie hivi ,hawa wanalindwa na kutetewa na Idara yao kwa hali ya juu sana. Ona mahali ambapo maafisa wa TRA,wametuhumiwa na hata kufunguliwa kesi mahakamani na hata kufungwa kwa makosa ya kukagua mzigo na kwa kutokuwa mwangalifu na kusababisha Serikali kupoteza mapato au kutoona mali ya ziada ndani ya containa ambayo haijalipiwa ushuru au containa kukutwa na madawa ya kulevya au kusafirisha mogogo ambayo yamepigwa marufuku, hawa wajamaa unakuta wakati wa ukaguzi wa shehena hiyo wanashiriki asilimia 100 na kama mgao ukitoka wanapata wa kwao,lakini likigarambuka,wao hawashitakiwi bwana. Sasa ni watu gani hawa ambao hawawezi kuwajibishwa? Kwa nini huyo ofisa wa TRA asulubiwe peke yake? Je,hii ni Idara ya nini hasa? Are they above the Law or they have immunity? Hili ni eneo dogo tu la kujifunzia kama hutaki nenda Bandarini ukasimame kwenye container wakati wa kukagua mizigo utaona wanavyofanya.They are too part of TRA Officials but they do not commit or sign any document partaining to the merchandise yet they demand their 'cut' and when things go astray they are unquetionable.I would expect that the first person to to be caught and be interogated is 'usalama wa Taifa guy' kwa sababu ameshiriki kuhujumu nchi ihali amekula kiapo kulinda nchi na mapato yake.Lakini yeye anaachiwa kwa vile tu hashiriki kusaini hiyo kadhia ya forodha.Naona kuna walakini hapa bwana. I think there is a need to overhall the whole department or create another organ to oversee their activities.
 
despite the fact kwamba intelligence yetu inaweza kuwa incompitence in one way or another lakini lets think rational kwanza, kazi ya kimsingi na ya kikatiba ya int. nyingi duniani, ikiwemo yetu ni KUISHAURI SERIKALI, asa inapokuja swala na last decision hio sio kazi tena yake, so sometimes it depends na political will ya pol. leaders tulionao icluding na uwezo wa ushawishi wa int. yenyewe kwa serikali.Dont tell me kuwa ufisadi kama wa BOT awa jamaa walikuwa hawajui,am sure walikuwa wanajua A to Z, sasa why didnt they take serious action?,asa frm there unaweza kupata picha ni aina gani ya viongozi tulionao ikichukuliwa kuwa they were well informed.[/
QUOTE]

Mimi hupata bahati ya kukaa na hawa jamaa,kwa hasira na chuki niliyonayo huwaambia ukweli kuwa CCM ni chama cha majambazi,ambacho sikipendi kabisa na sitojali hata kama Watanzania 40m watakipigia kura ya ndiyo WATAKUTA KURA YANGU MOJA TU YA HAPANA.Ukishaanza kuzungumzia mambo ya CCM wao hukaa kimya na huanza kuniona mie kama Adui.
Point yangu ni kuwa huo ushauri wanaotoa,wanautoa kwa manufaa ya CCM au manufaa ya Nchi?? Wao hutoa ushauri ili mambo yasiende kombo kwa CCM na si kwa Watanzania(Nchi).Hawa usalama wa Taifa ni kajibwa fulani ka CCM ili kuhakikisha wanaendelea madarakani.
 
Mwaka jana, Mwanakijiji alituletea mada kuhusu matamshiya Waziri wa Khabari Seif Khatibu kuhusu uhuru wa vyombo vya habari na ile Sheria ya Usalama wa Taifa ya mwaka 1970.

Bunge letu mnamo mwaka 1996, lilipitisha kuanzishwa kwa taasisi ya Usalama wa Taifa TISS kwa mujibu wa katiba.

Naomba kuuliza, je Usalama wa Taifa ni kitu gani? Chombo hiki TISS kina manufaa gani kwa Taifa?

Mosi, Chombo hiki kinawajibika kwa Rais pekee kwa utashi wake na si utashi wa Taifa. Kwa nini mkurugenzi mkuu na Taasisi nzima haziwajibiki kwa Bunge hata kupitia kamati yake ya Ulinzi na Usalama?

Pili, Mkurugenzi Mkuu ni uchaguzi na uteuzi wa Rais, kwa nini mtu huyu asipendekezwe na Rais na kisha kuidhinishwa na Bunge ?

Ukiangalia kipengele cha nne cha kuundwa kwa TISS ambacho ni kuhusu nguvu za kidola na mamlaka, sheria hii inashindwa kubainisha kuwa Usalama wa Taifa ni kitu gani na ni vipi TISS lishughulikie Usalama wa Taifa.

Hivyo basi, sheria hii ya 1996 ina udhaifu mkubwa sana kwa kulenga shughuli za Usalama wa Taifa kuishia kuwa mambo ya kuvamiwa, kupindua nchi au kuchafua hali ya hewa kwa mlengo wa kisiasa badala ya shughuli hizi kuhusisha mambo mengine ya muhimu kwa Usalama wa Taifa kama uzalishaji mali, uchumi, afya, elimu na kadhalika.

Aidha, chombo hiki si kwa manufaa ya taifa bali ya Serikali na Raisi wake. Je ni vipi tunaweza kuwa na umahiri katika vita dhidi ya uhujumu wa Usalama wa Taifa letu ikiwa chombu husika kimejengwa kwa Sheria dhaifu na mipaka yake ya kazi na utendaji kazi si makini katika masuala yote yanayuhusu Usalama wa Taifa?

Napenda kutoa hoja.
 
Ukisoma tangazo la Usalama wa Taifa la mwaka 1970 ambalo bado linatumika, kila tunachofanya humu ni batili kwa kuwa sheria hii bado inatumika na ni sheria hii inayokipa CCM nguvu za kuburuza Taifa.

Je, hu siwakati muafaka kupitia Sheria hizi mbili hii ya Usalama wa Taifa ya mwaka 1970 na hii ya kuundwa Idara ya Upelelezi wa masuala ya usalama wa Taifa ya 1996 na kuziandika upya kwa mazingira tuliyonayo au Mary Nagu na Mwapachu watatuambia kuwa kila kitu ni shwari?
 
Ki-Historia chombo hiki kilianzishwa kwa ajili ya manufaa ya Rais Nyerere,1967 baada ya Azimio la Arusha.Lilikuwa ni giza kubwa na jinamizi ktk anga za Tanzania.Mkuu wa kaya kwa Udikteta wake kwa vile ilikuwa "lazima" afanikiwe malengo YAKE basi akaamua kuanzisha hayo sijui ma-Usalama wa Taifa.(Kwa ajili ya Usalama wake)
Waliokuwa against nae akawaita Terrorist so kukawa na Terror campaign.Mambo tunayajua yalivyoenda.

Nyerere ili kutimiza malengo yake ya azimio la Arusha,miaka ya 1970's akaja na Vijiji vya ujamaa.ETI katika hali ya kuimalisha Ulinzi(security) wa Taifa akaanzisha utawala wa mabalozi,m/kiti,katibu kata nk hadi ngazi ya taifa.Watu wakakaa chini ya uongozi wa nyumba kumikumi.Hapa ndo hilo dudu li-Usalama Wa taifa lilipopanuka zaidi.Balozi alikuwa anawajua watu wake barabara.Wanasema nini,wanakula nini na wanaishi maisha ya style gani na yeye alikuwa anaripoti taarifa hizo ngazi kwa ngazi hadi mkuu wa kaya anazipata.

Kama tutakumbuka vizuri,kipindi hiki ndicho watu waliishi kwa hofu sana.Watu walikuwa hawaaminiani. Ilifikia kipindi hata wanandoa hawaaminiani.Yote hii ni kwa ajili ya Usalama wa Taifa.Watu waliogopa hata kupiga stori mtaani wakiogopa atakapoongea hapo kuna Usalama wa Taifa atamripoti.Basi ikawa kimya na watu hadi wakashindwa kuongelea kero zilizokuwepo wakati wa operation ya vijiji.Ulitakiwa uongee kile tu Nyerere anachotaka uongee na si vunginevyo.Basi Nyerere huyo na li-Usalama lake hadi leo.

Kikatiba sawa ni kama hivyo mnavyosema lakini ukweli unabaki tu kuwa Chombo hicho kipo kwa ajili ya manufaa ya rais.

KISASA basi,sie (Inawezekana wewe haumo)tunaiona Usalama wa Taifa na idara zake kama Chombo cha kujaza makataratasi/mafaili tu ya watu.Watakuwepo mkoani wataandika habari za Majita weeeeeeeeee hadi wanajaza kabati.Baada ya hapo...Ziiiiii.

So mimi sioni UMUHIMU wa hili dudu,umuhimu wa kurekebisha sheria inayoihusu wala umuhimu wa kuijadili.Ninaloweza kusema tu ni kuwa Usalama Wa taifa Imepitwa na wakati.Wavunje na waje na kitu kingine.Aibu kukalia majungu na kuandika habari za watu tu.Si wajiite tu idara ya kuandika historia za Watu????
 
Majita,

Shikrani sana kwa kunikumbusha ya mbala ya kuhofia Nyoka na kuswoka lupango.

Lakini kuna haja sasa kujiuliza ni vipi chombo hiki kinabidi kibadilishwe na kulitumika Taifa na si Rais na woga wake?
 
Mwaka jana, Mwanakijiji alituletea mada kuhusu matamshiya Waziri wa Khabari Seif Khatibu kuhusu uhuru wa vyombo vya habari na ile Sheria ya Usalama wa Taifa ya mwaka 1970.

Bunge letu mnamo mwaka 1996, lilipitisha kuanzishwa kwa taasisi ya Usalama wa Taifa TISS kwa mujibu wa katiba.

Naomba kuuliza, je Usalama wa Taifa ni kitu gani? Chombo hiki TISS kina manufaa gani kwa Taifa?

Mosi, Chombo hiki kinawajibika kwa Rais pekee kwa utashi wake na si utashi wa Taifa. Kwa nini mkurugenzi mkuu na Taasisi nzima haziwajibiki kwa Bunge hata kupitia kamati yake ya Ulinzi na Usalama?

Pili, Mkurugenzi Mkuu ni uchaguzi na uteuzi wa Rais, kwa nini mtu huyu asipendekezwe na Rais na kisha kuidhinishwa na Bunge ?

Ukiangalia kipengele cha nne cha kuundwa kwa TISS ambacho ni kuhusu nguvu za kidola na mamlaka, sheria hii inashindwa kubainisha kuwa Usalama wa Taifa ni kitu gani na ni vipi TISS lishughulikie Usalama wa Taifa.

Hivyo basi, sheria hii ya 1996 ina udhaifu mkubwa sana kwa kulenga shughuli za Usalama wa Taifa kuishia kuwa mambo ya kuvamiwa, kupindua nchi au kuchafua hali ya hewa kwa mlengo wa kisiasa badala ya shughuli hizi kuhusisha mambo mengine ya muhimu kwa Usalama wa Taifa kama uzalishaji mali, uchumi, afya, elimu na kadhalika.

Aidha, chombo hiki si kwa manufaa ya taifa bali ya Serikali na Raisi wake. Je ni vipi tunaweza kuwa na umahiri katika vita dhidi ya uhujumu wa Usalama wa Taifa letu ikiwa chombu husika kimejengwa kwa Sheria dhaifu na mipaka yake ya kazi na utendaji kazi si makini katika masuala yote yanayuhusu Usalama wa Taifa?

Napenda kutoa hoja.

Rev.Kishoka I have agreed on so many issues that you have brought forward. Kudos. lakini hapa nakupinga.(Mitazamo inayogongana)....

Aidha, chombo hiki si kwa manufaa ya taifa bali ya Serikali na Raisi wake. Je ni vipi tunaweza kuwa na umahiri katika vita dhidi ya uhujumu wa Usalama wa Taifa letu ikiwa chombu husika kimejengwa kwa Sheria dhaifu na mipaka yake ya kazi na utendaji kazi si makini katika masuala yote yanayuhusu Usalama wa Taifa?

How do yo envisage such an organ?
Asante.
 
Happiness Katabazi

BAADHI ya Watanzania, wakiwamo viongozi mbalimbali wastaafu na wale wa vyama vya upinzani, wamekuwa wakiliambia taifa kwamba limepungukiwa viongozi waadilifu na kwamba umaskini unaolikabili taifa letu ni wa kujitakia.

Kwa sababu, licha ya rasilimali kubwa tulizonazo, hatuna viongozi wenye upeo wa kutuonyesha njia ya kuzitumia vyema ili kutupatia maendeleo.

Badala yake tunaona kuwa tunao viongozi wasio waadilifu, mafisadi, wazandiki na wababaishaji wa kutupwa.

Uongozi wa taifa una mfumo wa kitaasisi ambao wengi wanaita ‘system’. Kwa lugha ya kawaida ‘system’ inamaanisha mfumo wa Idara ya Usalama wa Taifa katika kuchagua na kudhibiti ubora wa viongozi na mwenendo wao.

Moja ya wajibu mkubwa wa idara hiyo ni kulipatia taifa viongozi bora, wazalendo na waliofundwa vya kutosha kutumia madaraka yao kutetea masilahi ya taifa. Lakini wimbi la ufisadi lililojitokeza nchini ni ishara kwamba Idara yetu ya Usalama wa Taifa imeshindwa kazi.

Moja, idara hiyo imegeuka kuwa ni sehemu ya CCM, badala ya kutekeleza wajibu wake tulioutaja kulingana na Katiba na sheria za nchi, ikiangalia vyama vyote, taasisi zote za kijamii nk.

Baadhi yao wamejifanya ni watendaji wa CCM na wanapotenda hivyo kazi yao kubwa inakuwa ni kuhujumu viongozi walio kwenye vyama shindani kana kwamba hawa si Watanzania, ila ni maadui wa nchi.

Pili, kuzuka kwa kundi la wanamtandao ambalo linadaiwa kumuweka madarakani Rais Kikwete kunaashiria ushiriki mkubwa wa idara hiyo kupanga mtandao kuhusisha sekta zote za jamii na kuhusisha watendaji muhimu serikalini ili wote kwa pamoja watekeleze azima ya CCM kubaki madarakani.

Inasemekana kwamba nyuma ya ufisadi unaofichuliwa, yapo makampuni ya kifisadi ambayo hayumkini yalianzishwa na Idara ya Usalama wa Taifa kukusanya mabilioni ya fedha yaliyotumiwa na wanamtandao na CCM kwenye Uchaguzi Mkuu wa 2005.

Hakika yeyote anayependa kusema ukweli atakiri kwamba mabilioni ya fedha yaliyotumika kwenye mchakato ndani ya CCM na mabilioni ya fedha yaliyotumiwa na CCM katika uchaguzi uliopita, hayana maelezo au chanzo kingine kama si makampuni hayo ya kifisadi ya kupora fedha za umma.

Sasa tujiulize, taasisi hii ina uadilifu kiasi gani, na je, aijashiriki katika ufisadi kwa namna yoyote ile?

Ikiwa watetezi wa Usalama wa Taifa watasema inatenda kazi zake kwa mujibu wa Katiba na sheria za nchi, je, walilala wapi Benki Kuu ilipohujumiwa?

Je, ilikuwa wapi masilahi ya nchi katika uzalishaji wa umeme yalipohujumiwa katika mradi wa IPTL na Richmond?

Je, walikuwa wapi masilahi ya nchi yalipohujumiwa katika ubinafsishaji wa Benki ya Taifa ya Biashara, TTCL na makampuni mengine mbalimbali ya umma?

Tunachokiona sisi, Idara ya Usalama wa Taifa haijui wajibu wake na ambayo ufisadi ni sehemu kuu ya kazi yake.

Pia, tunachokiona sisi ni idara hii kutojua kutetea masilahi ya nchi, ambayo ipo tayari kuona rasilimali za nchi zikihujumuiwa ili mradi wanaofanya hivyo ni marafiki zao.

Kazi kubwa ni kulindana, kupeana vyeo bila kuwa na sifa na pia kuwapiga vita wale wanaojitokeza kupingana na mwenendo wa kifisadi.

Tumefikishana mahala watu sasa wanamwagiwa tindikali, wanahushishwa kwenye ajali za kupangwa, bila shaka siku si nyingi tutashuhudia mauaji ya watu kwa mtindo wa kijambazi, unaotumiwa na kundi la Mafia.

Inapotokea kwamba viongozi wa taifa ama serikali wanapata nyadhifa au kuajiliwa kazini kwa sifa za ubabaishaji au kughushi, na hilo likafumbiwa macho, basi hakuna usalama wa taifa.

Kwa maana kwamba ikiwa uongozi utawekwa mikononi mwa matapeli walioghushi sifa za elimu, basi hatima ya taifa itakuwa hatarini.

Je, viongozi wa aina hii wataelewa nini kinachoendelea kuhusu mikataba ya biashara ya madini au mikataba ya umma? Kwa hiyo tusishangae serikali yetu kuendeshwa kama viongozi wake hawajaenda shule, kwani si kila anayejiita daktari ni daktari wa kweli.

Mfano, ilikuwaje kampuni ya kihuni ya Richmond kupewa mkataba wa mabilioni ya fedha kununua majenereta ya umeme bila Idara ya Usalama wa Taifa kujua?

Je, kukosekana kwa umeme si jambo nyeti na hatari kwa usalama wa taifa? Au labda idara hii inaona Watanzania wamelala usingizi na wako tayari kufanyiwa vitendo viovu na wako tayari kulipishwa kodi na kubebeshwa gharama kubwa za maisha bila kulalamika au hata kufanya maandamano?

Labda Watanzania wamekuwa wapole mno katika kutetea haki zao. Bila shaka Idara ya Usalama wa Taifa itaona ugumu wa maisha wanaopata wananchi pale tutakapokuwa tayari kuandamana na kuwatoa maofisini na kuwafukuza kwa bakora hao mafisadi!

Kwa ujumla, vyombo vyetu vya ulinzi na usalama tulivyonavyo, chombo ambacho akijatutendea haki ni Idara hii ya Usalama wa Taifa. Hawa wamelala usingizi wa pono wakati nchi inahujumiwa, wananchi tunapata taabu.

JWTZ, Magereza, JKT na Polisi wanafanya kazi nzuri, tunawapongeza, licha ya kwamba wamekuwa wakilalamikia bajeti za wizara zao kuwa ni finyu kuliko bajeti ya Idara ya Usalama wa Taifa.

Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), chini ya Davis Mwamunyange, wanafanya kazi nzuri na ndiyo maana hadi sasa nchi yetu haijavamiwa na maadui.

Polisi chini ya IGP - Said Mwema, nao wamejitahidi kwa kiasi kikubwa kupunguza wimbi la uhalifu.

Magereza chini ya Kamishna Mkuu, Agustino Nanyaro nao wamejitahidi, kwani hadi sasa hatujasikia kuwa wafungwa wamevunja magereza na kutoraka. JKT nao wanajitahidi kwa kuwalea vijana na kuzalisha mali.

Wakati umefika sasa watendaji wa Idara ya Usalama wa Taifa wawajibike kikamilifu bila kumuonea haya kiongozi yeyote, ama sivyo itabidi idara hii ivunjwe, tuunde chombo kipya, na hilo linawezekana, kama tuna uchungu wa kweli na Tanzania yetu.

Mungu ibariki Afrika, Mungu ibariki Tanzania.

KWA namna moja ama nyingine nashawishika kukubaliana na mwandishi huyu,sijui wana Jf mnasemaje?manaake muda mrefu idara hii haijaguswa lakini mambo yanaenda sege mnege
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom