Usafiri wa Anga: Jee Tunaibiwa Au...?!. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Usafiri wa Anga: Jee Tunaibiwa Au...?!.

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by Pascal Mayalla, Feb 28, 2011.

 1. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #1
  Feb 28, 2011
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,565
  Likes Received: 18,309
  Trophy Points: 280
  gWanabodi,
  Kuna hili nimelishuhudia kwenye usafiri wetu wa anga wa kimataifa, ndio maana nauliza ni tunaibiwa, au tunasaidiwa kwa sababu wenyewe hatuwezi?.

  Kwenye usafiri huu wa kimataifa, kila nchi inapewa haki ya international routes na protection ya local routes ili kulinda mashirika ya nchi yasimezwe na mashirika makubwa.

  Katika route ya Afrika Kusini, kuna shirika moja jipya linajiita Com Air linafanya biashara kubwa ya kusafirisha abiria kati ya Dar na J'burg kwa bei poa.

  Nauli ya kawaida ya return ticket ya Dar-J'burg -Dar ni Dola 700 lakini nauli ya Com Air ni Dola 300!.

  Ndege inakuja Dar mara tatu kwa wiki kila Jumatatu, Jumatano na Ijumaa. Inatua saa 7:30 za usiku na kutuka saa 8:30 za usiku, yaani inakuja na kuondoka kama mwizi!.

  Mahali tunapoibiwa ni hapa!. Kumbe hili shirika linalojiita Com Air, sio lolote, si chochote bali ni Ndege ya BA inayotoka London kupitia Dar kuelekea J'burg!.

  Kwa mujibu wa sheria za kimataifa za usafiri wa anga, ndege inayopitia Tanzania kwa utaratibu wa Via, hairuhusiwi kubeba abiria local, inatakiwa kushusha tuu na kuendelea na safari yake badala ya kusanya abiria wa Tanzania kwa nusu bei!.

  Inawezekana wizi huu unafanywa kwa nia njema kwa vile flag carrier yetu ATC haina uwezo wa kupeleka ndege yake ya ngama safari ndefu, hivyo BA imeamua kuokoa jahazi japo kwa kijiita Com Air matokeo yake ni kuwa hata ATC ikifufuka, itaishia kukosa abiria kwa sababu haitaweza kihimili ushindani huu wa nusu bei!.

  Pia ikumbukwe Tanzania hatuna tena ile route yetu ya London bado inahodhiwa na SAA kwa kisingizio cha kifidia hasara iliyosababishwa na Alliance Air!. Sasa hata ATC ikifufuka, itapumulia wapi?.

  Kitu kingine kibaya kabisa hawa Com Air wanachowatendea Watanzania ni menu yao ya ndani ya ndege. Wanatangaza kuwa ni beef lakini menu inayokuja ni sausages za 'mkuu wa meza'!. Masikini wenzetu kwa vile hawawezi kuzijua, hujilia kwa imani beef ya wenzetu ni nyeupe, laini na ina ladha sana!. Japo mimi ni Mkristu lakini hili sio kuwatendea haki wenzetu.

  Nawasilisha.
  Pasco
  Pretoria.
   
 2. kipipili

  kipipili JF-Expert Member

  #2
  Feb 28, 2011
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 1,499
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  Duu mkuu inabidi niwatafute hao com air nije sauzi kutembea manaake nauli bei poa kama vile basi
   
 3. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #3
  Feb 28, 2011
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 308
  Trophy Points: 180
  Hii ni habari nyeti sana na ya kiintelijensia, inayotakiwa KUFANYIWA KAZI mara moja na TCAA.
  Actually kilichotakiwa kufanywa ni kuwashitaki hawa jamaa ili waache mchezo huo, na kuwa severely fined..
  Hairuhusiwi kabisa kupakia abiria enroute!...labda aBiria hao wawe wanaenda kwenye final destination ya ndege hiyo, na si vituo vya VIA...vinginevyo hiyo inakuwa ni daladala, na inapoteza ile sifa maalum ya usafiri wa anga ya fastness , reliability and comfortability..

  Otherwise mashirika yanayo'emerge yasingesimama kwa miguu yao ever!
   
 4. K

  KyelaBoy JF-Expert Member

  #4
  Feb 28, 2011
  Joined: Nov 9, 2008
  Messages: 206
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Asavali hao ni bei poa inabidi tuwapongeza kutoka dolali 700 hadi 300 mungu akupe nini,sasa pasco unacholilia nini hilo shirika letu liko ICU,wacha nasi akina yakhe tukwee pipa ,
   
 5. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #5
  Feb 28, 2011
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,565
  Likes Received: 18,309
  Trophy Points: 280
  KyelaBoy, ndio maana nikauliza kama ni tunaibiwa au tunasadiwa?.
   
 6. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #6
  Mar 1, 2011
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,565
  Likes Received: 18,309
  Trophy Points: 280
  Tena wa bongo hatuhitaji viza. Yaani kuja South na kurudi ni bei poa kuliko kwenda Mwanza au Arusha na kurudi?. Swali sanya sanya za ndege zinaruhusiwa?.
   
 7. Wacha1

  Wacha1 JF-Expert Member

  #7
  Mar 1, 2011
  Joined: Dec 21, 2009
  Messages: 12,766
  Likes Received: 920
  Trophy Points: 280
  Tanzania ndio wajinga wameuza route zote kwa mashirika ya nje kwa sababu hatuwezi kuendesha usafiri wa anga. Mugabe ameweza kuendelea kushika madaraka kwa kutegemea foreign currency kwenye safari za Air Zimbabwe nje ya nchi. Hii ni biashara kubwa sana yaani hii mizoga ya CCM haiwezi hata kufikiria. Wameua ATC, wameua shirika la Reli, wameua shirika la Posta na simu, wameuza viwanda vyote, wanaua taratibu kila aina ya rasilimali ya nchi hii kwa tamaa binafsi. Then wanakuja na kusema kuna watu wanataka kuleta machafuko? Wao wenyewe ndio wanaleta machafuko.

  Ndege zilizonunuliwa na baba wa Taifa baada ya EAC kuvunjika ndio hizo hizo hadi wamezimaliza yaani tulianza tukiwa hatuna kitu na sasa hatuna kitu tena.
   
 8. m

  masssaiboi JF-Expert Member

  #8
  Mar 1, 2011
  Joined: Feb 10, 2009
  Messages: 637
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 33
  Hapo hakuna wizi wowote ila ni kitu kinaitwa strategic alliance, haina tofauti sana na ile ya KQ na KLM na Precision. Unaweza nunua tkt ya klm au precision ukajikuta umepanda KQ.
  Ni njia makampuni yote makubwa yanatumia kukuza masoko yao na kupunguza ushindani.
  Inasaidia pia kukuza makampuni madogo/local mfano precision
   
 9. TANMO

  TANMO JF-Expert Member

  #9
  Mar 1, 2011
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 8,916
  Likes Received: 216
  Trophy Points: 160
  Mkuu madam ATC bado ipo kaburini basi tuendelee kuifaidi hiyo Ofa "isiyo halali" tuliyobahatika kupewa na BA. Ila tukisema tupige kelele ofa ifungwe bado tutakaoumia ni sisi. Unless unajua ni lini ATC itafufuka na una uhakika beyond any doubt kuwa itafufuka kweli kwa sera tulizonazo....
   
 10. Kaizer

  Kaizer JF-Expert Member

  #10
  Mar 1, 2011
  Joined: Sep 16, 2008
  Messages: 24,646
  Likes Received: 1,472
  Trophy Points: 280
  Ila mkuu Pasco apo kwenye beef sausages umetia chumvi sana bana...yaana wajamaa wanazifurahia kabisa ladha yake? hahahah

  Kusema ukweli unapoangalia mashirika ya wenzetu , unajiuliza how long it will take kwa ATC kurudi kwenye its senses....hivi ni lazima kuwa na shirika la ndege la taifa?
   
 11. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #11
  Mar 1, 2011
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,565
  Likes Received: 18,309
  Trophy Points: 280
  TANMO, kweli ATC bado iko ICU, lakini kama ni kusaidiwa, si tusaidiwe basi angalau na Precision!
   
 12. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #12
  Mar 1, 2011
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,565
  Likes Received: 18,309
  Trophy Points: 280
  Kaizer, sijatia chumvi, hizo ni beef sausages jina, ila you can not tell kitu ambacho hujawahi, hebu nenda pale Mlimani City kanunue beef sausages za ukweli na zile nyingine, chemsha halafu kula, utaniambia. Zile nyingine wanazitia spice hivyo za beef ni chamtoto!
   
 13. Anko Sam

  Anko Sam JF-Expert Member

  #13
  Mar 1, 2011
  Joined: Jun 30, 2010
  Messages: 3,216
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  We panda hiyo ya US$ 300 achana na wezi ATC watupu, wala usimwambie mtu.
   
 14. Margwe

  Margwe JF-Expert Member

  #14
  Mar 1, 2011
  Joined: Apr 30, 2008
  Messages: 256
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Hiyo naona inafanana na daladala zisizo na line za masela hapa arusha !Imekuwa komba komba! Hapa bongo hiyo sio issue kabisa na isije ''ikavunja amani na mshikamano'' tulionao na 'wafadhili'(mix with urs):hand:
   
 15. mfianchi

  mfianchi JF-Expert Member

  #15
  Mar 1, 2011
  Joined: Jul 1, 2009
  Messages: 7,940
  Likes Received: 1,498
  Trophy Points: 280
  Du siku hizi 540 na Precision ni kama kampuni za simu,bei ya promo hadi mwanza 98,000 hakika ushindani mzuri precision siku hizi wamepata mpinzani wa ukweli
   
 16. babukijana

  babukijana JF-Expert Member

  #16
  Mar 2, 2011
  Joined: Jul 21, 2009
  Messages: 4,811
  Likes Received: 1,146
  Trophy Points: 280
  wabongo bana mna tabu sana,mmepunguziwa nauli mnataka ipandishwe tena,kisa mmelishwa sausage,yaani kuchamba kwiingi ndio.......... m.vi

  ndio maana dowans wanazidi kuwalamba chenga za mwili kila leo,maana mmekalia porojo tu.

  NB.waandikie hao BA uwaambie hiyo bei ndogo sana hamutaki ipandishwe ili ATC yenu ikirudi ipate wateja,mwee
  MASIKINI AKIZOEA MAHARAGE UKIMPA KUKU NAE ATAGAWA,HAJAZOEA
   
Loading...