Usafi wa mikono baada ya kutoka haja

Usafi wa mikono baada ya kutoka haja

Hivi wakuu hili suala la kwenda haja kubwa, halafu wakati wa kuchamba mtu anashika shika mavi ili kujiosha mnalionaje?

Ukweli ni kwamba wengi wamelishwa mavi. Huwezi kusema wote hujisafisha mikono vizuri na maji ya kutosha na sabuni au ikiwa wote hunawa na sabuni.

Na wengine hujisafisha na maji ya ndoo ya chooni au kopo la chooni linalotumiwa na wengi. Tena utakuta ni maji kidogo sekunde 2 tu mtu kashamaliza kunawa anarudi jikoni au kwenye mgahawa anaendelea kuaanda chakula au kupakulia chakula wateja wake. Hivi kweli kuna usafi unazingatiwa hapo?

Unakuta mmama au dada wa nyumbani ambaye ndiye mpishi wa familia akienda chooni anajisafisha kwa njia hiyo hivi kweli mna uhakika huwa hawawalishi kinyesi walaji?

Ifikie wakati huu utamaduni wa kuchamba kwa kushika shika kinyesi Watanzania waachane nao. Unatia kinyaa sana.
Ongea na wazazi wako kwanza
 
-7dibzy.jpg
Na juice ya miwa mnashushia mikund nyie!!!
 
Mimi ndiyo maana silagi chakula kwa watu au sehemu nisiyoielewa elewa
 
Limbukeni huyo kaenda Ulaya amekuta wanatumia toilet paper na wao kutumia maji ni uchafu mkubwa ndio ka copy na kuweka hapa hata South Africa ukitumia maji watakuona hivo..limbukeni wa kuiga tu huyo,huko kijijini kwao kuna hizo toilet paper??
Toilet paper huwa sizielewi kabisa, maji ndo unyama.
 
Tissue za fine😀😀😀vinaacha pumba kabisa...
Kuna jirani zetu wanaotumia tissue hunuka kimavi.

Mwendo mmoja tu maji yanayotililika ya kutosha,fanya choo chako kiwe pahala safi,uchafu ni jadi yetu sio chooni tu.
Maofisini unakuta watu ni PhD holders na watu warembo haswa vyooni kama jalala vile😀😀

Hata majumbani kwetu vyoo vya watu ni vichafu kupita maelezo.

Mkuu naungana na wewe kuwa na ratiba na adabu kuhusu kunya sio kunya hovyo hovyo kama bata.
Hahaha Kama Bata haitakiwi kabisa.
 
Binafsi choo cha ugenini kinanipa ugumu sana kukitumia labda kiwe na mazingira mazuri zaidi ya kwangu ila vinginevyo siendi

Nakumbuka nilienda kijijini kusalimia sikujisaidia mpka nilipofika mjini ndani ya siku mbili najikaza tu
Kabisa, ugenini na sehemu za public kujisaidia ni mtihani sana.
 
Ndio maana kuna baadhi ya watu hawali kachumbari, kwasababu ya haya masuala ya usafi ,Mtu katoka kushika kinyesi kwa mikono kanawa bila sabuni halafu anaenda kukata kachumbari,kibaya zaidi mkono ulioshika kinyesi ndio unaoshika nyanya kitunguu kabeji hoho nk
 
Shattaf huwa haimalizi uchafu wote, toilet paper pia
ili ujisafishe vizuri lazima utumie maji na mkono kujisafisha
 
Back
Top Bottom